Muongozo wa Serikali: Kuhusu Muhula wa I na II 2020 Baada ya Ugonjwa wa Corona

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
1. Muhula wa kwanza utaanza tarehe 29.06.2020 mpaka tarehe 28.08.2020

2. Likizo fupi itakuwa kuanzia tarehe 29.08.2020 mpaka 06.09.2020

3. Muhula wa pili utaanza tarehe 07.09.2020 mpaka tarehe 18.12.2020

4. Siku tulizosoma kabla ya kufunga shule kwaajili ya corona ni 52,siku zilizobaki kukamilisha siku za masomo kwa mwaka mzima ni 142,siku zilizotolewa na wizara kufundisha baada ya corona ni 125, hivyo basi zitabaki siku 17 kukamilisha siku 194 za masomo kwa mwaka mzima .

Siku hizo 17 zitafidiwa kwa masaa mawili yaliyoongezwa,ambapo jumla ya masaa ya nyongeza ni 250 ambayo ni sawa na siku 30 za kazi.(hivyo basi wanafunzi watatoka saa 11 jioni).

Zingatio.

Hakuna siku zilizopotea, siku zote zimefidiwa.

5.Ili kukabiliana na ugonjwa wa corona kila mwanafunzi mwenye umri wa miaka mitano na kuendelea anatakiwa kuvaa barakoa.

6. Mwanafunzi ashonewe barakoa ya kitambaa cha pamba* *rangi ya bluu(blue), angalau awenazo mbili kila siku kwaajili ya dharura.

7. Maji na sabuni kwaajili ya kunawa mikono atapata shuleni.(mtoto haruhusiwi kupaka au kuja na vitakasa mikono(sanitizers) kwasababu zina hatari ya kulipuka).
 
Back
Top Bottom