Habari wakuu,
Kuna wadogo zetu wamepata matokeo yao ya kidato cha nne leo. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio inayotoa upepo awe nani baadae kitaaluma kwa uchaguzi anaofanya sasa japo kwa baadhi wanaweza kuwa na wigo mpana wa kuchagua tena baadae.
Hapa jukwaani kuna wengi ambao walipita huko na wana uzoefu wa matokeo tofauti, iwe ya kufaulu, wastani au kufeli na jinsi gani walijikwamua kutoka kwenye hali yaliyokuwa nao wakati husika.
Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu ama kukata tamaa kwa kupata matokeo hafifu. Kwa heshima ningependa kuwaita wanajamvi wote katika kufikisha lengo la mada hii.
Karibuni!

Swala la kwanza kama mzazi/mlezi muulize mwanao anapenda kwenda A level au anapenda kwenda chuo?maana kuna wazazi wengine wanalazimisha watoto wao kwenda A level ilihali mtoto hataki kwenda huko ,anataka kwenda chuo!
Akikujibu chuo, muulize anapenda kusomea mambo gani,kutoka moyoni akujibu anavyofeel!
Then,mpeleke akasomee anachotaka!
Faida yake
Kutokana na kuwepo kwa wimbi la ukosefu wa ajira ,itamsaidia kufanya kitu akipendacho,hali itakayompelekea aweze kujiajiri!
Mfano,akisema anataka kuwa mwalimu mpeleke,kwani huko atasoma kwa bidii na kuelewa mambo hivyo itamsaidia kufanya chochote juu ya field yake kwa sababu utakuwa na uelewa wa kutosha! Kuliko kumpeleka kusoma kwa kuangalia kuajiriwa hali itakayomfanya asome akifikiria kuajiriwa hivyo atakariri kuliko kuelewa (hii itamcost sana)
Akisema A level
Kuna baadhi ya wazazi hawapendi wanao waende A level,wanataka waende diploma baada ya form iv,tafadhali kama mwanao anapenda A level,mpeleke A level...,hii itamsaidia kusoma kwa bidii kwa sababu hili ndilo limekua chaguo lake!
Mwisho napenda kuwakumbusha wale wazazi ambao watoto wao wanataka kwenda chuo ,waombe kwani dirisha la maombi litafunguliwa Siku si nyingi kwa ajili ya march intake 2019
Nitaendelea kuelezea wanafunzi ambao wamepata matokeo ambayo hawakuyatarajia wafanye Nini ili kuwepo kwenye njia sahihi!
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
Blogger boy