Museven : Trump kushinda urais ni matokeo ya laana ya Afrika kwa Marekani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1480084878858.jpg
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema ushindi wa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani kupitia uchaguzi uliopita umetokana na laana ya afrika na mashariki ya kati kwa taifa hilo

Kupitia tamko lake lililosambaa kwenye vyombo vya habari ikiwa pamoja na BBC, Rais Museveni amesema kuwa kwa kipindi kirefu Marekani, Uingereza na nchi marafiki zao wamekuwa wakikandamiza mataifa ya Afrika na Mashariki ya kati, hivyo wamepata pigo la laana ya kisiasa

"Ingawa kuna sababu nyingine ambazo sisi watu wa nje hatuwezi kuzifahamu kirahisi, kuna sababu moja ambayo imebadilika kuwa laana kwa mataifa haya makubwa (Marekani na Uingereza) "ameandika

Amesema Marekani imepata laana ya kisiasa kutoka kwa mataifa ambayo ilianzisha vita isiyo na msingi dhidi yake, Alizitaja vita ziliyoratibiwa na Marekani dhidi ya Iraq na Libya kuwa haikuwa za haki

Aliongeza kuwa laana ya hizo ndizo zilipelekea pia aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kupata janga la kujiuzulu baada ya wananchi wake kuamua kujiondoa katika umoja wa Ulaya kupitia kura za maoni, huku Marekani Hillary Clinton akishindwa uchaguzi

"Iwe iwavyo, waliochangia mshambulizi mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika, waliibua majanga na laana ambazo zilipelekea kuangushwa kwa Clinton na Cameron,"linaeleza tamko la Museveni

Museveni ni mmoja kati ya marais wa Afrika ambao walimpongeza Trump kwa kushinda uchaguzi wa Urais na kuwa Rais Mteule wa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani.

Chanzo : Dar24
 
Nitafurahi sana museveni aki. aki. aki,
Nimepatwa na kigugumizi mnisamehe, nisaidieni kuimalizia sentesi yangu.
 
Na kama angeshinda Hilary museveni angesema kuwa ni Baraka kutoka wapi?marais wengi wa afrika wanatakiwa kuandikishwa chekechea! Alivyo kumbafu badala ya kuongea kabla ya uchaguzi yeye anaropoka sasa hivi wakati tayari keshatuma na salamu za pongezi kwa huyo huyo mlaaniwa!pathetic
 
mtu aliye kwenye madaraka zaidi ya miaka 28 anaongelea uchaguzi wa marekani. Haya bwana
 
mtu aliye kwenye madaraka zaidi ya miaka 28 anaongelea uchaguzi wa marekani. Haya bwana
Dalili kwamba.. nyani huoni kundule, kule kung'ang'nia kiti kwa baadhi ya viongozi wa Afrika ni laana tosha pia
 
Anaijua haki huyu shetani toka lini, kila siku anatesa mpinzani wake kisiasa kama vile siyo binadamu.

Asitufanye sisi kama hatuoni ujinga wake
 
Back
Top Bottom