Museveni: Naendelea kufikiria chanjo nzuri ya kuchoma

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872

m

Rais wa Uganda' Yoweri Museveni amesema bado anaangalia ni chanjo ipi atakayochomwa, siku chache baada serikali yake kuanza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa wananchi.

Tayari marais wengine barani Afrika wameonesha kwa umma wakipata chanjo ili kuhakikishia usalama na ubora wa chanjo.

Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutosha ". Aisema mke wake, Janet Museveni,pia bado hajapata chanjo hiyo.

Mwezi uliopita Waziri wa afya wa nchini humo Jane Aceng , alikanusha taarifa kuwa rais na watu wake wa karibu walikuwa wanapokea chanjo nyingine kwa siri kabla ya taifa hilo kupokea chanjo rasmi.

Alitoa ufafanuzi baada ya gazeti la nchini humo la Daily Monitor na gazeti la Marekani la jarida la Wall Street.

Aidha rais Museveni amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kwa kuandika barua kwenye kurasa ya mbele ya gazeti au atawafuata.
Uganda ina mpango wa kutoa chanjo kwa 49.6% ya idadi ya watu katika awamu ya kwanza.

Nchi hiyo imepokea dozi 864,000 za chanjo kutoka Covax mapema mwezi huu na inatarajia kupokea nyingine 2,688,000 mwishoni mwa mwezi Juni.
 
Nchi za kiafrika bana kauli ilipaswa iwe.

Wataalamu wetu wapo katka hatua za mwisho kupata chanjo bora dhidi ya huu ugonjwa ktk maabara yetu ya kisasa iliyopo hapa nchini.
 
Habari za muda huu ndugu zangu,

Ngoja niende kwenye point natafuta mtu mwenye connection ya kupata vyuo Uganda au hata mashirika ya kusaidia kupata chuo huko. Mfano niliongeaga na education link ila wao waliniambia wanasaidia kutafuta chuo nje ya E. AFRICA ila ndani ya E. Africa wao hawawezi.

Naombeni msaada wa kupata shirika au hata mtu atayeweza nisaidia kupata chuo Uganda. Nomba msaada wa chuo chochote cha goverment course medical doctor matokeo yangu ya A LEVEL CHEM C BIOS C PHY S

Asante sanaa
 
Back
Top Bottom