Museven awaita viongozi wa Mataifa ya ulaya na Mahakama ya ICC wapuuzi

the ultimatum

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
402
114
Navutiwa na kujiamini kwa Museven rais wa Uganda wa kuwaeleza mataifa ya ulaya kuwa waache kuwaonea viongozi wa mataifa ya Afrika. Ameyasema hayo leo tarehe 12/12/2014 nchini Kenya kwenye maazimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Kenya.

Amesema wazi kuwa ni wapuuzi na waache upuuzi wao wa kulikandamiza bara la Afrika na viongozi wake. Amesema hafurahii ukiukwaji wa haki za binadamu popote pale duniani lakini hafurahii pia kuona ukiukwaji huo unapewa uzito zaidi kwa viongozi wa Afrika na kuwaacha wao wa Ulaya.

Akipongeza kufutwa kwa kesi iliyokuwa ikimkabili Uhuru Kenyatta rais wa Kenya, alisema anawashangaa wapuuzi wa Ulaya kuhusu kesi ya Uhuru Kenyatta kwani viongozi wote wa Afrika walikutana na kuazimia kuwa Uhuru aachiwe hadi pale muda wake wa utawala utapoisha lakini walikaidi na hatimaye leo wamemuacha huru.

Amewaita wapuuzi na amelitumia neno hilo la kuudhi kwa takribani mara 15. Kama ambavyo alionya juu ya Ushoga hapa pia hakumung'unya maneno. Tanzania tunawakosa viongozi wa namna hii wa kuthubutu.
 
Back
Top Bottom