#COVID19 Rais Museveni: Mungu ana kazi nyingi, hawezi kuwa tu hapa Uganda akiwaangalia wajinga

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,367
2,217
Mseven adressing the nation

2020_04_19_22.44.14.jpeg

======


















Rais Yoweri Museveni amewaonya wananchi wanaoenda kinyume na taratibu wakati huu wa vita dhidi ya #CoronaVirus akisema, Mungu ana kazi nyingi na hawezi kuwa Uganda tu akiwaangalia wajinga

Ameongeza kuwa Mungu amewalinda na hakuna kifo mpaka sasa, lakini anahitaji kuwaangalia watu wengine walio katika wakati mgumu

Amesema wamepewa taarifa za kutosha ili kujua namna ya kujilinda na kama watu hawafuati maelekezo, Mungu na Serikali hawawezi kulaumiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu huwa hawajielewi.

Mchezaji wa mpira anaulizwa jinsi timu yao ilivyojiandaa, anakujibu, "Watanzania mtuombee ili tupate ushindi". Unajiuliza, hivi hao unaoenda kushindana nao ni viumbe wa shetani?

Fikra hizo ndizo zinazotufanya kuacha kutimiza wajibu wetu, na kukimbilia kumtaka Mungu atufanyie miujiza. Mungu hamwigi neema hewani bali kwenye kile unachokifanya.
 
Ukitaka kumwelewa Mseven angalia graph yake ya corona inavyopendeza


Period uganda ina mafanikio makubwa sana juu ya vita dhidi ya corona

Screenshot_20200418-091210.png
 
Huyo jamaa amekomaa madarakani, anajua wajibu wake kwa anaowaongoza, huku kwetu bado tunaijaribu ofisi, kazi yenyewe ngumu kweli tunaomba Mungu muda uishe tuondoke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waganda kuanzia Wananchi hadi viongozi wanajitambua linapokuja suala la kupambana na maradhi hasa makubwa, yenye kusababisha vifo na ya mlipuko. Walipambana sana hadi wakaudhibiti UKIMWI kwani walikua wakiongoza barani Afrika kwa wingi wa maambukizi

Kwa uelewa wao kuhusu magonjwa ya mlipuko najiuliza hii twitter ya M7 ilikusudia wananchi wa Uganda tu au inavuka hadi nje ya mipaka ya Uganda?
 
Ukitaka kumwelewa m7 angalia graph yake ya corona inavyopendeza


Period uganda ina mafanikio makubwa sana juu ya vita dhidi ya corona
Mafanikio ya Uganda katika maeneo mengine, kama uchumi nako hayako nyuma.

Kenya anaanza kulia, anazuia bidhaa za Uganda zisiuzwe kwake akijua wote wamo kwenye jumuia moja.

Uganda imekuwa mteja mkuu kwa Kenya miaka yote, sasa kibao kinabadilishwa, Kenya anagoma.

Hapa JF hakuna anayeangalia wala kusema chochote kuhusu hiyo 'graph'; ambayo ndio ujumbe mhimu zaidi kuliko hadithi nyinginezo hapa..

Je, ya kwetu ikoje?
Kwanza ipo? Takwimu zenyewe tunaweka kama za kiwiziwizi hivi!

Naisikitikia sana nchi yangu hii!
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom