Murambi memorial genocide, tumuombe Mungu atuepushe na majanga ya vita vya ndani

godson njamakuya

Senior Member
Mar 6, 2021
170
195
Wakati mauaji ya kimbari yanatokea nchini Rwanda mwaka 1994-95, nilikuwa Arusha nikijishughulisha na ufugaji na kilimo huku nikifuatilia kwa karibu kupitia BBC na kwenye magazeti kilichokuwa kinajiri huko Rwanda, ilikuwa huzuni kuona picha za matukio jinsi miili iliyouawa kwa kukatwa mapanga ilivyokuwa imezagaa mitaani, kuna jamaa yangu alikuwa anafanya kazi mpakani mwa Tanzania na Rwanda, (Rusumo border) anasema alikuwa akishuhudia miili kama kumi ikiwa imetungwa kama mishikaki kwenye jiti ikipita kwenye maporomoko ya Rusumo.

Ilikuwa haipiti siku bila kuona maiti zikipita katika maporomoko hayo. Ndipo raia wakaanza kuikimbia nchi yao na kuingia nchini kwetu na kupewa hifadhi eneo la Benaco, pale Ngara. Mwaka 2011 nilibahatika kwenda Rwanda kushiriki kwenye zoezi la Nchi za Afrika ya Mashariki, nilifurahia sana mandhari ya Rwanda, kuanzia unapovuka mpaka kuingia upande wa pili yaani Rwanda, unakutana na mazingira tulivu na safi, kadri tulivyokuwa tukienda mbele ndio mazingira yalizidi kuvutia, barabara nzuri zilizopambwa na bustani za maua pembeni na katikati kukiwa kumepandwa miti ya kupendeza, nchi ya Rwanda ni ya miinuko inayopendezeshwa na uoto wa kijani kibichi.

Baada ya kumaliza zoezi letu tulipelekwa kuona ng'ombe wenye pembe ndefu sana waliokuwa wamehifadhiwa kwenye eneo maalum lililokuwa na nyumba za kitamaduni za watu wa Rwanda. Tulipata pia fursa ya kutembelea kituo cha utamaduni (Rwanda Cultural Center ) nchini humo na kushuhudia wacheza ngoma wakicheza kwa ustadi mkubwa wakiwa wamevaa mavazi ya utamaduni wa Rwanda.

Siku iliyofuata tulisafiri kwa Mabasi maalum kwenda kwenye mji uitwao Murambi, ambapo ndipo yalipohifadhiwa mabaki ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbari (Murambi Memorial Genocide), safari ilikuwa ndefu tukipita kwenye milima na mabonde ya mito yaliyokuwa yakitiririsha maji safi pembeni kukiwa na mashamba ya migomba yaliyostawi vizuri. Tulifika eneo husika na kupokelewa vizuri na wahudumu wa eneo hilo, mwanzo nilidhani ni shule, au kambi ya Kijeshi kwani kulikuwa na mahanga kama nane hivi, wale wahudumu wakatupitisha kwenye jengo lililobandikwa picha za watu waliouawa na jinsi mauaji yalivyokuwa yakifanyika, baadhi yetu hasa kinadada walishindwa kuvumilia na kudondosha machozi.

Tulipotoka hapo tukaanza kuingia kwenye yale mahanga, sio siri mimi ni jasiri lakini pale machozi yalinilengalenga kwa nilichokiona, baada ya kuingia hanga la kwanza, ambalo lilikuwa na urefu wa mita sabini mpaka themanini, ndani tulikuta vichanja mwanzo hadi mwisho wa hanga, mabaki ya miili iliyouawa ikiwa imepangwa kwenye vile vichanja, miili hiyo ilikuwa imetiwa dawa ikiwa imekauka na ngozi yake, miili mingi ikionyesha alama za kuuawa kwa kukatwa mapanga yaani kulikuwa na watoto wadogo, vijana, mpaka watu wazima, mahanga yote nane yalikuwa yamehifadhi mabaki ya miili hiyo na mengine idadi matatu yalikuwa yamehifadhi nguo na viatu vya wahanga.

Kwa kweli nikikaa ile picha ya mabaki ya binadamu wenzangu walivyowekwa juu ya vichanja inanijia, ndipo hapo tunapoona madhara ya vita vya ndani, tumuombe Mungu atuepushe na majanga kama hayo na nchi yetu izidi kuwa na amani, tusiwe na ukabila bali wote tutambuane kama Watanzania.
 
Hizo ni zama zao na Muumba wao aliwaambia njia na aina ya vifo vyao!
Nakushangaa Kama ni mtanganyika mwenzangu badala ya kuhuzunika na kuumizwa na madhara ya vita vya majimaji na vile vya kunyongwa hadharani Kwa machifu wetu na wananchi wetu unawasikitikia majirani waliokuwa wanajisawazisha kiutawala!
Kama ndivyo usiwe biased uhuzunike ni vifo vyote vya kimbari vilivyowahi kutokea sehemu mbalimbali Duniani! Vinginevyo nitaamini Ile ujinga wenu ccm kutuchezea picha za vita za wenyewe Kwa wenyewe huko Rwanda na Burundi kututisha! Anyway, acha ikae hivyo!
 
Nilipata fursa ya kutembelea ndio nikaamua kuandika mambo niliyoyaona kwa wenzetu, lakini kimsingi mimi siko biase kama unavyosema.
 
Nilipata fursa ya kutembelea ndio nikaamua kuandika mambo niliyoyaona kwa wenzetu, lakini kimsingi mimi siko biase kama unavyosema.
Ulikwenda Kwa kiherehere chako! Be with it and live with it yourself! Usitie watu hofu na usiwatishe. Wenye wafu wao wametulia wewe unatuhangaisha na mizimu isiyotusaidia kunyesha mvua!
 
Nakubaliana na mleta mada, amani ni tunu kweli lakini tatizo watawala wanatutishia vita tusiweze kusimama dhidi yao wanapoenda ndivyo sivyo. Wanyarwanda walipigana baada ya upande mmoja kuchoka kuwa daraja la pili kwenye nchi yao, logic ya amani kusipokuwa na haki sana ni mmoja kukubali kuwa mnyonge.

Anyways bora ugali kwa chumvi kwenye amani kuliko pombe na nyama choma vitani.
 
Ulikwenda Kwa kiherehere chako! Be with it and live with it yourself! Usitie watu hofu na usiwatishe. Wenye wafu wao wametulia wewe unatuhangaisha na mizimu isiyotusaidia kunyesha mvua!
Hukuombwa kusoma wala kuweka comment yako, ni kiherehere chako, wee vipi kama umeshiba kande lala.
 
Hukuombwa kusoma wala kuweka comment yako, ni kiherehere chako, wee vipi kama umeshiba kande lala.
Kama hukutaka isomwe umeipandisha jf ili ifanywe Nini? Ungebaki nayo mwenyewe Kwa kuwa ulijipendekeza kwenda mwenyewe na hukutumwa na wasomaji! Nyakati nyingine mjifunze namna nzuri ya kutisha watu! Aliyekuambia kutakuwa na vita nani? Punguza kuhemkwa na kujua kwingi na kujipa kazi ya kumshauri ujinga! Kimbelembele wahed!
 
Wewe unaye comment pumba hukutakiwa kusoma
 
Cccm wanajua kabisa kuwa wanaongoza nchi vibaya lakini wakiona maji ya shingo wanaleta movie za genocide kutisha watu mimi nawaambia kuwa wajitahid kuwa na hekima vita si ujinga bali ni njia murua ya wanyonge kujitetea
 
Back
Top Bottom