Muongozo na ushauri kwa wanafunzi waliopokea matokeo ya kidato cha nne 2018

Habari wakuu,

Kuna wadogo zetu wamepata matokeo yao ya kidato cha nne leo. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio inayotoa upepo awe nani baadae kitaaluma kwa uchaguzi anaofanya sasa japo kwa baadhi wanaweza kuwa na wigo mpana wa kuchagua tena baadae.

Hapa jukwaani kuna wengi ambao walipita huko na wana uzoefu wa matokeo tofauti, iwe ya kufaulu, wastani au kufeli na jinsi gani walijikwamua kutoka kwenye hali yaliyokuwa nao wakati husika.

Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu ama kukata tamaa kwa kupata matokeo hafifu. Kwa heshima ningependa kuwaita wanajamvi wote katika kufikisha lengo la mada hii.

Karibuni!

Habar wanaJF mi nmemaliza kidato cha nne 2017 kutoka katika Technical School na nmepata :
English B
Engeneering Science C
Geography C
Electrical Draughting C
Electrical engeneering science D
Kiswahili D
Chemistry D
Civics D
Basic Mathematics D
Radio &TV servicing FF

Je kutokana na matokeo hayo nnawezakuchaguliwa chuoni moja kwa moja na serikal ??
Natanguliza shukran zangu.
 
Hey naitwa Hellen nina miaka 19 nimemaliza form 4 mwaka juz 2016 nilipata division 2.21 na masomo yalikua hivi.
Chemistry D
Biology B
Geography D
Physics D
Mathematics D
English C
Kiswahili C
Naombeni ushauri jinsi gani naweza kupata chuo na nikasomee course gan???
 
kweli?? hiyo mbona kama ni 24, au ndalichako siku hizi two ameifikisha huko. siku hizi raha sana hata civics hamsomi??
 
Back
Top Bottom