Musiba: 70% ya mawaziri wa Magufuli ni mizigo

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,515
21,541
Akiongea katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI leo kupitia televisheni ya Star TV, kada maarufu wa CCM, Bwana Cyprian Musiba, amesema kwamba 70% ya mawaziri wa serikali ya Magufuli ni mizigo. Hivyo, amemshauri Rais Magufuli kuwatumbua haraka iwezekanavyo.

Akiongea kwa hisia kali, kada huyo amemtaka Magufuli kuwafuta kazi mawaziri hao hata ikiwa ni ndani ya wiki moja baada ya kuwateua.

Aidha, kada huyo alidai kwamba 80% ya wananchi wanaolia maisha magumu yaliyosababishwa na utawala wa Rais Magufuli ni wanaCCM.

Kwa sababu hizi alizozitaja kada huyo wa CCM, amemshauri Rais Magufuli kuwafuta kazi mawaziri hao na kuwafuta uanachama wanaCCM wote wasiokubaliana na utawala wake.
 
Acheni maneno fanyeni kazi . Tufanye kwanza yetu
 
Kusema tu kuwa mawaziri ni mizigo bila kueleza ni mizigo kwa vipi na kushauri mawaziri wasio mizigo waweje haina tija, kwani yawezekana yeye ndio yupo nyuma ya wakati na ana matatizo akafikri wenzake ndio mizigo
 
Back
Top Bottom