MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

Uzi mzuri sana huu ila tunaomba utuwekee na upande wa pili... Mambo ya kuzingatia unapouza gari! . Mimi nauza Spacio new model, sasa nimekutana na mambo kadhaa. Hapo kwenye namba 3. wameshakuja madalali kama watatu, wote wanakwamia bei ya 6.5m, mwingine 7m, mwingine 7.5m. Mimi nimetangaza 8m siyumbi. Maana yake ni kwamba dalali ataenda kutangaza 8m au zaidi huku mimi naambulia 7, ujinga kabisa. nimewatimua.

Namba 5. Kuna watu wananishauri nipige rangi gari wakati halijagongwa wala halina mbamizo wowote, sana sana kuna vimistari vidogo sana ambayo labda ukute nilipita sehemu ikaguswa na kitu kama mwiba ukaweka alama, sasa vitu kama hivyo mimi nimekataa kwenda kupiga rangi ili mteja akija aone gari katika uhalisia wake.

No.8. Madalali wengi wanaangalia plate no. Anakuja anasema bro hiyo gari yako namba C huwezi pata mteja wa 8m, mimi ukinipa 7.5m nakuletea IST yenye namba D. Wanasahau factors zingine kama utunzaji wa gari, mileage, ajali, na imetumika barabara zipi na kwa matumizi gani kabla haijauzwa. Unaweza kuletewa namba D mbovu kuliko hata namba C au B.
 
Labda tutabadilika, maana ukweli matapeli wanatumia m,wanya wa utamaduni wetu kutupiga sana. Watanzania sijui tumerithi wapi tabia ya kutokuwa wadadisi na kupenda vya rahisi. Yani kuna mtu kanunua coaster kwa sh, milioni saba. Hebu fikiria, huyu mtu timamu kweli?

Asante kwa kutukumbusha, asiyesikia na asikie!
 
Bado wapo binadamu waaminifu sana duniani. Nimenunua Brevis wiki mbili zimepita, jamaa aliyeniuzia akanambia niikague na kunipa wiki ya kuitumia na kwamba nikikuta ina tatizo la kiufundi nimrudishie. Gari hizi ni tamu balaa, they are eye catching luxury cars.
Brevis ni semi-luxury. Siku ukinunua AUDI au Mercedes Benz japo S-class ndio utaelewa maana ya luxury hivyo Tuliza wenge hilo.
BG421468_fa4028.jpg
BG421468_9fd3f2.jpg

 
Hivi ukinunua gari kwa mtu gharama ya kulipa TRA wakati wa kutransfer kadi inakuwa kiasi gani..maana nimesikia ni 18% ya bei uliyonunulia gari, sasa mfano nimenunua IST milion 9 nikilipa na 18% ya transfer inafika milion 10.6 , sasa hapa si bora niagize Japan au ikoje hapa
Umepigwa Mkuu.
 
Katika hizo, namba 8 na 10 zimenikuna. Unakuta mtu ana nunua gari namba C limechoka vibaya! Kwa wanaojua gari, body na Engine na Gear Box ni vitu vya msingi sana. Unakuta gari ni namba C lakini body limetoboka hadi unajiuliza kulikoni.

Watanzania wanapaswa kuelewa kwamba zile namba B,C, na D kwa sasa ni herufi tu na ni kiashiria kuwa gari limeingia nchini limekuta mfululizo gani wa namba( number Serie) lakini haina maana upya wa gari!
 
Back
Top Bottom