MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako!

JamiiForums

Naomba kufahamu kwanini tangazo langu la "TAIRI MPYA ADIMU ZINAUZWA" limefutwa bila sababu ya msingi zaidi ya kusahau kuandika mahali bidhaa inapatikana? Jee, mnatumia mabavu zaidi ya fairness? Kweli kulikuwa na sababu ya kufuta tangazo zima badala ya Kuniikumbusha kurekebisha tangazo kwa kuweka wazi mahali bidhaa inapatikana? Hata wasomaji wangeweza kunikumbusha niseme wapi bidhaa ilipo. Hatua ya kufuta tangazo zima kwa jambo dogo kama hilo inaonyesha muhusika ana lake jambo. Ujinga mtupu!!
 
Mnaolalamika matangazo yenu kufutwa pelekeni kwenye magazeti au runinga pamoja na television matangazo yenu yatapata airtime.

Muache kusumbua mods humu, wanayo mengi ya kufanya
 
Mnaolalamika matangazo yenu kufutwa pelekeni kwenye magazeti au runinga pamoja na television matangazo yenu yatapata airtime.

Muache kusumbua mods humu, wanayo mengi ya kufanya
Acha ukuda wewe! Kwanini tangazo la kuuza Tairi za Gari lifutwe kwa sababu za kipumbavu?

Kuna tatizo mahali, na linaanzia na Moderator wa hili jukwaa. Hafai!

JF muwe mnaaajiri watu ambao ni rational, reasonable and fair in their day-to-day, on the job decision making kwa nafasi za Moderators.

Moderator anajiona Mbabe na Mungu Mtu sababu tu ana uwezo wa kufuta bandiko lolote akiamua bila ya sababu za msingi?

Hapa chini ni matangazo machache ambayo wauzaji hawakuweka wazi mahali huduma/bidhaa zinapatikana, lakini matangazo hayakufutwa.






Kama ni Vigezo na Masharti kuzingatiwa, basi vi-apply kwa wote across the board. Vinginevyo Moderator atakuwa hatimizi wajibu wake ipasavyo, na baadhi tutachukulia kufutwa holela kwa matangazo kama ni uonevu na ubabe tu.
 

Attachments

  • Untitled.jpg
    Untitled.jpg
    19.4 KB · Views: 78
Ndugu wadau wa Jukwaa la Matangazo Madogo,

Tunafarijika kuona mnaendelea kutumia vizuri jukwaa hili katika kufanya biashara.

Hata hivyo, kuna changamoto kwa baadhi ya wenzetu kushindwa kuzingatia vigezo vya kuweka matangazo yao hivyo kupelekea matangazo yao kuondolewa hewani.

Vigezo vya msingi unavyopaswa kuzingatia kabla hujaweka tangazo;
  1. Elezea huduma/bidhaa unayouza kwa maelezo machache yanayojitosheleza
  2. Kama ni bidhaa, elezea hali yake (mpya au imetumika muda gani) huku ukiambatanisha na picha yake halisi.
  3. Taja bei
  4. Taja mahali huduma/bidhaa hiyo inapopatikana pamoja na mawasiliano yako.(Usiwaambie watu wakufuate PM kwa Mawasiliano. Weka namba ya simu)
  5. Weka taarifa mpya kuhusu bidhaa hiyo kwenye uzi husika, usianzishe uzi mpya.
  6. Usiweke tangazo moja mara nyingi.
Ni vyema kuzingatia hatua hizo chache. Kinyume na hapo, tangazo lako litaondolewa hewani.

Kuna baadhi ya matangazo hayaruhusiwi kabisa JamiiForums. Mfano matangazo ya kurasa za Blogs, Facebook, Instagram, Twitter, au mtandao wowote yataondolewa mara moja. Pia haturuhusu matangazo ya madawa ya asili, vipodozi, Tiba ya asili nk.

Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili

NB: Matangazo yote yakae Jukwaa la Matangazo.

Karibuni kwa maswali na ufafanuzi zaidi..
Mbna tangazo langu limezuiliwa
Kama nimekosea mnisamehe
Jaman ndio mda WA biashara huu
 
Back
Top Bottom