MUONEKANO WA MWEZI MWANDAMO WA IDDI = OBSERVING THE IDD CRESCENT

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
272
250
(English version at the bottom)
(Tafsiri kwa Kiingereza ipo chini)

Mwisho wa mwezi huu, watu watavutwa kuangalia angani jioni upande wa magharibi mara baada ya magharibi kutafuta Mwezi mwandamo ambao utakamilisha ibada ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wengine watavutiwa na sayari mbili ambazo pia zinang’aa angani mara baada ya giza kuingia. Sayari hizo si zingine ila ni sayari maarufu za Mushtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn). Mushtarii inang’aa vikali karibu na utosi, na Zohali inaonekana upande wa mashariki karibu na upeo. ingawa Zohali siyo kali sana, mwanga wake unavuta na ni wa kutulia, mbali na nyota ambazo humeremeta.

Wanaoamka mapema kwa ajili ya sala ya alfajiri na kwenda kazini wanashangazwa na sayari nyingie inayong’aa kwa ukali sana jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza. Syari hiyo ni Zuhura (Venus) ambayo kwa sasa ina jina la Nyota ya Alfajiri, na baada ya miezi kadhaa sayari hiyo hiyo itakuwa Nyota ya Jioni itapohama nafasi na kuingia katika anga ya Jioni

Kwa wakati huu Mwezi upo katika anga ya alfajiri jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza. Kila mwezi, Mwezi husogea nyuzi 12 angani, kwa hiyo ifikapo tarehe 23 Juni, Mwezi utakuwa bado upo anga ya alfajiri upande wa mashariki na hilali yake inatambulika ukiangalia vizuri. Siku ya pili, yaani tarehe 24, Mwezi utakuwa umesogea kiasi cha kuhamia upande wa pili wa Jua na kuingia katika anga ya jioni.

Wakati wa machweo jioni ya tarehe 24 Juni, Mwezi utakuwa mchanga sana, na hilali yake nyembamba kiasi cha asilimia 0.4% tu na nyuzi 7 jirani na upeo wa magharibi. Pamoja na hiyo, kwa vile anga ya magharibi huwaka sana wakati wa machweo kwa hiyo hilali changa hufunikwa kabisa ndani ya uang’avu wa anga. Kwa vile Mwezi unazidi kushuka upeoni muda unavyosogea ni vigumu sana kuuona Mwezi mwandamo siku hiyo.

Lakini jioni ya Jumapili tarehe 25 Mwezi utakuwa umesogea juu kwa nyuzi 12 zaidi, na kufikia nyuzi 20 juu ya upeo wa magharibi. Hilali ya Mwezi pia utatanuka kufikia asilimia 3.3% kwa hiyo kutakuwa na muda wa kutosha kabisa kuuona Mwezi hilali, mara giza litapoingia.

Kutafuta Mwezi mwandamo inabidi kuwa katika eneo lenye uwazi upande wa magharibi na kuanza kuangalia dakika kumi au kumi na tano baada ya magharibi ili kupata anga lenye giza ya kutosha. Kwa Dar es Salaam muda mzuri ni kuanzia saa 12:30 jioni, na upande wa pili wa Tanzania, sehemu za Kigoma, itakuwa baada ya saa 1:15 jioni.


VMwezi mwandamo wa Iddi wakati wa magharibi tarehe 24 na 25 Juni=.jpg


==xx==​

OBSERVING THE IDD CRESCENT

Towards the end of this month soon after sunset, the evening skies will draw the attention of millions looking out for the Idd crescent. Many others will also be attracted by two planetary jewels, Jupiter and Saturn that are also visible in the night skies as soon as the darkness sets in. Early risers, especially for those up for dawn prayers are dazzled by an extremely bright star that is the planet Venus. Looking out for the Idd crescent is done regularly by Muslims to complete their daily fasts of the holy month of Ramadhan. Celestial bodies provide the basis for the passage of time, and the Moon is closely followed for marking the lunar month.

Currently the Moon is in the early morning sky before sunrise. Each day the Moon shifts in the sky by 12 degrees, so by June 23 it will be quite close to the Sun and its crescent can just be seen at dawn. By the next day, 24 June, it will have shifted to the other side of the Sun and so will move out of the morning sky and enter the evening sky. By the evening of 24 June, the Moon will be near the western horizon and around 7 degrees above the setting Sun. However, the crescent will be extremely thin (0.4%) and hidden in the brightness of the setting Sun and extremely difficult to see directly.

However, on 25 June the Moon will be nearly 20 degrees above the setting Sun in the western horizon. Its crescent will be quite big (3.3%) and will be high in the sky once the sky is dark enough. Look for a flat open area with a clear view of the western horizon, and search for the crescent starting from around 6:30pm for observers along the eastern coast, and at later times for those in the interior, while for west Tanzania it will be after 7:15pm.

VIdd Moon at sunset 24 AND 25 June.jpg


==yy==​
 

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
272
250
tutaangalia kesho jioni ama Jumapili jioni
Kutafuta ni kuanzia kesho jioni, ila kesho Mwezi utakuwa chini sana karibu na upeo wa magharibi, kwenye angahewa iliyoangazwa na Jua lililozama tu upeoni.

Keshokutwa utakuwa juu kiasi cha kutoka kwenye mng'ao wa angahewa na kuwa ndani ya kiza.
 

privacy

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
1,345
2,000
Kuna hicho kitu kinaendelea nimeshindwa kujua ni nini ila juaa la saa saba kasoro lakini linatoa mwaka wa kama la Machweo nilipo

Picha hiyo sijaweka marekebisho yoyote ya rangi na hilo ndivyo anga linavyoonekana
 

Mikhail Tal

JF-Expert Member
May 12, 2016
255
500
Kuna hicho kitu kinaendelea nimeshindwa kujua ni nini ila juaa la saa saba kasoro lakini linatoa mwaka wa kama la Machweo nilipo

Picha hiyo sijaweka marekebisho yoyote ya rangi na hilo ndivyo anga linavyoonekana
Upo mkoa gani.. Maana hapa Dar mvua tu
 

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,574
2,000
Jana ni usiku wa 29 wa Ramadhani,ni Sikh ya witiri ya mwisho ya zile Sikh 10 za kuidowea Lailatul kadir,hii halo ya mvua na juwa kuwa dhaifu ukali wake ni katika alama ya kuwa Jana ilikua siku hiyo tarajiwa ya lailatul kadir
Taqabbali Llaha min aamalina
 

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
272
250
Kuna hicho kitu kinaendelea nimeshindwa kujua ni nini ila juaa la saa saba kasoro lakini linatoa mwaka wa kama la Machweo nilipo
Picha hiyo sijaweka marekebisho yoyote ya rangi na hilo ndivyo anga linavyoonekana

Picha hiyo sijaweka marekebisho yoyote ya rangi na hilo ndivyo anga linavyoonekana[/QUOTE]
Nadhani wingu nene lilikuja mbele ya Jua saa hizo. Ndio maana hata kamera iliweza kuvuta mviringo wa Jua. La sivyo picha yote ingejaa mwanga kwa vile Jua linatoa mwanga kali sana.
 

privacy

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
1,345
2,000

Picha hiyo sijaweka marekebisho yoyote ya rangi na hilo ndivyo anga linavyoonekana
Nadhani wingu nene lilikuja mbele ya Jua saa hizo. Ndio maana hata kamera iliweza kuvuta mviringo wa Jua. La sivyo picha yote ingejaa mwanga kwa vile Jua linatoa mwanga kali sana.[/QUOTE]

Ni kweli ila picha nilipiga kukiwa angavu zaidi maana pana wingu zito pia, na hilo ringi au mduara rangi yake ndio inayoshuka muonekano huo huo mpaka ardhini kama vile unaangalia kwa kutumia zile negative sijui kama ndio zilikuwa zinaitwa hvyo (Mikanda ya plastic iliyokuwa inatumika kipindi cha nyuma katika upigaji picha). Nilidhani kuna tukio katika anga linaendelea ndio maana nikauliza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom