Musoma: Akamatwa kwa tuhuma za kuwalewesha abiria Dawa ya Congo na kuwaibia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Polisi mkoani Mara inamshikilia mkazi wa kijiji cha Rugasha Bukoba Vijijini, Marco Saidi (68) kwa tuhuma za kuwalewesha abiria kwenye mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mwanza-Musoma na kuwaibia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kituo cha mabasi wilayani Bunda mkoani Mara baada ya kumywesha abiria mmoja.

Kamanda Tibishubwamu amesema kuwa mtu huyo anadaiwa kuwalisha na kuwanywesha abiria dawa za kienyeji zinazojulikana kwa jina la khabharagata kutoka nchini Congo kwa lengo la kuwalewesha abiria na kuwaibia mali zao.

Amesema mtu huyo akishirikiana na watu wengine watano (bado hawajakamtwa) wamekuwa wakiwanywesha abiria dawa hizo kwa kuziweka kwenye maji au soda na kupaka kwenye biskuti au pipi kisha kuwapa abiria ambao baada ya kunywa ujikuta wamelewa na kupoteza fahamu.

"Walikuwa wanaweka kwenye kinywaji au anapaka kwenye shati lake eneo la mkononi kisha anasubiri abiria akishakaa yeye anapitisha mkono kama anafungua au kufunga dirisha wakati huo mkono wake anauelekeza kwenye pua ya abiria hivyo abiria anajikuta amevuta hewa baada ya hapo mtu analewa na kupoteza fahamu au anakupa pipi ama biskuti ukila unalewa kisha anaiba na kushuka kabla hajagundulika" amesema.


Mwananchi
 
Jeshi la Polisi Mara lamkamata Abdul Said (68) mkazi wa kijiji cha Rugasha Katoro mkoani Kagera kwa tuhuma za kuwalisha abiria ndani ya mabasi dawa za kienyeji zinazojulikana kwa jina la 'khabharagata' zinazoagizwa kutoka Congo ambazo huwalewesha abiria na kisha kuwaibia.

Chanzo: itvtz

Yaani Watani zangu wakubwa Wahaya mna matatizo sana. Aliyewadanganyeni kuwa Watu wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) huwa tunaibiwa hovyo na 'Kizembe' namna hii nani?

Kwahiyo Watani zangu wakubwa Wahaya mmejisahaulisha kwa makusudi kuwa Tanzania nzima Watu Wajanja, Makini na wenye Machale ya Kutoibiwa au Kukumbwa na Hatari yoyote ( Balaa lolote ) wanapatikana ( wanatokea ) Mkoani Kwangu GENTAMYCINE wa Mara?

Sasa Adhabu pekee ambayo wana Mara ( wana Mkoa wa Mara ) tunawapeni Watani zetu wakubwa Wahaya ili tumuachie huyu 'Kibaka' na arudi Bukoba ( Kagera ) Kwenu ni Kuwahitaji Wanawake wote wa Kihaya wake upesi Mkoani Mara ( Musoma ) tuwabebeshe Mimba zetu kisha warudi Kuzalia huko Watoto wetu ambao wataleta mabadiliko Mkoani Kwenu na kuwafanyeni muwe Mashujaa, Werevu na Wachapakazi ili muachane na hulka hizi za Uwizi Uwizi.

Watani zangu Wahaya mpo? Mtanikoma!
 
Hii kweli Kuna dogo nilimzaba makofi nilimsajiria line ya simu ili atunze pesa zake Sasa yeye aliweka sijui mfukoni akapanda basi kutoka babati akafanyiwa hivyo na kuibiwa laki sita inasikitisha sana
 
Amesema mtu huyo akishirikiana na watu wengine watano (bado hawajakamtwa) wamekuwa wakiwanywesha abiria dawa hizo kwa kuziweka kwenye maji au soda na kupaka kwenye biskuti au pipi kisha kuwapa abiria ambao baada ya kunywa ujikuta wamelewa na kupoteza fahamu
🐕‍🦺
 
Musoma wakati Jeshi la Polisi likimshikilia Marco Saidi (68) mkazi wa Kijiji cha Rugasha Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa tuhuma za kuwalewesha abiria kwenye mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mwanza- Musoma na Sirari kisha kuwaibia, mmoja wa waathirika asimulia.

Mwathirika huyo, Maulidi Omary aliliambia gazeti hili juzi kuwa alijikuta Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara akiwa amelazwa baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa siku tatu.

Omary anasimulia kuwa, Novemba 27 mwaka huu alipanda basi kutoka Mwanza kuelekea Musoma, dakika tano baada ya kupanda aliingia mzee mmoja aliyekwenda kukaa pembeni na kiti alichokuwa amekalia.

Omary alisema hakuwa na wasiwasi wowote kwa kuwa alijua ni abiria na baada ya muda kidogo safari ya kuelekea Musoma ikaanza.

Alisema muda wote alikuwa na chupa ya maji aliyokuwa akinywa taratibu. “Tulipofika Magu nilishuka kwenda kujisaidia na kuacha maji yangu kwenye basi, niliporejea nilikunywa yale maji kwa kuwa sikuwa na wasiwasi wala hofu yoyote, baada ya dakika tano hivi, nikaanza kuhisi usingizi, lakini nikajua ni usingizi tu wa kawaida,” alisimulia Omary ambaye ni mfanyabiashara.

Alisema muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo alivyozidi kupata usingizi mzito.

Omary alisema anakumbuka walipofika Nyashimo abiria mwenzake alipitisha mkono karibu na pua yake hali iliyomfanya ashtuke kutoka usingizini.

Nilimuuliza vipi bwana akajibu nilikuwa nafungua dirisha nikamuuliza sasa mbona umepitisha mkono mpaka puani, akasema samahani baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi nilipojikuta hospitalini,” alisema Omary.

Alisema katika tukio hilo alipoteza simu zake mbili, fedha na vitambulisho.

Jeshi la Polisi lazungumza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu alisema Saidi na watu wengine, wanadaiwa kuwalewesha abiria kwa kutumia dawa za kienyeji zinazoitwa ‘Khabagarata’ ambazo huziagiza kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) mahususi kwa kazi hiyo.

Kamanda Tibushubwamu alidai juzi kuwa, Saidi alikamatwa Desemba 2 mwaka huu katika Kituo cha Mabasi Bunda baada ya kudaiwa kumlewesha abiria kisha kujaribu kutoroka.

Vitendo hivyo vya kulewesha abiria kwenye mabasi yanayotoa huduma kupitia njia hizo vinadaiwa kuanza kukithiri Oktoba mwaka huu na hadi sasa zaidi ya matukio matano yameripotiwa polisi.

Kamanda Tibushubwamu alisema mbali na kumshikilia mtu huyo, jeshi linawasafirisha watuhumiwa wengine wawili kutoka Kagera kuja Musoma wanaodaiwa kumlewesha na kumuibia abiria Sh3 milioni kwenye meli.

Alisema watuhumiwa hao ni miongoni mwa watu ambao jeshi lilikuwa likiwasaka na kuweka mtego baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa wanamtandao wa uhalifu huo.

Kamanda Tibushubwamu alisema baada ya mahojiano na Saidi, alikiri kushiriki vitendo hivyo huku akisema upo mtandano wa watu wengi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo vya kuibia abiria baada ya kuwalewesha.

Huyu mtu amesema kuwa ingawa yeye ni mzaliwa wa Kagera lakini makazi yake hivi sasa yapo Nairobi, Kenya kwa hiyo huku anakuja maalumu kwa ajili ya huu uhalifu wake ambao amekuwa akifanya kwa muda mrefu,’ alidai Kamanda Tibushubwamu.

Pia, alisema katika uchunguzi wao wamebaini vitendo hivyo vya kuwalewesha abiria vimekuwa vikifanywa na mtu huyo pamoja na washirika wake kutoka mikoa Mara, Mwanza, Simiyu, Kagera na Dar es Salaam na hata nje ya nchi ikiwamo Kenya.

Alisema mtu huyo amekuwa akiwanywesha au kuwalisha abiria dawa hizo kupitia soda, juisi au maji pamoja na kupaka dawa hiyo kwenye biskuti au pipi.

Wana njia nyingi sana tofauti na kwenye soda, maji, pipi na biskuti, sasa hivi wamegundua njia nyingine ya kuipaka kwenye shati eneo la mkononi.

Mkishakaa anapitisha mkono wake kama anataka kufunga au kufungua dirisha wakati huo anahakikisha amemuelekezea kwenye pua abiria ambaye hujikuta amevuta ile dawa kwa njia ya hewa, baada ya muda analewa na kupoteza fahamu, ndipo jamaa anatimiza lengo lake,” alisema Kamanda Tibushubwamu.

Alisema watu ambao wameripotiwa kunyweshwa dawa hiyo wamekuwa wakilewa na kupoteza fahamu kati ya siku moja hadi tatu na wengi wao hukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Wakati Kamanda Tibushubwamu akisema hayo, Jeshi la Polisi Simiyu na Mwanza limesema hawajapata taarifa zozote kuhusiana na matukio hayo ndani ya mikoa yao.

Mkoani Mwanza hatuna tukio lililoripotiwa la mtu kunyweshwa au kuleweshwa kwenye mabasi lakini niseme tu tunachukua tahadhari,” alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi kwa njia ya simu.

Akizungumzia uhalifu wa namna hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda alisema upo uwezekano wakazi wa mkoa huo kufanyiwa vitendo hivyo.

Mtu anaweza kufanyiwa hivyo akiwa Simiyu, lakini madhara yakatokea kadri safari inavyoendelea, sisi baada ya kusikia jambo hili tulianza mara moja kuchukua tahadhari, tunawaelimisha abiria kuchukua tahadhari,” alisema Kamanda Chatanda.

Baadhi ya maderava na makondakta wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtuhumiwa mmoja huku wakiomba jeshi hilo kuongeza jitihada zaidi ili mtandao wote uweze kukamatwa.

Walisema matukio kama hayo yamekuwa yakiathiri biashara yao kwa kuwa wanakuwa hawana amani muda wote wa safari, hali inayoweza kuwa kikwazo katika kazi zao.

Ingawa hatujapata taarifa za kifo chochote kutokana na hali hii, ni vema suala hili likapatiwa ufumbuzi mapema kabla halijaleta madhara makubwa kwenye biashara zetu au hata uhai wa mtu,” alisema Jonathan Magige, ambaye ni kondakta wa basi linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Musoma.

Magige alisema watu hao wanaojihusisha na vitendo hivyo wamekuwa wakibuni mbinu tofauti ili kufanikisha uhalifu wao.

Alisema ni vigumu kuwatambua watu hao kwa kuwa wamekuwa wakiingia kwenye mabasi kama abiria wa kawaida kwa nia ya kufanya uhalifu.

Unakuta wanaingia hata watano na wanakaa sehemu tofauti na hapo unakuta tayari wameshamuona mtu wanayehisi na pesa au kitu chochote cha thamani, kwa hiyo wanahakikisha wanamuweka kwenye ‘target’ yao,” alisema Magige.

Alisema ili waweze kufanya uhalifu wao bila kushtukiwa ni lazima mtu wanayetaka kumfanyia uhalifu huo akae dirishani ili kuepuka kugundulika na hata ikitokea amelewa au kupoteza fahamu asianguke, badala yake aegemezwe kwenye gari upande wa dirisha.

Magige alisema watu hao mbali na kuwalewesha abiria wanatembea na vifaa kadhaa, zikiwamo nyembe ambazo hutumika kuchana mifuko ili iwe rahisi kwao kuchukua vitu wanavyovihitaji kwa urahisi bila kugunduliwa.

Kondakta mwingine, Adriano Buzinza alisema mara nyingi abiria huleweshwa wakiwa wanatoka Mwanza, huku wengi wao wakibainika baada ya basi kufika mwisho wa safari.

Buzinza alisema jinsi wanavyokuwa wamelala kwa kuegeshwa inakuwa vigumu kugundua kama kuna shida.

Mara nyingi watu wananyweshwa wakiwa wanatokea Mwanza, kwa hiyo mkifika mwisho wa safari ndipo unapogundua kuwa kuna mtu amepata shida baada ya abiria wote kushuka na mwingine kubaki,” alisema Buzinza.

Alisema linapotokea tatizo kama hilo wanakuwa hawana cha kufanya zaidi ya kumfikisha mwathirika kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi, ikiwamo kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Maneno Baraka, ambaye pia ni dereva wa basi alisema kutokana na hali hiyo wanajitahidi kuchukua tahadhari ili kuwanusuru wateja wao na kadhia hiyo.

Alisema tayari uongozi wa Serikali umeshatoa maelekezo na mwongozo wa nini cha kufanya, ikiwamo kuwatangazia abiria mara kwa mara kuchukua tahadhari wawapo safarini.

Mara kwa mara tunawatangazia abiria kutomuamini abiria mwenzake waliyekutana ndani ya basi, tunawaambia waepuke kupokea na kutumia vitu kama soda, pipi, biskuti, karanga, maji na juisi kutoka kwa abiria wenzao kwa kuwa huwezi kujua nani ni nani,” alisema Baraka.

Alisema wameanzisha utaratibu wa kukagua mara kwa mara kwenye basi kuangalia kama abiria wote wako salama ili kuepuka kwenda mwendo mrefu na abiria aliyepoteza fahamu.


Madaktari wanasemaje?
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Juma Mfanga alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana takwimu sahihi.

Ni kweli tatizo lipo lakini siwezi kuongea chochote mpaka nikusanye taarifa kutoka kwa watu wangu, labda unitafute wiki ijayo naweza kuongea chochote,” alisema Dk Mfanga.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tarime, Innocent Kweka alisema ili kuweza kujua madhara ya kiafya ambayo mtu aliyenyweshwa au kulishwa dawa hizo ni lazima kufanywe vipimo.

Kwa hospitali ya Tarime sijapata kesi kama hii, lakini kuhusu madhara ya kiafya ni lazima sampuli ya damu ya mwathirika ichukuliwe na upimaji ufanyike kujua ni aina gani ya dawa, ndipo unaweza kujua madhara ya kiafya, tofauti na hapo huwezi kujua,” alisema Dk Kweka.


Kauli ya DC
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Halfan Haule alisema baada ya kupokea taarifa ya matukio hayo waliamua kutoa taarifa ngazi ya juu ili kudhibiti hali hiyo.

Alisema mbali na kutoa taarifa ngazi za juu, ofisi yake ilitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili liweze kufuatilia suala hilo kisheria.

Alisema pia elimu imekuwa ikitolewa kituo cha mabasi ili kuepuka kufanyiwa vitendo hivyo kila baada ya dakika 15 tangazo la abiria kuchukua tahadhari linatolewa.



Wananchi wazungumza
Magreth Masanja ambaye ni mfanyabiashara katika kituo cha mabasi Musoma alisema mbali na kuwathiri kiafya waathirika, vitendo hivyo vinawafedhehesha.

Alisema mtu anapokuwa amelewa kabla ya kupoteza fahamu yapo mambo mengi wanayofanyiwa ambayo yanashusha utu wake.

Kuna siku mzee mmoja alishuka hapa inaonekana alikuwa ndo amemaliza labda kunyweshwa dawa hizo, sasa akawa kama mlevi wa pombe, watu wakaanza kumzonga wanamwambia amelewa mara wengine wanamdhihaki wakijua ni ulevi hadi alipojitokeza mtu anayemfahamu akasema kuwa huyo baba huwa hanywi pombe,” alisema Magreth.

Mkazi wa Musoma, Angel Mwita alisema kufuatia matukio hayo hivi sasa wafanyabiashara wengi wamekuwa waoga kusafiri kufuata bidhaa Mwanza wakihofia kuibiwa fedha na mali zao.

Chanzo cha habari: Mwananchi
Imetayarishwa na: Beldina Nyakeke

images (6).jpeg
 
Back
Top Bottom