Muono wa muungano kutoka Zanzibar: Je, muda wa marekebisho umefika?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000
[h=1][/h]
December 22, 2013 by zanzibariyetu
Na Salma Said,
Mwezi wa April mwaka huu (2014) itatimia miaka 50 tokea kuibuka muungano kati ya Tanganyika and Zanzibar, lakini mijadala kuhusu hatima ya muungano imekuwa mikubwa.
Mwaka 1971, rais wa zamani wa Zanzibar, Abeid Karume, alisema: “muungano ni kama koti, likikubana, utalivua”. Leo nukuu hii imekuwa ikieleweka kama (the pan-africanist) Karume alishaanza kutilia mashaka umuhimu wa muungano kwa faida ya Zanzibar.
Mwezi wa January 2013, ‘koti’ limerudishwa tena na Seif Sharif Hamad, kiongozi wa upinzani wa muda mrefu ambaye sasa ni makamu wa kwanza wa rais Zanzibar, alisema: “hatutulivua, lakini tutalirekebisha na kulishona upia kutokana na hali ya leo”. Wazanzibari wengi, kutoka pande tofauti za siasa, wanakubaliana na msimamo huu.
Katika maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya muungano, Tanzania itamaliza kutunga katiba mpya. Hii ni kama vile mjadala kuhusu muungano umepata upepo mpya katika tanga, hasa upande wa Zanzibar, ambapo mjadala kuhusu muungano umechukua sehemu kubwa katika kutunga katiba mpya.
Mfumo uliopo
Leo hii Tanzania ina maraisi wawili,serekali mbili na mabunge mawili: moja ni kwa upande wa muungano na mwingine kwa Zanzibar. Isipokuwa kwa badhi ya vitengo (kama vile fedha, ulinzi na usalama na mambo ya nje), kuna vitengo pacha kwa upande wa sera nyingi. Tokea mwaka 1977, serekali zote mbili simetoka kutoka chama kimoja – Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mfumo wa vyama vingi ambao umeanzishwa tena mwaka 1992, haukubadilisha tabia hii. CCM ilishinda chaguzi miaka1995, 2000 na 2005, lakini CUF imekuwa ikipinga matokeo ya kila uchanguzi. Kwa hivyo uchaguzi na mizozo imekuwa kama pete na kidole kwa Zanzibar kwa miongo ya hivi karibuni iliyopita. Kwa miaka mingi CCM imekuwa inastumiwa kwa vitendo vya kutumia nguvu, kusweka watu ndani na kuwabaguwa kisiasa – hasa wapinzani.
Uchaguzi wa rais mwezi wa October 2010 ulihitimishwa tena kwa ushindi wa CCM, kwa vile kabla ya hapo idadi kubwa ya wazanzibari walishatangiliza kupiga kura ya kutaka mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kuhakikisha kwamba vyama vyote vya CCM na CUF vinashirikiana katika kuunda serekali mpya, hii ikiwa ni serekali ya kwanza ya pamoja tokea baada ya mapinduzi.
‘Hakuna ajenda ya siri’
Mwanzoni kuukosoa muungano ikichukuliwa kama ni kosa la jinai. Lakini baada ya kuletwa tena mfumo wa vyama vingi, ukosoaji umekuwa wa kiwango cha juu. Hata hivyo, mara nyingi wazanzibaris ambao wanahoji muungano hutuhumiwa kuwa na ajenda ya siri; kuazimia kuurejesha utawala wa kisultan au kuunda serekali ya kidini. Wazanzibari wengi wanachukulia shutuma hizi kua zinaonyesha upeo mdogo kuitambua historia ya Zanzibar na pia ni shutuma za kipuuzi. Badala yake wanatia maanani zaidi suali la demokrasi na uchumi kuwa ni kitu muhumu zaidi kwao kinachoweza kurekebisha uhusiano wao na upande wa Tanzania bara.
“Kero za Muungano”
Neno kero ni Kiwahili kwa “kitu ambacho kinakera sana” na linatumika Zanzibar kuashiria matatizo ndani ya muungano. Kwa ujumla, waanzibari wanakubali kwamba kuna kero kadha lazima zirekebishwe. Uanzishili wa muungano mwaka 1964 ulihusisha idadi ndogo tu ya viongozi. Inasemekana kwamba lau kama wazo lingelipitishwa katika baraza la kutunga sheria zanzibar wakati huo – baraza la mapinduzi – ingelitupiliwa mbali.
CCM pia imekuwa ikishutumiwa, chini ya utawala wake, kua makubaliano ya muungano yameongezeka kutoka 11 hadi 22 katika mwaka 1977 – yamekuwa yakiamuliwa na bunge lisilotayarishwa kwa mijadala hii. Profesa maarufu wa sheria Issa Shivji kutoka chuo kikuu Dar es Salaam amedai kuwa nyongeza hii (hadi mambo 22) ilikuwa kinyume cha katiba. Mifano kama hiyo – kama CCM-bara imekuwa ikidhibiti – imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika mijadala ya hivi leo Zanzibar.
Mfano mmoja ni kuhusu mgawano wa mapato: Kutokana na makubaliano, Zanzibar inastahiki kupata asilimia 4.5 ya bajeti ya muunganor, lakini Tanzania ikipata misaada kutoka nje, Zanzibar mara nyingi ‘husahauliwa’. Hapo badaye Zanzibar inataka kufunga mikataba moja kwa moja na wafadhili wa nje na kuvutia wawekezaji kwa kutoza kodi ndogo. Lakini katika mfumo uliopo sasa Zanzibar haiwezi kuamua yenyewe. Wazanzibari wengi wanakerwa na kulazimishwa kulipa kodi mara mbili kwa kuingizi na kutoa bidhaa – ndani ya muungano na kwa Zanzibar.
Muundo ujao
Je, kuna fikra gani za ufumbuzi? Msimamo rasmi wa CCM ni kubaki na mfumo uliopo – serekali moja ya muungano na moja ya Zanzibar. Kwa muda mrefu CUF kilitaka muundo wa serekali tatu – moja ya Zanzibar, moja ya bara na moja ya muungano. Uamsho, jumuhia ya kiislamu yenye makaazi yake Zanzibar, imekuwa ikikusanya sahihi na pia kufanya maandamano kuhamasisha mamlaka kamili ya Zanzibar.
Njia ya nne, inayoshadiwa na CUF, na makubaliano ya mkataba ambapo yanafanana na yale ya EU, mataifa mawili huru yenye makubaliano maluum katika nyanja maluum. Mawazo haya yalipokewa wa wanachama wengi kutoka vyama vyote viwili vya CCM na CUF kupitia tume ya kusanya maoni ilipokuwa Zanzibar.
Rasimu ya katiba mwezi June 2013 ilipendekeza mfumo wa serekali tatu. Pamoja na hayo tume ilipendekeza kwamba mafuta na gesi asilia yasiwe tena katika mambo ya muungano – mada ambayo hapo kabla ilikuwa ni kama moto ilipojadiliwa katika mijadala ya muungano, na iliwaweka pamoja wanasiasa kwa misingi ya itikadi za kivyama Zanzibar. Rasimu ya katiba inapendekeza zaidi kwamba muungano utajumuisha mambo saba tu – tofauti na sasa mambo 22.
Mustakbal
Hatuwezi kutambua sasa jinsi gani serekali ya muungano itachukulia rasimu ya katibal. CCM bara na pia baadhi ya wawakilishi wa serekali ya Zanzibar wameonyesha nia ya kutokubaliana na rasimu hii. Ndani ya Zanzibar, watu wengi wanaamini kua zoezi limeshafikia mbali kiasi kwamba maamuzi yatakayokubalika ni uhuru kamili kwa Zanzibar au makubaliano ya kimkataba.
Zanzibar ilianzisha sheria mpya ya kura ya maoni mwaka 2010 na inategemewa kwamba sauti za watu zitasikika kabla katiba mpya kuanza kufanya kazi. Hata hivyo, kitu kimoja kiko wazi: Wazanzibari walio wengi wanataka muundo mpya wa muungano na mamlaka zaidi. Kutumia msemo wa rais Karume kuhusu ‘koti’ – kuna haja ya kulipitisha kwa fundi charahani kabla koti kuchanika.

Chanzo www.mzalendo.net
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom