Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Habari wakuu!

Mungu wa kweli, mwenye uweza wote, na aliyeumba kila kitu hahitaji mambo yafuatayo:-

1. Hahitaji Zaka wala Sadaka
Mungu wa kweli si mhitaji, uhitaji ni karba ya viumbe. Mungu hana anachohitaji kutoka kwa kiumbe. Yeye ndiye huamua nini kiwe na nini kisiwe. Mungu wa kweli hahitaji sadaka kama watu wengi wanavyoaminishwa. Hahitaji zaka kama wachungaji wanavyosema. Wachungaji wanamsingizia Mungu mambo mengi ikiwemo hili la zaka na sadaka. Wanachoshindwa kusema ni kuwa wao ndio wanahitaji hizo zaka na sadaka kama sehemu ya huduma yao. Ni uongo na dhambi kubwa kusema Mungu anataka sadaka na zaka jambo ambalo linamdhalilisha Mungu muweza wa yote.

Wachungaji, mashehe na viongozi wote wa dini kwa majina yao. Muache kuhadaa watu na kumdhalilisha Mungu. Tutatoa sadaka na zaka kwa kujua kuwa mnatupa huduma za kiroho na si kusema kuwa Mungu anahitaji sadaka na zaka tena fungu la kumi. Kama tunawalipa waalimu, madaktari, wanasheria na kada zingine iweje tusiwalipe nyie. Kwa nini mumsingizie Mungu mambo ya uongo. Eti fungu la kumi ni la Mungu. Si kweli. Mtu atatoa zaka na sadaka kulingana na umuhimu wa huduma anayoipata na si kumtishia vitisho vya uongo.

2. Kafara si ondoleo la dhambi
Watu wameaminishwa kuwa eti ili mtu asamehewe dhambi basi sharti amwage damu. Zamani walimwaga damu ya wanyama lakini sasa hivi wanaamini kuwa Yesu(mtu ninayemheshimu sana) alikufa kwa ajili ya watu jambo ambalo ni uongo. Mungu wa kweli hawezi kufikiri achilia mbali kutenda jambo kama hilo. Hiyo ni mila za kuabudu miungu ya Kiyahudi ambayo msingi wake mkuu umetokana na Abrahamu aliyechukua baadhi ya mila za Kiashuru( kwa sasa ni Syria). Miungu ya Abrahamu ndiyo ilimtaka amtoe Isaka kafara kama ilivyodesturi.

Mungu wa kweli hahitaji mchakato huo kusamehe dhambi, na kumwaga damu si suluhu ya dhambi kuishi. Kwa kutambua hili jambo hili moja kwa moja linaonekana ni wazo la kibinadamu zaidi kuliko la Mungu.

3. Maombi hayabadili chochote kwa Mungu mwenye uweza.
Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengine kwa majina yao wanawadanganya watu kuwa ukimuomba Mungu jambo lolote anaweza akakupa kitu ambacho si kweli hata kidogo. Vile Mungu alivyopanga kabla hajakuumba ndivyo itakavyokuwa. Kusema kuwa ukimuomba Mungu anabadili mipango yake ni kujidanganya na kupoteza muda. Kumuomba Mungu ni kumfundisha namna ya kufanya mambo yake. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa mtu akiomba jambo kwa Mungu hupewa isipokuwa ushahidi uliowazi ni kuwa Mtu akifuata maagizo ya Mungu na sheria zake ndio hupata akitakacho. Mungu anataka watu wafuate sheria zake na si kuomba omba tuu.

Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini jukumu lao ni kuwafundisha watu sheria za Mungu na si kuwadanganya waombe au kuwaombea. Kuwaombea watu ni kuwafundisha uvivu. Na kuamini katika hamna.

Ukitaka uamini nikisemacho, kaa ndani omba alafu usiende kufanya kazi uone kama Mungu atakupa ukitakacho, alafu mwenzako asiombe aende kufanya kazi uone nani atapewa/atapata. Hakuna sheria ya Mungu mahali popote kwenye torati inayomtaka mtu aombe. Tafsiri yake nadhani mnaelewa ni nini. Usishangae kwa nini bara la Afrika ni masikini ilhali ndilo linaloongoza kwa waumini wenye kuomba makanisani na misikitini. Jibu unalo.

4. Wachungaji/mashehe na viongozi wa dini si watu pekee wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kuna dhana watu huaminishwa kuwa kundi fulani la watu ndilo linalotakiwa kupewa heshima kuliko kundi jingine. Huu ni uongo mkubwa. Mchungaji ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine. Anahudumia watu kama wanavyohudumia wengine. Hana uspesho wowote zaidi ya wao kuwahadaa watu wenye akili ndogo na wasioujua ukweli ndio maana wamegeuka watumwa wa makuhani na mashehe. Kila mtu duniani anahitaji heshima ikiwa anafanya kazi ya kuhudumia wengine. Iwe ni fundi nguo, fundi magari, mbunge, mwalimu, muuguzi, mhandisi wote wapo sawa na wote wanategemeana. Kumpa mtu fulani heshima kuliko mwingine si tu kwamba ni ukosefu wa maarifa bali ni kuonyesha hali ya kutoujua ukweli.'

Viongozi wa dini wamejipa hadhi kubwa na kujiona wao ndio wenye mamlaka. Usishangae kiongozi wa dini mjinga akisema kuwa anakulaani kwa Mungu. Nikisiaga hivi huwa nacheka sana. Mtu hupata laana kwa kuacha sheria za Mungu na si maneno ya Mchungaji au mzazi. Kwa ujumla ni kuwa mtu hujilaani yeye mwenyewe ikiwa ataacha sheria za Mungu.

Hivyo watu wamejikuta wakiwaogopa wanadamu wenzao kwa kutoujua ukweli. Unamuogopa mtu aliyezaliwa na mwanamke? Mtu anayehitaji chakula ili apate nguvu ya kuishi. Unakuta mtu anaenda kanisani anaitwa na mchungaji mbele ya kanisa na kutabiriwa vitu vya uongo na yeye anasema kweli wakati sio kweli. Kwa mfano;
Mchungaji: wewe unatatizo la ugumba
muumini: Kweli
Mchungaji: Mama yako anakuloga
Muumini: Kweli
wakati yote ni uongo, anasema kweli kwa uoga na utumwa wa kifikra.

Wito wangu, lazima watu waishi kwa kupendana na kuzishika amri na sheria za Mungu ili wapate kuwa huru na maisha. Vinginevyo tutabaki kuwa watumwa na kuona sisi ni wasindikizaji wakati wengine ndio walioumbiwa huu ulimwengu jambo ambalo si kweli
Hata mungu aliumba ulimwengu kwa kujitolea ni sadaka, kunyesha kwa mvua ili maji yajaze mito, mimea ipateota, wanyama wale mimea na kunywa maji, na binadamu aweze kuwa nyama, kula mimea, kunywa na kuoga maji ni Sadaka. Sadaka ni Guludumu, Binadamu ni nani aache kutoa sadaka na Zaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja yako ni ya ajabu sana!!, Mungu kujua kwamba Firauni atakuwa jeuri hakuhusiani na yeye Firauni kuwa jeuri, yaani hali hiyo siyo "cause and effect", mfano wa "cause and effect" ni huu hapa; mtu uking'atwa na mbu mwenye vimelea vya malaria matokeo yake utapata malaria, hapo cause ni kung'atwa na mbu na effect ni kupata malaria. Sasa Mungu kujua kama Firauni angekuwa jeuri siyo cause ya Firauni kuwa jeuri, ujeuri wa Firauni au mtu yeyote ni kazi ya dhamira ya matendo ya mtu mwenyewe.

Hapa naomba nifafanue zaidi, ni kwamba hata mtu yeyote atende wema naye atahukumiwa kwa malipo mema kutokana na wema aliotenda, swali ni hili kwanini Mungu asilipwe thawabu kutokana na huo wema wa huyo mtu kwasababu ni Mungu ndiye aliyemuumba huyo mtu huku akijua kuwa huyo mtu angekuwa mwema.------- hapo ninakuonyesha "counter argument" ya hoja yako.

Hilo Swali lako wewe siyo mtu wa kwanza kuuliza na unayo mapungufu fulani ya MSINGI katika elimu ya dini ndiyo yamepelekea wewe kutoa hiyo hoja dhaifu nikipata wasaa nitajaribu kuweka hiyo misingi ndipo utaelewa hekima yote.

Ila lazima utambue, mtu atakaye hukumiwa mbele ya Mungu ni yule aliyefanya mema au mabaya huku akitambua kuwa anachofanya ni wema au ubaya, na kutokana na wema mtu atalipwa thawabu na kutokana na ubaya mtu ataadhibiwa. Mtu hawezi kuhukumiwa kwa kulipwa thawabu au adhabu akitenda wema au ubaya bila kujua/bila kudhamiria.

Bottom line ni kwamba, mema au mabaya ya mtu ni kutokana na utashi wa mtu mwenyewe na Kujua kwa Mungu hakuna mahusiano yoyote na utashi na dhamira ya huyo mtu.

Mimi ninakujua wewe "dogo" Sasa utauliza swali hili, "kwanini Mungu aumbe watu ambao anajua hatimaye watakuwa watu waovu??"😁😁😁

Mimi ninakuita "dogo" kwa sababu maswali yako ni madogo.
Matokeo ya mechi yanajulikana , kuna haja gani ya kuingiza team uwanjani ? wewe jitoe akili tu Mungu anafahamu firauni kabla ata ajamuumba kuwa atakuwa mtu wa jeuri, sasa firauni ana ubavu gani wa kubadilisha kile Mungu alichotaka kuwa awe mtu jeuri? wewe rukaruka lakini utachezea sana za uso hapa ahahaahahahahahahajajjajj unaleta mifano ya kitoto kwenye mambo yaliyokuzidi umri
 
Ingiza team tu usiwe na khofu, watazamaji wanayohamu ya kuuona mechi,

Sasa kama hilo ndilo swali lako, mbona nilishakujibu, kwamba Mungu kujua kwake kama Firauni angekuwa muovu hakuhusiani kabisa na yeye Firauni kuwa muovu, nikakupa mfano (counter argument) kwamba kama ingalikuwa kujua kwa Mungu kwamba fulani atakuja kuwa muovu kabla hajamuumba ni Mungu anatakiwa abebe makosa ya huyo mtu basi hata kwa mtu mwema pia Mungu angepaswa apewe thawabu pia, kwanini wewe umeshikilia tu kwa ajili ya mtu muovu??, au wewe nawe ni mtu muovu nini??!!.

Uovu au wema wa mtu hutokana na dhamira ya matendo yake mwenyewe na hapo Mungu hausiki japo anajua kabla mtu huyo hajatenda chochote hata kabla hajamuumba.

Angalia huu mfano, wewe umeandika maneno hapo juu kunijibu hebu niambie ni nani aliyekushurutisha kuandika??, kama yupo toa ushahidi.

Mwishowe yakupasa ujue hekima ya wewe kuwepo hapa duniani, na hekima ya hatima yako baada ya kuondoka duniani ukufahamu mambo hayo wala maswali madogo unayouliza hutouliza tena.

Pia Kumbuka "cause and effect" phenomenon.
 
Team naingiza ila nawachosha maana hawawezi badili matokeo "; Ahahahahahhhaahahahaha
HALAFU ; mbona huyu Mungu unamshusha labda nikuulize swali jepesi maana unatia huruma, Mungu alikua anafahamu firauni ni mtu wa motoni kabla ajamuumba au baada ya kumuumba ? utaelewa tu
 
Alikuwa anajua, kwasababu sifa yake ni kutokuwa na muda (a reference time frame) yaani yeye hana muda uliopita, muda wa sasa na muda ujao, yeye kwake muda ni uleule (kitu kimoja) ndiyo maana anajua ya kabla, ya sasa na ya baada ya kuumba----na hiyo ndiyo sifa ya Mungu ambayo ha- share na yeyote.

Kumbuka, kujua kwake kabla hajaumba hakuna mahusiano yoyote na matendo ya mtu. (There is no cause and effect phenomenon in that case), ni hivi, cause and effect ni kama: kunywa sumu na kufa, kunywa sumu ni "cause" na kufa ni "effect" kwa hiyo kuna mahusiano kati ya sumu na kifo. Nadhani kwa mfano huo utakuwa umeelewa nini maana ya "cause and effect" (sababu na matokeo).

Nataraji hutaulizwa tena swali kama hilo.
 
Unadhani misikiti na makanisa yataendeshwa vipi tusipotoa zaka na sadaka?
masheikh na mapadre watakula wapi?
Yesu na mitume wengine wa zamani walikula vip?. Jamaa alibadili mikate mitano na samakii wawili na kulisha maelfu mkuu. KWA SASA HV KAZI WALIZOFANYA MITUME WA ZAMANI BURE LEO HII WATU WANAFANYA TENA KWA MALIPO YA JUU SANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa anajua, kwasababu sifa yake ni kutokuwa na muda (a reference time frame) yaani yeye hana muda uliopita, muda wa sasa na muda ujao, yeye kwake muda ni uleule (kitu kimoja) ndiyo maana anajua ya kabla, ya sasa na ya baada ya kuumba----na hiyo ndiyo sifa ya Mungu ambayo ha- share na yeyote.

Kumbuka, kujua kwake kabla hajaumba hakuna mahusiano yoyote na matendo ya mtu. (There is no cause and effect phenomenon in that case), ni hivi, cause and effect ni kama: kunywa sumu na kufa, kunywa sumu ni "cause" na kufa ni "effect" kwa hiyo kuna mahusiano kati ya sumu na kifo. Nadhani kwa mfano huo utakuwa umeelewa nini maana ya "cause and effect" (sababu na matokeo).

Nataraji hutaulizwa tena swali kama hilo.
Braza embe acha bange yaani Mungu anajua firauni anaenda motoni halafu ashindwe kujua ni kitu gani kitamfanya aende motoni ? cause and effect ni kwako wewe sio Mungu ,ahahahhaahahajaajajjaa Mungu anajua mpaka lita ngapi za maji utakunywa , punje ngap za mchele utakula halafu uniambie "kujua kwake kabla hajaumba hakuna uhusiano yeyote na matendo ya mtu"; wewe una mshusha Mungu hadhi kabisa, kujua kwake kuna uhusiano na matendo ya mtu kabisa vinginevyo huyo Mungu ajui future
 
Mbona unaifagilia bangi sana, au unavuta??!!,

Umeshaelewa somo ila naona kilichobakia ni mbwembwe tu, huna hoja tena.
 
Braza acha kurukaruka jibu swali , inawezekana vip Mungu ajue firauni anaenda motoni , halafu asiweze kujua vitu gani vitampeleka motoni? huyo Mungu unae msema wewe hajui future ahahahahahaahha ni sawa na kusema Mungu huyo anajua matokeo lakini wafungaji wa magoli hawajui !! Braza acha vituko
 
Nasema hivi kama wewe ni bado mwanafunzi basi huko Shuleni ni kilaza, lakini kama ulishamaliza shule/chuo basi ulikuwa kilaza au uliwasumbua sana walimu wako.
Sijui kama unao uelewa wa kutosha;, Mimi nilisema hivi katika posts za nyuma kuwa Mungu hana muda kama tulionao sisi binadamu, Yeye muda wake ni mmoja tu, yaani hana jana, leo au kesho, yeye jana,leo na kesho ni kitu kimoja ndiyo maana anajua kila kitu kilivyokuwa, kilivyo sasa na kitakavyokuwa hapo baadaye, kwa msingi huo Mungu anajua kila kitu, mfano hata wewe kama utavuta bangi kwa hiyari yako miaka kadhaa ijayo, basi Mungu anajua sasa hivi na anajua hadi mtu atakayekuuzia na anajua ela ya kununulia utapata wapi na vipi nk,

Ndiyo maana anaitwa "al ghuyuub".yaani mwenye elimu ya ghaibu.

Kama hutoelewa hapo niambie wewe ni kabila gani, labda nitakuwa najua kilugha chako ili nikufahamishe kwa kilugha chako huenda ukafahamu vyema "for we are told by psychologists that a person understands better in his mother tongue language".

Umeshaelewa nini maana ya "cause and effect",na ushaelewa kuwa Kujua kwa Mungu juu ya mabaya au mema atakayotenda mtu hayahusiani na Mungu kujua hiyo mabaya na mema ya mtu.

Nasubiri uulize swali hili:- kwanini Mungu aumbe mtu anayejua kuwa atakuwa muovu???😁😁😁
 
Jokajeusi lipo kazini, hiyo mada inaakisi jina lako, yaani hoja zako nizakimpinga kristo sijui umelitambua hilo au umeandika tu.

Kama binadamu sisi kwa sisi tunaombana kwanini tusimuombe Mungu ili naye atupe yale ambayo unazani binadamu mwenzangu hawezi kunisaidia.

Unaposema kafara haitajiki, umeshajiuliza waganga wamekopi wapi kutoa kafara ili kuwasaidia wateja wao wanapoleka maombi ya shida zao, kwamba bila kafara mganga hafanyi Kazi yako, umeshajiuliza why?

Unahitaji kujitazama upya kama umaanisha kweli hiki ulichokoposti bado unanafasi ya kujilekebisha, always Mungu hutupa second chance to repent kabla ule mwisho haujafika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu!

Mungu wa kweli, mwenye uweza wote, na aliyeumba kila kitu hahitaji mambo yafuatayo:-

1. Hahitaji Zaka wala Sadaka
Mungu wa kweli si mhitaji, uhitaji ni karba ya viumbe. Mungu hana anachohitaji kutoka kwa kiumbe. Yeye ndiye huamua nini kiwe na nini kisiwe. Mungu wa kweli hahitaji sadaka kama watu wengi wanavyoaminishwa. Hahitaji zaka kama wachungaji wanavyosema. Wachungaji wanamsingizia Mungu mambo mengi ikiwemo hili la zaka na sadaka. Wanachoshindwa kusema ni kuwa wao ndio wanahitaji hizo zaka na sadaka kama sehemu ya huduma yao. Ni uongo na dhambi kubwa kusema Mungu anataka sadaka na zaka jambo ambalo linamdhalilisha Mungu muweza wa yote.

Wachungaji, mashehe na viongozi wote wa dini kwa majina yao. Muache kuhadaa watu na kumdhalilisha Mungu. Tutatoa sadaka na zaka kwa kujua kuwa mnatupa huduma za kiroho na si kusema kuwa Mungu anahitaji sadaka na zaka tena fungu la kumi. Kama tunawalipa waalimu, madaktari, wanasheria na kada zingine iweje tusiwalipe nyie. Kwa nini mumsingizie Mungu mambo ya uongo. Eti fungu la kumi ni la Mungu. Si kweli. Mtu atatoa zaka na sadaka kulingana na umuhimu wa huduma anayoipata na si kumtishia vitisho vya uongo.

2. Kafara si ondoleo la dhambi
Watu wameaminishwa kuwa eti ili mtu asamehewe dhambi basi sharti amwage damu. Zamani walimwaga damu ya wanyama lakini sasa hivi wanaamini kuwa Yesu(mtu ninayemheshimu sana) alikufa kwa ajili ya watu jambo ambalo ni uongo. Mungu wa kweli hawezi kufikiri achilia mbali kutenda jambo kama hilo. Hiyo ni mila za kuabudu miungu ya Kiyahudi ambayo msingi wake mkuu umetokana na Abrahamu aliyechukua baadhi ya mila za Kiashuru( kwa sasa ni Syria). Miungu ya Abrahamu ndiyo ilimtaka amtoe Isaka kafara kama ilivyodesturi.

Mungu wa kweli hahitaji mchakato huo kusamehe dhambi, na kumwaga damu si suluhu ya dhambi kuishi. Kwa kutambua hili jambo hili moja kwa moja linaonekana ni wazo la kibinadamu zaidi kuliko la Mungu.

3. Maombi hayabadili chochote kwa Mungu mwenye uweza.
Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengine kwa majina yao wanawadanganya watu kuwa ukimuomba Mungu jambo lolote anaweza akakupa kitu ambacho si kweli hata kidogo. Vile Mungu alivyopanga kabla hajakuumba ndivyo itakavyokuwa. Kusema kuwa ukimuomba Mungu anabadili mipango yake ni kujidanganya na kupoteza muda. Kumuomba Mungu ni kumfundisha namna ya kufanya mambo yake. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa mtu akiomba jambo kwa Mungu hupewa isipokuwa ushahidi uliowazi ni kuwa Mtu akifuata maagizo ya Mungu na sheria zake ndio hupata akitakacho. Mungu anataka watu wafuate sheria zake na si kuomba omba tuu.

Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini jukumu lao ni kuwafundisha watu sheria za Mungu na si kuwadanganya waombe au kuwaombea. Kuwaombea watu ni kuwafundisha uvivu. Na kuamini katika hamna.

Ukitaka uamini nikisemacho, kaa ndani omba alafu usiende kufanya kazi uone kama Mungu atakupa ukitakacho, alafu mwenzako asiombe aende kufanya kazi uone nani atapewa/atapata. Hakuna sheria ya Mungu mahali popote kwenye torati inayomtaka mtu aombe. Tafsiri yake nadhani mnaelewa ni nini. Usishangae kwa nini bara la Afrika ni masikini ilhali ndilo linaloongoza kwa waumini wenye kuomba makanisani na misikitini. Jibu unalo.

4. Wachungaji/mashehe na viongozi wa dini si watu pekee wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kuna dhana watu huaminishwa kuwa kundi fulani la watu ndilo linalotakiwa kupewa heshima kuliko kundi jingine. Huu ni uongo mkubwa. Mchungaji ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine. Anahudumia watu kama wanavyohudumia wengine. Hana uspesho wowote zaidi ya wao kuwahadaa watu wenye akili ndogo na wasioujua ukweli ndio maana wamegeuka watumwa wa makuhani na mashehe. Kila mtu duniani anahitaji heshima ikiwa anafanya kazi ya kuhudumia wengine. Iwe ni fundi nguo, fundi magari, mbunge, mwalimu, muuguzi, mhandisi wote wapo sawa na wote wanategemeana. Kumpa mtu fulani heshima kuliko mwingine si tu kwamba ni ukosefu wa maarifa bali ni kuonyesha hali ya kutoujua ukweli.'

Viongozi wa dini wamejipa hadhi kubwa na kujiona wao ndio wenye mamlaka. Usishangae kiongozi wa dini mjinga akisema kuwa anakulaani kwa Mungu. Nikisiaga hivi huwa nacheka sana. Mtu hupata laana kwa kuacha sheria za Mungu na si maneno ya Mchungaji au mzazi. Kwa ujumla ni kuwa mtu hujilaani yeye mwenyewe ikiwa ataacha sheria za Mungu.

Hivyo watu wamejikuta wakiwaogopa wanadamu wenzao kwa kutoujua ukweli. Unamuogopa mtu aliyezaliwa na mwanamke? Mtu anayehitaji chakula ili apate nguvu ya kuishi. Unakuta mtu anaenda kanisani anaitwa na mchungaji mbele ya kanisa na kutabiriwa vitu vya uongo na yeye anasema kweli wakati sio kweli. Kwa mfano;
Mchungaji: wewe unatatizo la ugumba
muumini: Kweli
Mchungaji: Mama yako anakuloga
Muumini: Kweli
wakati yote ni uongo, anasema kweli kwa uoga na utumwa wa kifikra.

Wito wangu, lazima watu waishi kwa kupendana na kuzishika amri na sheria za Mungu ili wapate kuwa huru na maisha. Vinginevyo tutabaki kuwa watumwa na kuona sisi ni wasindikizaji wakati wengine ndio walioumbiwa huu ulimwengu jambo ambalo si kweli
UMEPATIA 2,3,NA 4. KATIKA NAMBA MOJA RUDI KASOME QUR'AN TENA AU BIBLE TENA! SAWA MKUU?
 
Nasema hivi kama wewe ni bado mwanafunzi basi huko Shuleni ni kilaza, lakini kama ulishamaliza shule/chuo basi ulikuwa kilaza au uliwasumbua sana walimu wako.
Sijui kama unao uelewa wa kutosha;, Mimi nilisema hivi katika posts za nyuma kuwa Mungu hana muda kama tulionao sisi binadamu, Yeye muda wake ni mmoja tu, yaani hana jana, leo au kesho, yeye jana,leo na kesho ni kitu kimoja ndiyo maana anajua kila kitu kilivyokuwa, kilivyo sasa na kitakavyokuwa hapo baadaye, kwa msingi huo Mungu anajua kila kitu, mfano hata wewe kama utavuta bangi kwa hiyari yako miaka kadhaa ijayo, basi Mungu anajua sasa hivi na anajua hadi mtu atakayekuuzia na anajua ela ya kununulia utapata wapi na vipi nk,

Ndiyo maana anaitwa "al ghuyuub".yaani mwenye elimu ya ghaibu.

Kama hutoelewa hapo niambie wewe ni kabila gani, labda nitakuwa najua kilugha chako ili nikufahamishe kwa kilugha chako huenda ukafahamu vyema "for we are told by psychologists that a person understands better in his mother tongue language".

Umeshaelewa nini maana ya "cause and effect",na ushaelewa kuwa Kujua kwa Mungu juu ya mabaya au mema atakayotenda mtu hayahusiani na Mungu kujua hiyo mabaya na mema ya mtu.

Nasubiri uulize swali hili:- kwanini Mungu aumbe mtu anayejua kuwa atakuwa muovu???😁😁😁
NADHANIA ATAKUWA ANATANGAZA U-ATHEIST HUYO KAMA LAKINI SINA UHAKIKA ETI!
 
Ahahahahaaaahahhahhaaha braza mbona unalalamika badala ya kujibu ulichoulizwa

1. Inawezekana vip Mungu ajue idadi ya magoli halafu asijue atafunga nani hayo magoli ? huyu Mungu kama Yupo aje huko TUBET nae , maana anabahatisha kama sisi huku mtaani, hata sisi tunampa ushindi livarpool lakini wafungaji hatuwajui mpaka mpira uishe , kama huyo Mungu wako ahahahahaaaahaaaaaaha

2.Mungu anajua wazi firauni anakwenda motoni kabla ajamuumba, halafu ashindwe kujua kipi kitampeleka motoni?
Huyo Mungu unae mzungumzia atakuwa ana BET kama wabashiri wengine , umekalia cause and effect , ujinga mtupu, yaani Mungu ajue wewe utakwenda motoni halafu sababu asiijue huyo atakua sheikh yahaya sio Mungu ahahahhha ahaahhhhhahaha komaa hapa acha kulialia
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom