Muongozo wa Wizara ya Elimu kuhusu suala la upigaji viboko mashuleni unasemaje? Je, walimu wanaokiuka muongozo huo ni hatua gani wanaweza kuchukuliwa?

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,197
2,000
Naomba ushauri juu hili la viboko mashuleni. Kumekuwepo na kasumba imejitokeza katika shule za sekondari wilaya ya kyela. Walimu wanapiga wanafunzi kama vile sio binadamu.

Mwanafunzi kupigwa fimbo hadi hamsini kwa wakati mmoja, tena maeneo tofauti tofauti. Kama mikononi, mgogoni, miguuni, matakoni ndio usiseme.

Kuna shule kama za sekondari Bojonde, Ngonga Masukila, hizo ni mifano tu ya shule nilizo na uthibitisho Nazo. Ila kwa taarifa zilizopo ni kwamba hii kasumba imeambukiza shule nyingi za wilaya ya kyela.

Athari zilizoanza kujitokeza ni kwamba wanafunzi wanaacha shule kisa kuogopa mijeledi ambayo haina kiasi. Ni mifano ya wanafunzi watatu katika shule ya sekondari Bujonde walioacha shule, (majina nitayahifadhi).

Athari nyingine ni kwamba sio kuwa nidhamu inatengezwa ila woga ndio uliotengezwa kwa wanafunzi. Hakuna mwanafunzi anayesema "mwalimu flani anafundisha vizuri" zaidi ya walimu kushindana idadi ya viboko anavyopiga wanafunzi.

Waziri wa elimu na wadau wa elimu liangalieni hili suala katika wiliya ya kyela. Kwa sababu moja, halijengi nidhamu kwa wanafunzi ila woga, Pili, haliongezi ufaulu kwa wanafunzi kwa sababu walimu hawafundishi afu wanapiga sana viboko.

Mfano wiki iliyopita shule ya Bujonde wa form one wamefanya test ya civics lakini hawajawahi fundishwa, wanafunzi wakapata zero wameambulia viboko zaidi ya ishirini kwa kila mmoja.

Ninaomba sana maana wanafunzi wameanza kutokupenda shule na kufikia kuacha shule. Maana wanaona shule sio sehemu ya kujifunza ila ni sehemu ya mateso.
 

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
5,265
2,000
Viboko mwisho vinne. Kibali Cha viboko hivyo hutolewa na mkuu wa shule na kumbukumbu ya kuchapwa huko huhifadhiwa ktk daftari la nidhamu maarufu black book. Mwanafunzi wa kiume ataadhibiwa na mwl wa kiume na wa kike mwl wa kike. Adhabu mbadala inasisitizwa Kama usafi, kulima shamba la shule nk. Nadhani umenipata kiasi.
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,788
2,000
"Hadhifu" ni nini? Ndo maana watoto wa siku hizi ni zero brain. Bila viboko wengi wetu tusingekuwa hapa kielimu. Siku hizi watoto wanabembelezwa kusoma, Watoto wenyewe manunda.
 

Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
2,421
2,000
Je, kuna muongpzo wa wakuu wa wilaya kucharaza watu hadharani na mbele ya camera?
 

ngwanduu

JF-Expert Member
Sep 20, 2018
485
500
Yani mwanafunzi apewe test ya civics alafu hajawahi kufundishwa sio kweli acha kusikiliza mameno fika shuleni utajua ukweli, Watoto nizamu imekua ndogo sana hujaona wale waliochapw na mkuu wa mkoa wa mbeya kisa nizamu mbovu, tumeona mwalimu aliekata mapanga na mwanafuzi acha kutetea hawa watoto ndugu yangu.
 

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,197
2,000
Mkuu nilichokiandika kina ukweli wa 100% . afu suala sio wanafunzi wasipigwe wakikosea, sasa ndio umpige mwanafunzi fimbo hadi hamsini? Kama kosa ni kubwa kwa nini usimfukuze?
 

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
813
1,000
Siku moja tutaangalia nyuma na kushangaa tulivyokuwa tunatandika wanafunzi shuleni. Tutajiona mafala sana.
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,785
2,000
Naomba ushauri juu hili la viboko mashuleni. Kumekuwepo na kasumba imejitokeza katika shule za sekondari wilaya ya kyela. Walimu wanapiga wanafunzi kama vile sio binadamu.
Inaonyesha kama baadhi ya watu hawa wanayo tabia hii ya ukatili kwa watoto wa shule. Kuna mwalimu aliwahi kunifanya mimi nimchukie milele sababu ya tabia hii ya ukatili huu wa kipumbavu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom