Muone Mwenye Akili Bungeni Sio Toto Tundu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muone Mwenye Akili Bungeni Sio Toto Tundu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumbatu, Jul 7, 2012.

 1. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  [​IMG]


  MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa. Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.
  “Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa. Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?” Alihoji Othman.
  Akijadili bajeti ya wizara ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano, huko Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki wa Chama Cha (CHADEMA) Tundu Lisu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Zanzibar imefanya katiba kwa kujitangazia kuwa ni nchi.
  Othman alisema marekebisho ya katika ya Zanzibar yalikuja baada ya hoja nyingi ambazo hazikuwa na majibu katika muungano ambayo ilikuwa ikisema ni Zanzibar ni sehemu ya muungano, lakini kama nini mkoa? Shehia? Kata? au kijiji?, haya hayakuwa na jibu katika katiba ya muungano.
  Kufuatia maridhiano Zanzibar ndipo wazanzibari wakamaua kufanya kukufikia marekebisho ya 10 ya katiba yao ambayo ilifafanua kuwa zanzibar ni nchi na ndivyo ilivyo kwa sababu haikuwahi kutawaliwa kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanavyofikiria.
  “Marekebisho ya 10 ilichofanya ni kusema kwamba ikiwa mtu hatambui, maana ilikuwa imeshaonesha dalili kwamba kuna wengine hawatambui hilo tena wakubwa. Sasa marekebisho ya 10 yalipokuja ni kufafanua tu, kama kuna mtu hatambui sisi wenyewe tunajitambua” alisema mwanasheria huyo huku akiungwa mkono na wajumbe kwa kupigiwa makofi.
  Huku akishangiriwa na wajumbe wa baraza hilo mwanasheria mkuu alisema hakuna mtu ambaye atawazuwia kusema “Aaah katiba yenu isiwe namna gani au isiwe hivi na ndio maana unakuta katiba za muungano zipo nyingi lakini kila mmoja ina muundo wake kwa mujibu mlivyokubaliana nyinyi wenyewe”.
  Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.
  Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.
  Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.
  “Mheshimiwa Naibu Spika nitumie fursa hii hapa hapa niseme wakati tupo katika mchakato wa maoni ya katiba nadhani ni wakati mzuri kuiweka sawa ile misingi ya muugano kama Uswizi”. Na kuongeza kuwa.
  “Wakati mwengine napata wasiwasi nasema hii khofu yangu niiseme hapa kwamba tunaanza kubishana kuhusiana na watunza nyumba wawe wangapi, waendeshaji nyumba wawe wangapi, wawili, watatu, wanane au watano?. Lakini tatizo letu la msingi mimi nadhani ni nyumba yenyewe iweje. Kama tunaamua kuishi, maana mfumo wa sasa hivi mmoja anaishi nyumba kubwa na mwengine mabandani huko uwani huo sio utaratibu tunao”alisema mwanasheria.
  Aidha aliwaambia wajumbe hao kwamba wanzanzibari wana mambo ya msingi ya kujadili kuliko kuzungumzia idadi ya watunza nyumba akimaanisha kero za muungano zilizopo na kushindwa kuafikiwa.
  “Kwa hivyo mimi niwaombe sana waheshimiwa wajumbe, niwaombe na wazanzibari wenzangu na wananchi wote, kwamba huko mbele tusije tukalaumiana kwamba tumefanya marekebisho ya 10 kimakosa na tumejitangazia uhuru. Sasa hivi tuondoe fikra hizo lakini tunaweza kujieleza kwa hoja za msingi na mambo ya msingi katika hoja hii hapo ndipo tutakapojenga utawala bora ndani ya muungano” aliongeza Mwanasheria huyo.
  Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe hao kuhusu muungano Othman alisema hata suala la uraia limepewa kipaumbele katika katiba ya Uswizi ambapo mtu anapozaliwa ndipo anapopewa uraia wake.
  “Pale unapozaliwa ndio panapokupa uraia, na kuna mengi ambayo nadhani tatizo liliopo kwa wenzetu ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu” alisema Othman.
  Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano’ aliwaambia wawakilishi hao kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.
  “Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hutuba ya Mhe Tundu Lisu… lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na mhehsimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyesema kuwa maeelzo ya Mbunge Lisu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye” alisisitiza huku makofi ya wajumbe yakitawala ndani ya baraza hilo.
  Tokea kuanza kwa kikao cha baraza la wawakilishi kwa kiasi kikubwa mijadala wa bajeti umetawaliwa na suala la muungano ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakiungana na wananchi kudai maslahi zaidi kwa zanzibar ikiwemo kurejesha kwa hadhi ya rais wa zanzibar na mamlaka kamili ndani na nje ya nchi.
   
 2. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.
  Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.
  Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa muda mrefu UAMSHO na washirika wake wamekuwa wanaita Tanganyika 'koloni'. Na mara nyingi sana wamekuwa wanasema wanataka waachwe 'wapumue', wanataka ;uhuru'. Hata ndani ya baraza la wawakilishi Mh Mansour amenukuliwa akisema hivyo (rejea hansard).

  Sasa huyu Othman anapingana na madai ya UAMSHO na hata Mwakilishi? Ni walikuwa na maana gani kusema Tanganyika ni koloni? Ni kitu gani alichosema Lissu ambacho ni tofauti na madai ya UAMSHO?

  Mimi nadhani kuna watu Zanzibar wanafikiri ni wajanja sana. Mwanzoni walikuwa wanadai kura ya maoni kuhusu muungano maana walitaka kuachana na 'koloni' sasa baada ya kuoneshwa 'bill' wamejigeuza kama kinyonga wanata serikali mbili na muungano wa mkataba.

  Sasa wafuate mkataba Jumuiya ya Afrika Mashariki. LET ZANZIBAR GO!

  NB: Huyu Othman si ndiye mume wake Batilda?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Huyo mwanasheria alisema kama Swiss na viti vingapi umoja wa Mataifa? Au Swiss wana safaru ngapi?
   
 5. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Soma vizuri hansard kuachiwa kupumua na uhuru ni vitu viwili tofauti usiwe mvivu wa kufikiri
   
 6. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Ni kwa sababu tumezaa na dada zenu hatuwezi kuacha damu yetu ikaingia ujingani
   
 7. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  So what?
   
 8. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Huyu ndio sifuri kweli, anasema Zenji haijawahi kutawalia? hajui kuwa ilikuwa inatawaliwa na Tanganyika!? ndio wakajipatia uhuru wa mabadiliko ya 10?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuachiwa kupumua ni kwa Mansour, uhuru ni UAMSHO. Ningeshukuru kama ungeacha personal attack na kujikita kwenye hoja.
   
 10. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Usiwe mvivu wa kufikiri maana yake tunaweza kuwa na muungano wakati zanzibar ikiwa kivyake tuasharikiana yale mambo ya msingi tu kila mmoja atakuwa na maamuzi yake ikiwa pamoja na veto kupinga lolote lislo na maslahi kwa zanzibar
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  let zanzibar go!!!
   
 12. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  mpaka kieleweke ikiwa ni pamoja na Tanganyika kubeba madeni ya iliyokuwa Tanzania ndio mliokopa sio sisi
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sina tatizo hapo kwenye red kwamba kila pande mbili zishirikiane kwenye mambo ya msingi kwa kuzingatia maslahi ya kila mmoja. Hata hivyo swali langu bado liko pale pale, Swiss wana viti vingapi UN, na Swiss wana safaru ngapi? I am using your state attorney's argument.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Wala usipate tabu, tumekuwa tunabeba madeni kwa miaka 48 including bill yanu TANESCO. But let me tell you one thing, kwa mtu mzima kulipiwa bill si jambo la heshma hata kidogo ndio maana hata huku bara wabunge wanapiga kelele kuhusu bajeti Tegemezi! Sijui huko mnatafsiri vipi kitendo cha kulishwa na mzazi mwenzako?
   
 15. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  hamtulishi mnatupa kilicho chetu msijifanye wajanja mna deni kubwa kwenu nyinyi msikimbie deni miaka 48 mmetuzulumu kwenye gawio na malipo ya mrahaba
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ni kiasi gani mchangia kwenye ulipaji wa madeni? Ni kiasi gani mnachangia kuendesha wizara za muungano? Binafsi nawatakia Zanzibar heri na nafaka tele huko mbeleni, ni wakati sasa muwe 'huru' au ukitaka 'kupumua'. Na kwa haki hiyo hiyo ni wakati sasa Tanganyika kutua mzigo.

  LET ZANZIBAR GO!!!
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mtumbatu amekimbia ile thread nyingine, hapa ni JF huwezi kujificha tutakupa vidonge huko huko.

  FJM, ukimsikiliza Mwanasheria wa ZNZ kama ilivyo wajumbe wa BLW hakujibu hoja hata moja zaidi ya kutafuta mipasho.
  Alichosema Tundu kimoja kati ya vingi ni kuwa ZNZ haina jeshi wala Polisi kwasababu hailipi hata senti tano kwa ulinzi na usalama wa raia. Hapo ndipo kwanza alipaswa kufikri kabla ya kutamka kuwa ni nchi. Haina chombo cha dola! kilichopo ni wafadhili tu.

  Alipaswa adadavue hoja za Tundu lisu badala ya kusema tu kuwa anahadaa. Anahadaa nini? Gharibu Bilal si huyo amekomba bilioni 4 na Bilioni 32 zinajadiliwa na BLW yeye akiwemo. Hapo kuna hadaa gani.

  Labda tumhabarishe kuwa Mshahara wa mwanasheri wa ZNZ na BLW unapelekwa kwa meli, yeye hana mshahara wa SMZ, sasa hapo hadaaa ipo wapi.

  Kwamba, wao wanabeba asilimia 7 wakati wanachangia silimia 0, hapo hadaa ipo wapi
  Kwamba bajeti yao ni fedha za Mtanganyika, hapo hadaa ipo wapi
  Kwamba watoto wao wanasoma buree! hapo hadaa ipo wapi

  Cha kusikitisha sana anaongelea muungano wa Swiss, kwanini asilete mswada akiwa kama mwanasheria kuvunja muungano. Anchoogopa ni kitu gani.
  Mwanasheri anatakiwa ajibu hoja si mapisho.

  Anapoongelea uraia kuwa ni ule pale mtu anapozailiwa, mwanasheria wa BLW ameshaingiwa na kiwewe kama kiwewe kinachowakumba WZNZ. Wanajua kuwa muungano ukifa itabidi waishi bara kama raia wa nchi nyingine.
  Sasa hapa ni hofu tu maana Tundu Lissu hakuliongelea hilo.

  Mwambieni mwanasheri alete mswada wa kuvunja muungano, vinginevyo atulie tuli mshahara utavuka bahari tu.

  Sisi tunasema LET ZNZ GO! Hatuhitaji Mkataba wa EU, SWISS ua upuuzi mwingine. Hatuwahitaji ni wao kuamua tu.
  Wakishindwa basi watulie katika kivuli cha Tanzania.

  LET ZNZ GO!
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Hata makusanyo ya kodi yanabakia huko huko na bado wanapekelewa hela. Hoja za mwanasheria mkuu ni zi ajabu sana maana hajajikita kwenye vifungu vya sheria badala yake anaongea kama mtu ambaye hana uelewa wa sheria. Kama wanatamani muungano unaofanana na wa Swiss kimewashinda nini kupeleka muswada BLW na kumaliza kazi badala ya hizi ngonjera zisizoisha?
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  FJM, inasikitisha sana kuona mwanasheria wa SMZ anaongea hovyo tu bila kujibu hoja kama yupo kijiweni. Hakujibu hoja hata moja, alichokisema ni Mipasho! Mwanasheria huyu wa SMZ!

  Mwanasheria wa SMZ anajaribu kubadili equation baada ya hoja za msemaji Ahmed Rajabu kugonga mwamba.
  Walianza na serikali 3 tukawauliza zihudumiwe vipi, hawana jibu wakakimbia. Hata mwanaseria wa SMZ haana jibu
  Wakaja na Mkataba, tukauliza uhusu nini kitakachofaidisha wote, wakafyata, hawana jibu
  Wakaja na uhusiano kama wa EU, tukawaambia uhusiano huo kwanini usiwe ndani ya EAC, hawana jibu
  Wakaja na hoja ya kudai ukanda wa pwani, Mkuu Kichuguu amewapa somo zuri ile thread nyingine na natumaini Mwanasheria wa SMZ ambaye amesoma Bure kwa kodi za Mtanganyika ataielewa.
  Sasa Mwanasheria wa SMZ amekuja na CD mpya ya muungano wa SWISS. Hili nalo hana jibu, uweje na kwa faida ipi

  Kila siku wanatoa 'single' sasa album tayari, wasichoweza ni kuuza album hiyo Tanganyika ikawaelewa.
  Huwezi kutengeneza album ya plastiki halafu uuze ili anayenunua aitengeneze vizuri. Tutanunua album pale ZNZ itakapotuambia inaweka nini mezani kwanza. Kama wanaweka 'zero' tunasema LET ZNZ GO!

  FYI huyu Mtumbatu ametumwa na Mzalendo.net kupima kina cha maji.
  Kwa taarifa kina cha maji ni kirefu sasa ni wakati mjiandae kuondoka, hatukubali tena upuuzi wa kuwabebea mgongoni huku mkicheza ngoma za msewe.

  Mwanasheria wa SMZ? Lete mswada wa kuvunja muungano, kinyume chake unaidhalilisha taaluma ya sheria, akina Takashi, Nonda, Jussa, Ahmed Rajabu na wengine. Unalidhalilisha BLW kwasababu kama mwanasheria anaongea hivyo, vipi mwana UAMSHO!
   
 20. F

  Falconer JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hahhahaah nyinyi muna kichekesho sana. Mswada wa kuvunja muungano unakuja kwani muna haraka ya nini. Wazanzibari munawajua au munawasikia tu. Sisi tuna akili zetu. Tunajua kuna vikosi vingapi na nia ni kufanya nini. Tuliamka zamani ndio maana tunakwenda mdogo mdogo mpaka kieleweke. Muungano mutauvunja nyinyi wenyewe. Ukiangalia nyuma, alieshikilia muungano huu ni Julius Nyerere. wazanzibari hawajataka muungano. Hakuna pahali raisi wa zanzibar alitia saini ya muungano. Hata barua ya UN haina signature ya zanzibar. Ilikuwa ni wizi wa mchana.
   
Loading...