Muongozo wa software developer anaeanza part-3 (WEB BASED APPLICATION)

Dr Orb

Member
Aug 4, 2019
10
40
Uzi huu unaletwa kwenu na

Orb Tech LLC.

Ni muendelezo wa uzi huu Muongozo wa software developer anaeanza part-2

Sehemu hii tutazumgumzia Web based applications.

Kama tulivyoainisha hapo awali hizi ni program zinazotumia internet katika kufanikisha jambo lililokusudiwa mfano Kupatana, amazon, eBay, facebook, simbanking CRDB na nyingine nyingi. programu hizi zinaweza kuwa ni kwa matumizi binafsi ya mtu au kikundi cha watu au ikawa ni kwa matumizi ya watu wengi na tofauti, inaweza ikawa ni maalumu kwa kifaa fulani (simu, kompyuta n.k) au system programu fulani (Windows, mac OS au Linux). kwa namna yeyote unayotaka application yako iwe itategemea zaidi ujuzi.

Kwa vile lengo la uzi huu ni kujifunza tuangalie kipi ni rahisi na unachopaswa kujifunza. katika sehemu hii ya kwanza ya web based app tutaangazia applications ambazo hufanya kazi katika vifaa vyote bila kujali system programu inayotumia kwa kuwa hii haihitaji ujuzi wa hali ya juu lakin pia itatoa ujuzi wa jumla kwako kwa kuwa inahusisha teknolojia ya aina moja.

Tekinolojia hii inajulikana kama web technology, ni tekinolojia ya kipekee ambayo inakubalika na na imewezeshwa na vifaa na system programu nyingi mno na ni uti wa mgongo kwa kila ujuzi wa kutengeneza programu. Tuangazie ni kwa namna gani unaweza kuingia hapa.

kuna namna mbili unaweza kumiliki application yako.
  • Kutumia wataalamu wafanikishe hilo, au
  • Unaweza tengeneza mwenyewe.

Tuchukue option ya pili ya kutengeneza mwenyewe kwa kuwa ndio dhima ya uzi huu.

katika ulimwengu huu wa web based applications development kuna vipengele zifuatazo;
  1. Kubuni muonekano na namna application yako inapaswa kufanya kazi (web apps design)
  2. Kuuwezesha ubunifu wa kimuonekano na utendaji kazi wa application yako kutengeneza ili ufanye kazi kama ilivyokusudiwa (web app Development)
Web design - ubunifu huu unafanywa na mtu yeyote ambaye anapenda kazi za ubunifu. inahusisha ubunifu wa muonekano, utendaji kazi na utumiaji wa application (UI/UX design). hapa unaweza kuchukua fursa hii pekee na ikakulipa ingawa ni vyema kuhusika na vipengele vyote kwa kuwa mbunifu anaweza buni kitu ambacho huwezi kukifanya au hakiwezi kufanikishwa na tekinolojia iliyopo.

Mbunifu wa application anapaswa kuwa na uwelewa wa ujuzi mbalimbali kama ifuatavyo.
  • Lugha mbalimbali zinazotumiwa katika web technology, ikiwamo lugha kwa ajili ya muundo (HTML/XHTML), lugha kwa ajili ya kunogesha muonekano na kutia nakshi application yako (CSS, BOOTSTRAP, W3CSS, Javascripts (JQUERY NA REACT.JS). (SIO LAZIMA LAKINI ILI KUWA IMARA ZAIDI NI LAZIMA)
  • Uwe na ufahamu kuhusu application mbalimbali za ubunifu kama vile zile za ubunifu wa picha na muonekano (Adobe photoshop, Sketch, inkscape, Gimp, n.k) huu ni ujuzi wa lazima kwa hivyo anza kujifunza kama uko interested na web design hizi zitakusaidia kuutoa ubunifu wako kutoka kichwani kuja kwenye muonekano halisi.
  • Ufahamu mbalimbali unaohusu ubunifu hapa kuna mengi ya kujifunza mfano jifunze kuhusu tabia za watu, tamaduni za watu, mapenzi ya watu mbalimbali, namna ya kuwasiliana, Saikolojia hasa zinazohusu mionekano ya vitu kwa watu, maujanja ya uandishi na uwasilishaji na mengine mengi.
Vyote hivi viapatikana buree mtandaoni (youtube au torrents sites) kwa msaada wasiliana nami kupitia whatsapp 0787 389 803.

Development part.
Hapa ndio utamu na umelala, hapa ndio unaweza kubadilisha ubunifu wako wa kimuonekano kuwa wa kiutendaji na kufanikisha adhma yako. sehemu hii uhusisha ubunifu wa kifikra, utumiaji wa lugha za kitaalamu katika mpangilio wa kitalaamu na weledi wa hali ya juu ili kufanikisha jambo. katika kipengele hichi unaweza kuchagua pia ujikite wapi.
Unaweza kuhusika na kutengeneza apps kwa kuhusika na utendaji kazi wa app kwa ngazi ya mtumiaji tu. (front end) hii inahusisha muonekano na namna gani mtumiaji anaingiliana na app yako, jinsi gani anaweza tazama, download au edit rasilimali za app yako.
Au unaweza kuhusika na kutengeneza miundombinu ambayo haionekani na mtu mtumiaji wa app yako. (back end). hapa utahusika na mambo yote ambayo mtumiaji hayajui kuhusu app mfano taratibu zinazopelekea mteja kuona rasilimali za app, wapi rasilimali zinatoka na zinapohifadhiwa na protocol kibao zinazohusu hifadhi ya rasilimali na muingiliano wake na app yako. (database programing).

kwa hivyo katika part hii unaweza chagua kipengele chako front end au back end au vyote na bado ukafanikiwa. ujuzi natofautiana kulingana na kipengele.

kwa front end - Uwe imara kwenye lugha za muundo na uwakilishaji wa app katika mtandao (HTML/XHTML, XML, CSS, BOOTSTRAP, JAVASCRIPT), uwe sawa katika lugha za kimantiki (programming languages). lugha zinakuwezesha kufanikisha namna gani app yako itafanya kazi kama vile kuingiliana na mtumiaji na kanzidata(databases). zipo nyingi lakini maarufu ni kama Javascripts, Typescripts, PHP, na java.

Kwa back end - uwe imara katika lugha za kimuundo hususa ni XML. Uwe imara kuhusu kanzidata(databases mfano MySQL, Oracle na Firebase), uwe imara kuhusu lugha maalumu kuhusu databases kama PL au SQL( SQL ni ya lazima). uwe sawa kwenye lugha za kimantiki (programming languages), zinazotumika zaidi ni Java, PHP,T, Javascript (Nodes.js) na Python.

Sio lazima ujue zote hizi, unaweza kuchagua mli au tatu na ukawa developer mtata na kufanya miradi mikubwa. Leo tuishie hapa, sehemu ijayo tutaangalia kwa ufupi na undani kidogo wa ujuzi mbalimbali tajwa hapo juu kubwa ikiwa ni (lugha za kimuundo na muonekano yaani zinazomuhusu zaidi front end developer)

Kama kuna shida yeyote, swali au jambo lolote kuhusu hapa tulipofika au zaidi unaweza kuwasiliana nami kupitia whatsapp 0787 389 803.
 
Mkuu nikukosowe Asp.net sio programing language bali ni Framework
Uzi huu unaletwa kwenu na

Orb Tech LLC.

Ni muendelezo wa uzi huu Muongozo wa software developer anaeanza part-2

Sehemu hii tutazumgumzia Web based applications.

Kama tulivyoainisha hapo awali hizi ni program zinazotumia internet katika kufanikisha jambo lililokusudiwa mfano Kupatana, amazon, eBay, facebook, simbanking CRDB na nyingine nyingi. programu hizi zinaweza kuwa ni kwa matumizi binafsi ya mtu au kikundi cha watu au ikawa ni kwa matumizi ya watu wengi na tofauti, inaweza ikawa ni maalumu kwa kifaa fulani (simu, kompyuta n.k) au system programu fulani (Windows, mac OS au Linux). kwa namna yeyote unayotaka application yako iwe itategemea zaidi ujuzi.

Kwa vile lengo la uzi huu ni kujifunza tuangalie kipi ni rahisi na unachopaswa kujifunza. katika sehemu hii ya kwanza ya web based app tutaangazia applications ambazo hufanya kazi katika vifaa vyote bila kujali system programu inayotumia kwa kuwa hii haihitaji ujuzi wa hali ya juu lakin pia itatoa ujuzi wa jumla kwako kwa kuwa inahusisha teknolojia ya aina moja.

Tekinolojia hii inajulikana kama web technology, ni tekinolojia ya kipekee ambayo inakubalika na na imewezeshwa na vifaa na system programu nyingi mno na ni uti wa mgongo kwa kila ujuzi wa kutengeneza programu. Tuangazie ni kwa namna gani unaweza kuingia hapa.

kuna namna mbili unaweza kumiliki application yako.
  • Kutumia wataalamu wafanikishe hilo, au
  • Unaweza tengeneza mwenyewe.

Tuchukue option ya pili ya kutengeneza mwenyewe kwa kuwa ndio dhima ya uzi huu.

katika ulimwengu huu wa web based applications development kuna vipengele zifuatazo;
  1. Kubuni muonekano na namna application yako inapaswa kufanya kazi (web apps design)
  2. Kuuwezesha ubunifu wa kimuonekano na utendaji kazi wa application yako kutengeneza ili ufanye kazi kama ilivyokusudiwa (web app Development)
Web design - ubunifu huu unafanywa na mtu yeyote ambaye anapenda kazi za ubunifu. inahusisha ubunifu wa muonekano, utendaji kazi na utumiaji wa application (UI/UX design). hapa unaweza kuchukua fursa hii pekee na ikakulipa ingawa ni vyema kuhusika na vipengele vyote kwa kuwa mbunifu anaweza buni kitu ambacho huwezi kukifanya au hakiwezi kufanikishwa na tekinolojia iliyopo.

Mbunifu wa application anapaswa kuwa na uwelewa wa ujuzi mbalimbali kama ifuatavyo.
  • Lugha mbalimbali zinazotumiwa katika web technology, ikiwamo lugha kwa ajili ya muundo (HTML/XHTML), lugha kwa ajili ya kunogesha muonekano na kutia nakshi application yako (CSS, BOOTSTRAP, W3CSS, Javascripts (JQUERY NA REACT.JS). (SIO LAZIMA LAKINI ILI KUWA IMARA ZAIDI NI LAZIMA)
  • Uwe na ufahamu kuhusu application mbalimbali za ubunifu kama vile zile za ubunifu wa picha na muonekano (Adobe photoshop, Sketch, inkscape, Gimp, n.k) huu ni ujuzi wa lazima kwa hivyo anza kujifunza kama uko interested na web design hizi zitakusaidia kuutoa ubunifu wako kutoka kichwani kuja kwenye muonekano halisi.
  • Ufahamu mbalimbali unaohusu ubunifu hapa kuna mengi ya kujifunza mfano jifunze kuhusu tabia za watu, tamaduni za watu, mapenzi ya watu mbalimbali, namna ya kuwasiliana, Saikolojia hasa zinazohusu mionekano ya vitu kwa watu, maujanja ya uandishi na uwasilishaji na mengine mengi.
Vyote hivi viapatikana buree mtandaoni (youtube au torrents sites) kwa msaada wasiliana nami kupitia whatsapp 0787 389 803.

Development part.
Hapa ndio utamu na umelala, hapa ndio unaweza kubadilisha ubunifu wako wa kimuonekano kuwa wa kiutendaji na kufanikisha adhma yako. sehemu hii uhusisha ubunifu wa kifikra, utumiaji wa lugha za kitaalamu katika mpangilio wa kitalaamu na weledi wa hali ya juu ili kufanikisha jambo. katika kipengele hichi unaweza kuchagua pia ujikite wapi.
Unaweza kuhusika na kutengeneza apps kwa kuhusika na utendaji kazi wa app kwa ngazi ya mtumiaji tu. (front end) hii inahusisha muonekano na namna gani mtumiaji anaingiliana na app yako, jinsi gani anaweza tazama, download au edit rasilimali za app yako.
Au unaweza kuhusika na kutengeneza miundombinu ambayo haionekani na mtu mtumiaji wa app yako. (back end). hapa utahusika na mambo yote ambayo mtumiaji hayajui kuhusu app mfano taratibu zinazopelekea mteja kuona rasilimali za app, wapi rasilimali zinatoka na zinapohifadhiwa na protocol kibao zinazohusu hifadhi ya rasilimali na muingiliano wake na app yako. (database programing).

kwa hivyo katika part hii unaweza chagua kipengele chako front end au back end au vyote na bado ukafanikiwa. ujuzi natofautiana kulingana na kipengele.

kwa front end - Uwe imara kwenye lugha za muundo na uwakilishaji wa app katika mtandao (HTML/XHTML, XML, CSS, BOOTSTRAP, JAVASCRIPT), uwe sawa katika lugha za kimantiki (programming languages). lugha zinakuwezesha kufanikisha namna gani app yako itafanya kazi kama vile kuingiliana na mtumiaji na kanzidata(databases). zipo nyingi lakini maarufu ni kama ASP.NET, Javascripts, Typescripts, PHP, na java.

Kwa back end - uwe imara katika lugha za kimuundo hususa ni XML. Uwe imara kuhusu kanzidata(databases mfano MySQL, Oracle na Firebase), uwe imara kuhusu lugha maalumu kuhusu databases kama PL au SQL( SQL ni ya lazima). uwe sawa kwenye lugha za kimantiki (programming languages), zinazotumika zaidi ni Java, PHP, ASP.NET, Javascript (Nodes.js) na Python.

Sio lazima ujue zote hizi, unaweza kuchagua mli au tatu na ukawa developer mtata na kufanya miradi mikubwa. Leo tuishie hapa, sehemu ijayo tutaangalia kwa ufupi na undani kidogo wa ujuzi mbalimbali tajwa hapo juu kubwa ikiwa ni (lugha za kimuundo na muonekano yaani zinazomuhusu zaidi front end developer)

Kama kuna shida yeyote, swali au jambo lolote kuhusu hapa tulipofika au zaidi unaweza kuwasiliana nami kupitia whatsapp 0787 389 803.
 
Hizi mada zinanipa hamasa sana japo programming imenipita kushoto kabisa. Itabidi nifanye jambo hasa kwa dunia ya sasa
 
Mkuu,usikate tamaa,ukiamua unaweza.Computer programming ni ustadi ambao unaweza kujifunza ukiwa na rasilimali sahihi na mtu wa kukupa muongozo. Fulgent careers ndio kazi yetu hii, wasiliana nasi kwa namba 0769 524 022. Utapewa muongozo wote wa namna ya kuanza mpaka kuwa mtaalam kwa kutumia rasilimali zilizopo mtandaoni na kwa mpangilio sahihi.
 
Back
Top Bottom