Muonekano mpya wa Mfungwa Ole Sabaya huu hapa

Hakuna ajuaye kitakachomtokea, tusimlaumu
Ni kweli mkuu hakuna ajuaye kesho yake lakini kuna wanaofanya mambo kama wana hakika ya kesho yao. Sabay alikuwa mmoja wa watu wa aina hiyo.

Hii iwe somo kwa sisi wote tuliobaki. Be humble hujui kesho itakuwaje. Ukijiona wewe ndio mwamba na kutesa na kudharau wengine hakika ipo siku utalia na kusaga meno.

Najaribu kumhurumia huyu jamaa lakini ndio hivyo tena anamalizia kitabu chake alichoanza kukiandika muda mrefu. Matukio yake ya nyuma ndio yamempeleka alipo. Kama unabisha jiulize kwanini sio wengine ni yeye? Kwanini kila mtu alie nae?

Mwisho wa unaya ni majonzi na aibu. Hukumu hii na maswahibu haya ya Sabaya yatukumbushe kuishi vizuri bila kujali mamlaka na nguvu tulizonazo.
 
Na uendelee hivyohivyo kutupostia kila mfungwa.......

Jela haina Mwenyewe....

Vuta subra. Hata mimi nasubiri kushuhudia huo ujasiri wa kumpiga mvua yule jamaa anayetukera sana. Hii fursa ikipotea ndio basi tena.
 
Haya akikaa mwezi tuu akitoka amenyooka. Lulu leo amekua mke mwema kabisa kwa mumewe Majizo.
 
Alinyoaga kipanki akanona akajikutaga rais wa korea saiz nipara na kukondeana kawa mkulima alofulia ...hata akitoka Leo tayari amejitia aibu kubwa mmno!!
 
Wewe nae...

Yaani unaiba, usijue matokeo ya wizi...!!?

Unapiga na kunyanyasa watu kwa kutumia vibaya madaraka yako, usijue matokeo yake...!?

Unazini, usijue matokeo yake..!?

Unapora watu mali zao kwa nguvu usijue matokeo yake...!?

Hebu jaribu kuwa serious kidogo basi kila unapoandika kutoa hoja..!!
Ni uelewa mdogo mkuu na ulimbukeni wala huitaji degree kujua kwamba kile unachotoa ndio utakachopata kama umepanda mahindi huwezi kuvuna vanilla..!
 
Makonda naye ataburuzwa mahakamani lini? Naye alikuwa jeuri na mzabinazabina kwenye madaraka, huyo ndiye angeanza kwanza halafu hao wengine wafuate. Au ni itifaki inafuata wanaanza wa chini wakifuatiwa na wa juu? Iwe fundisho kwa vijana wanapopata madaraka makubwa wasiyatumie vibaya.
 
Kama ni mjinga ukiona hao Askari walivyo busy unaweza kufikiri kuwa Tanzania kuna mahakama.
 
Maisha ni mambo ya ajabu kwa kweli, Mkuu wa wilaya uliejipambanua kuwa ni muwakilishi mzuri wa Rais leo hii, Huna ata neno la kusema. Mungu akupe hekima.
 
Back
Top Bottom