Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Sasa Mungu akimuadhibu kiumbe wake aliyemuumba mwenyewe kosa lipo wapi??, si kamuimba yeye mwenyewe na anajua mapungufu yake!!.

Vipi we dogo!!
Na ndiyo maana Mungu alipotaka kuichoma sodoma na gomora alimwacha LUTU kwasababu ya rafiki yake Ibrahim, na Ibrahim alimwambia Mungu waweza angamiza watu wote ikiwa kuna 1 mwenye haki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo usipotoa sadaka au hizo zaka kanisa litaendeshwa vipi?
Mchungaji na familia yake wataishi vipi? Kumbuka ile ndo kazi yake.
Mtumishi wa Mungu riziki yake hupatikana madhabauni na si vinginevyo.
Labda useme hawa manabii uchwara ndo wanazingua harakati za kanisa la Yesu coz wana warubuni nakuwahadaa waumini wao kwa tamaa ya pesa
Watumishi wa Mungu wapo pia hata makanjanja wapo, ila yote hayo Mungu ndiye anaye wajua, hata kipindi Yesu anahubiri walikuwepo watumishi kama mafarisayo na aliwambia mnawatwisha watu mizigo mizito ukiwa nyie hambebi, hapo hapo mtu kama Kornelio aliambiwa Sala zako sadaka zakozimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu, kwa faida ya wabishi Matendo 10:1-4 na ili kuelewa wasome sura yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza sadaka inapaswa kuwa siri!
Lakini Siku hizi utasikia Mwenye shilingi kadhaa anyooshe mkono Juu n.k
Mara walotoa nyingi wapite mbele waombewe madhabahuni !
Kuna mambo huko mmh?!
Wakati saingine Yule alotoa kidogo Kama katoa kwa moyo wa imani ndo atakaepewa thawabu!
 
Ila yote tisa kumi binafsi naona bado kuna umuhimu mkubwa wa kumtolea Mungu sadaka kwa moyo wa Imani na Upendo !
Haijalishi kitu chochote!
 
Ila ktk mambo yote tunapaswa kuwa na tunda la kiasi!
Siyo utoe hela yote halafu ukose ada ya Shule ya watoto kwa mfano!
Imeandikwa " mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, kwa roho yako yote na kwa AKILI yako yote!
Mungu hapendi ujinga na upumbavu!
 
Habari wakuu!

Mungu wa kweli, mwenye uweza wote, na aliyeumba kila kitu hahitaji mambo yafuatayo:-

1. Hahitaji Zaka wala Sadaka
Mungu wa kweli si mhitaji, uhitaji ni karba ya viumbe. Mungu hana anachohitaji kutoka kwa kiumbe. Yeye ndiye huamua nini kiwe na nini kisiwe. Mungu wa kweli hahitaji sadaka kama watu wengi wanavyoaminishwa. Hahitaji zaka kama wachungaji wanavyosema. Wachungaji wanamsingizia Mungu mambo mengi ikiwemo hili la zaka na sadaka. Wanachoshindwa kusema ni kuwa wao ndio wanahitaji hizo zaka na sadaka kama sehemu ya huduma yao. Ni uongo na dhambi kubwa kusema Mungu anataka sadaka na zaka jambo ambalo linamdhalilisha Mungu muweza wa yote.

Wachungaji, mashehe na viongozi wote wa dini kwa majina yao. Muache kuhadaa watu na kumdhalilisha Mungu. Tutatoa sadaka na zaka kwa kujua kuwa mnatupa huduma za kiroho na si kusema kuwa Mungu anahitaji sadaka na zaka tena fungu la kumi. Kama tunawalipa waalimu, madaktari, wanasheria na kada zingine iweje tusiwalipe nyie. Kwa nini mumsingizie Mungu mambo ya uongo. Eti fungu la kumi ni la Mungu. Si kweli. Mtu atatoa zaka na sadaka kulingana na umuhimu wa huduma anayoipata na si kumtishia vitisho vya uongo.

2. Kafara si ondoleo la dhambi
Watu wameaminishwa kuwa eti ili mtu asamehewe dhambi basi sharti amwage damu. Zamani walimwaga damu ya wanyama lakini sasa hivi wanaamini kuwa Yesu(mtu ninayemheshimu sana) alikufa kwa ajili ya watu jambo ambalo ni uongo. Mungu wa kweli hawezi kufikiri achilia mbali kutenda jambo kama hilo. Hiyo ni mila za kuabudu miungu ya Kiyahudi ambayo msingi wake mkuu umetokana na Abrahamu aliyechukua baadhi ya mila za Kiashuru( kwa sasa ni Syria). Miungu ya Abrahamu ndiyo ilimtaka amtoe Isaka kafara kama ilivyodesturi.

Mungu wa kweli hahitaji mchakato huo kusamehe dhambi, na kumwaga damu si suluhu ya dhambi kuishi. Kwa kutambua hili jambo hili moja kwa moja linaonekana ni wazo la kibinadamu zaidi kuliko la Mungu.

3. Maombi hayabadili chochote kwa Mungu mwenye uweza.
Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengine kwa majina yao wanawadanganya watu kuwa ukimuomba Mungu jambo lolote anaweza akakupa kitu ambacho si kweli hata kidogo. Vile Mungu alivyopanga kabla hajakuumba ndivyo itakavyokuwa. Kusema kuwa ukimuomba Mungu anabadili mipango yake ni kujidanganya na kupoteza muda. Kumuomba Mungu ni kumfundisha namna ya kufanya mambo yake. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa mtu akiomba jambo kwa Mungu hupewa isipokuwa ushahidi uliowazi ni kuwa Mtu akifuata maagizo ya Mungu na sheria zake ndio hupata akitakacho. Mungu anataka watu wafuate sheria zake na si kuomba omba tuu.

Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini jukumu lao ni kuwafundisha watu sheria za Mungu na si kuwadanganya waombe au kuwaombea. Kuwaombea watu ni kuwafundisha uvivu. Na kuamini katika hamna.

Ukitaka uamini nikisemacho, kaa ndani omba alafu usiende kufanya kazi uone kama Mungu atakupa ukitakacho, alafu mwenzako asiombe aende kufanya kazi uone nani atapewa/atapata. Hakuna sheria ya Mungu mahali popote kwenye torati inayomtaka mtu aombe. Tafsiri yake nadhani mnaelewa ni nini. Usishangae kwa nini bara la Afrika ni masikini ilhali ndilo linaloongoza kwa waumini wenye kuomba makanisani na misikitini. Jibu unalo.

4. Wachungaji/mashehe na viongozi wa dini si watu pekee wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kuna dhana watu huaminishwa kuwa kundi fulani la watu ndilo linalotakiwa kupewa heshima kuliko kundi jingine. Huu ni uongo mkubwa. Mchungaji ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine. Anahudumia watu kama wanavyohudumia wengine. Hana uspesho wowote zaidi ya wao kuwahadaa watu wenye akili ndogo na wasioujua ukweli ndio maana wamegeuka watumwa wa makuhani na mashehe. Kila mtu duniani anahitaji heshima ikiwa anafanya kazi ya kuhudumia wengine. Iwe ni fundi nguo, fundi magari, mbunge, mwalimu, muuguzi, mhandisi wote wapo sawa na wote wanategemeana. Kumpa mtu fulani heshima kuliko mwingine si tu kwamba ni ukosefu wa maarifa bali ni kuonyesha hali ya kutoujua ukweli.'

Viongozi wa dini wamejipa hadhi kubwa na kujiona wao ndio wenye mamlaka. Usishangae kiongozi wa dini mjinga akisema kuwa anakulaani kwa Mungu. Nikisiaga hivi huwa nacheka sana. Mtu hupata laana kwa kuacha sheria za Mungu na si maneno ya Mchungaji au mzazi. Kwa ujumla ni kuwa mtu hujilaani yeye mwenyewe ikiwa ataacha sheria za Mungu.

Hivyo watu wamejikuta wakiwaogopa wanadamu wenzao kwa kutoujua ukweli. Unamuogopa mtu aliyezaliwa na mwanamke? Mtu anayehitaji chakula ili apate nguvu ya kuishi. Unakuta mtu anaenda kanisani anaitwa na mchungaji mbele ya kanisa na kutabiriwa vitu vya uongo na yeye anasema kweli wakati sio kweli. Kwa mfano;
Mchungaji: wewe unatatizo la ugumba
muumini: Kweli
Mchungaji: Mama yako anakuloga
Muumini: Kweli
wakati yote ni uongo, anasema kweli kwa uoga na utumwa wa kifikra.

Wito wangu, lazima watu waishi kwa kupendana na kuzishika amri na sheria za Mungu ili wapate kuwa huru na maisha. Vinginevyo tutabaki kuwa watumwa na kuona sisi ni wasindikizaji wakati wengine ndio walioumbiwa huu ulimwengu jambo ambalo si kweli
Joka mada za imani bado huziwezi. Hapo juu inajichanganya sana unawaasa watu juu ya Mungu wa kweli ambaye yote uliyoyakataa anayahitaji. Inatakiwa usiwevuguvugu no iwe no na yes iwe yes.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Halafu Kwani kumtolea Mungu sadaka lazima ukatoe kanisani?
Mtu akijiwekea utaratibu wa kusaidia wajane na yatima kwa mfano au wagonjwa mahospitalini Je si ni Sawa pia?
Ila inapaswa kufanyika kwa uaminifu wote pasipo Mtu kujidanganya mwenyewe nafsi Yake!
 
Mungu akambarikia mwanadamu, nendeni mkatawale wanyama wa mwitu,
ndege wa angani na samaki wa baharini, acha tule mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app


Ni sahihi, neno "kutawala" lina maana maana pana sana na ndiyo maana tunakula nyama ya swala na hapohapo hatuli nyama ya mbwa au simba ingawa wote tunawatawala.

Watu tumekatazwa kula nguruwe kwa sababu nguruwe anasababisha watu wawe (MASHOGA), utafiti unaonyesha kwamba Mashoga walianza kula nyama ya nguruwe kwa wingi (staple food) toka walipokuwa wadogo hadi ukubwani.

Tule vyakula kwa kutafakari ili tusijekula vyakula vinavyoweza kutuingiza katika kutenda dhambi.
 
Ni sahihi, neno "kutawala" lina maana maana pana sana na ndiyo maana tunakula nyama ya swala na hapohapo hatuli nyama ya mbwa au simba ingawa wote tunawatawala.

Watu tumekatazwa kula nguruwe kwa sababu nguruwe anasababisha watu wawe (MASHOGA), utafiti unaonyesha kwamba Mashoga walianza kula nyama ya nguruwe kwa wingi (staple food) toka walipokuwa wadogo hadi ukubwani.

Tule vyakula kwa kutafakari ili tusijekula vyakula vinavyoweza kutuingiza katika kutenda dhambi.

 
Ni sahihi, neno "kutawala" lina maana maana pana sana na ndiyo maana tunakula nyama ya swala na hapohapo hatuli nyama ya mbwa au simba ingawa wote tunawatawala.

Watu tumekatazwa kula nguruwe kwa sababu nguruwe anasababisha watu wawe (MASHOGA), utafiti unaonyesha kwamba Mashoga walianza kula nyama ya nguruwe kwa wingi (staple food) toka walipokuwa wadogo hadi ukubwani.

Tule vyakula kwa kutafakari ili tusijekula vyakula vinavyoweza kutuingiza katika kutenda dhambi.
Acha kudanganya watu , hao hao wanaosema hawali nguruwe ndiyo wanaongoja kwa huo usodoma, tunajua sana tatizo huwa tuna staha ya maneno, nakukaribisha nina ninafuga hao nguruwe nitafutiage wateja mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma Matendo ya mitume 10 labda uwe ni wale wanyofoa vifungu vinavyokufunga mwenyewe
 
Back
Top Bottom