Ulisema tukiomba tutapewa. Tukitafuta tutaona. Tukibisha tutafunguliwa. Kwa nini haya yanatokea kwenye ardhi yako iliyojaa baraka zisizo kifani...Lakini tunajipa moyo. Jambo jema ni kuwa tunaamini dunia itapita na mambo yake. Na zaidi sana tunaamini hakika mtetezi wetu yu hai, naye hatatuacha tuangamie kabisa. Hatutokata tamaa. Kwani muda wako Mungu wetu ni muda sahihi.