Museveni: Tangu niifunge Facebook hatujawahi kukosa Sukari wala Nguo. Sijutii, wao sio Mungu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Kwa mara nyingine tena Rais Yoweri Museveni ameishutumu kampuni kubwa ya teknolojia ya mawasiliano Facebook kwa kuwa na upendeleo dhidi ya chama tawala cha Uganda na wafuasi wake.

Matandao huo wa kijamii ulifunga akaunti kadhaa zenye uhusiano na chama cha National Resistance Movement (NRM) siku kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Januari, ikizituhumu kuhusika katika uratibu wa mienendo isiyo ya kuaminika katika jaribio la kushawishi mdahalo wa umma kabla ya uchaguzi huo.

Wakati huo Bw Museveni aliishutumuFacebook kwa "majivuno " na akatangaza kupigwa marufuku kwa mtandao huo. Hadi sasa mtandao huo haupatikani nchini Uganda isipokuwa kwa kutumia mtandao wa) Virtual Private Network (VPN

Katika mkutano wa Jumapili na "waathiriwa wa Facebook" – Wajumbe wa NRM ambao akaunti zao zilifungwa-rais aliwaambia wako vyema bila mtandao huo.

"Tangu Facebook iondoke, mliwahi kusikia kuna uhaba wa sukari mjini? Hamna nguo ? Facebook itaongea lakini tutasonga, wao sio Mungu ,"Bw Museveni alisema.

Aliongeza kuwa: ‘’Hii ndio sababu katika baahdi ya nchi hawaruhusiwi, je wanafanya kazi Uchina? Tuachane na hayo, kile nilichosikia ni kwamba Mungu yupo kila mahali, kila mahali na anafahamu kila kitu. Sijawahi kusikia kwamba Facebook iko katika kitengo hicho."

BBC
 
Yeye hajakosa sukari wala nguo, wengine wamekosa umbeya na furaha katika maisha yao ya kila siku as well as ku-like na kujumuika na watu wao.

Tusipende kupangiana maisha, yeye kukusanya kodi tu haitoshi hadi kuingiliana faragha na kupangiana jinsi ya kuishi, hio ni definition fupi ya Dictatorship.
 
M7 a master mind, kyagulany haikuwa saiz ya m7, mpaka Sasa hana mpinzani labda miaka kumi ijayo.pengine umri unaweza ukawa agenda ya kumpumzisha,na ikawa na mashiko.
 
Habari za muda huu ndugu zangu,

Ngoja niende kwenye point natafuta mtu mwenye connection ya kupata vyuo Uganda au hata mashirika ya kusaidia kupata chuo huko. Mfano niliongeaga na education link ila wao waliniambia wanasaidia kutafuta chuo nje ya E. AFRICA ila ndani ya E. Africa wao hawawezi.

Naombeni msaada wa kupata shirika au hata mtu atayeweza nisaidia kupata chuo Uganda. Nomba msaada wa chuo chochote cha goverment course medical doctor matokeo yangu ya A LEVEL CHEM C BIOS C PHY S

Asante sanaa
 
Back
Top Bottom