MUSOMA, MARA: Ambulance ya Hospitali ya wilaya Tarime yakamatwa ikisafirisha shehena ya mirungi

Ambulance ya hospitali ya Wilaya ya Tarime ambayo imekamatwa na Inspekta Nathaniel pamoja na timu yake usiku huu huko Bunda ikiwa imebeba Magunia ya Mirungi kama inavyoonekana wengine ni watuhumiwa akiwemo dereva wa gari hilo.




Picha tu tosha, inaonekana watuhumiwa wote ni wavutaji mmea haramu. Tarime kweli kuna kazi kuishi kule.....Dar nako hakukaliki kutokana na kuzungukwa na wanaume tata. Ngoja nikaombe ombe Dodoma kama ndugu zangu Wagogo.
 
kuna mtu kachoma utambi hapo. sio rahisi ambulance kupigwa mkono juu king'ora na taa full hapo kuna kusalitiana/kudhuluniana mzigo/kutokuelewana kwenye malipo n.k
Dereva alifanya Kosa kubwa kusimama yeye angetembea tu
 
Tatizo lingine ni kwamba hawa madereva wamepewa mamlaka makubwa sana na hizo ambulance,,,, unakuta dereva ana sauti kuliko hata mganga mkuu........ ndio maana wanatumia vibaya magari ya wagonjwa.


ifike mahali madereva wawe wanawajibika moja kwa moja kwa mganga mkuu.

Unakuta wanajiendeshea wanavyotaka
 
Sawa ajali kazini ila ajali nyingine za kujitakia kama hizi
ajali kazini, kujitajilisha kwenye mali ya uma ndio sawa mambo ya kudhurumu watu binafsi wenye kipato cha kuunga unga haifai

Ukipata nafasi kwenye umma iba tu, wao mbona wanasaini mikataba inayo tuua sisi (umma) kwa manufaa yao.
 
Back
Top Bottom