Music Industry: Kenya Vs Tanzania

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,727
10,023
Kwenye nyanja mbalimbali kenya wametuacha sana lakini nini tatizo kubwa linalofanya muziki wa Kenya usifanye poa kuliko wa Tanzania kwenye mziki wao?

Tz pamoja na kutumia zaidi Swahili katika nyimbo zetu tofauti na majirani Kenya wenye kutumia lugha zaidi ya moja; bado angalau katika soko la mziki barani Afrika huwezi kukosa bongo fleva itokayo Tz.

Ukienda kwenye trendin' nchini kenya kati ya wasanii 10 Bora 6-7 ni kutoka Tanzania.

Huku Tanzania kwenye trendin' ya angalau 10 bora unaweza kuta artist wa kwenya 1-2 au non kabisa😁 kutoka Kenya.

Ndugu zetu Wakenya tatizo nini tujuzane.
 
Wasanii wa tanzania wako vizuri katika kutafuta melodies za mziki wao tofauti na wakenya.. Hapa nazungumzia producers na artist wenyewe..

Wasanii wa Tanzania pia wanasauti za ki-music tofauti na wakenya

Halafu tanzania tunafanya aina mbalimbali za Muziki tofauti na kenya...

Wasanii wa Tanzania pia upande wa choreography wako vizurii
 
Wasanii wa tanzania wako vizuri katika kutafuta melodies za mziki wao tofauti na wakenya.. Hapa nazungumzia producers na artist wenyewe..

Wasanii wa Tanzania pia wanasauti za ki-music tofauti na wakenya

Halafu tanzania tunafanya aina mbalimbali za Muziki tofauti na kenya...

Wasanii wa Tanzania pia upande wa choreography wako vizurii
Kuna wasanii kenya wanaweza kufanya yote hayo wanayofanya watz kama akina otile, Nadia, Nasipendei, Bahati , Sauti sol wangeweza kuwa funguo. Lkn ninachoona ni kwamba wakenya shida ni moja hampendani.
 
I like the idea of this thread. As someone who sometimes moonlights in the music biz...I'd like us to talk about managers/promoters publishing rights, freedom of creativity and nature vs nurture in terms of developing artists of different genres
 
Nachokubali kenya ni kuwa ina ma producers wazuri sana japokua ni wachache kinachowakwamisha tu ni kitu kimoja ni selfishness ambacho wanacho hata wasanii....

Pia ina DJs wengi wenye skills wengine wamefika mbali zaidi kimataifa compared na huku mwetu TZ pia wana umoja sana tofauti na wa kwetu na wanasaidiana sana DJs wa Kenya..

Tatizo lao ni moja kwenye muziki wamebase kwenye local market sana, na nyimbo zao ni kama za aina moja, hawataki kuendana na kasi ya usasa katika muziki, Japokua wanaoimba HipHop/Trap wanajaroibu usasa kina Kaligraphy Jones n.k napenda sana HipHop/Traps za Kenya..
 
Back
Top Bottom