Mungu nisaidie bado nina ndoto za kumuoa Butogwa Shija

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,895
25,944
Aman iwe juu yenu wakuu wa jukwaa hili

Kama kichwa cha cha habari kinavyosomeka hapo juu

Nishawahi kuleta uzi hapa nikielezea kwa masikitiko makubwa sana ni kwa namna gani namzimikia butogwa, watu waliniponda sana na kudai kuwa nimepotea njia kwa kuwa demu ana sura ya baba yake ni mbaya sijui hana shep

Niliwashangaa sana walionibeza maana wao wanazani kila aliye mbaya kwao basi pia atakuwa mubaya kwa wengine,

Mimi kwangu butogwa ni wife material ni mwanamke aliye kamilika kuanzia sura, umbo urefu hadi akili

Kuna watu watasema kuwa yule dada ni msomi hivyo sitaweza lakin mimi nitawacheka kisukuma hiiiiiiii afu nitarudi kwenye mandiko ya kitabu kimoja kitakatifu cha bible ambacho kimesema ishini na wanawake kwa akili tu, kwa msitari huo wa biblia inamanisha kuwa mwanamke akikuzid urefu siyo mbaya pia mwanamke akikuzidi rangi siyo mbaya pia mwanamke akikuzidi kipato siyo mbaya ila kibaya tu asikuzidi akili na pia kibaya zaid ni kuwa malio hicho ndo kibaya


Mimi bado sijachoka kukupenda wewe butogwa shija mimi nakupenda sana tena upendo kutoka moyoni kabisa

Nakuhitaji sana wewe dada

Ni bora nipigwe mawe lakin si kukosa upendo wako

Ni ukweli usio na shaka ya kwamba mimi hunijui wala hujawahi kuniona lakin mimi nakupenda sana, naomba ujue hilo na kama itakupendeza bas unijue pia


Butogwa wewe ndo mwanamke ambaye niko tiar nikose chakula lakini siyo kukukosa wewe, ndo maana ninamuomba Mungu mwenyezi afanikishe katika hili

Mimi ni kijana mwenzako wa kisukuma

Nakuzimikia sana butogwa

Kwa wasiojua maana ya butogwa, BUTOGWA ni jina la kisukuma likiwa na maana ya UPENDO AU PENDO


Naomba dunia nzima inisaidie kufukikisha ujumbe huu kwa mhusika naomba hata media au blog zinisaidie sana

Naomba dunia nzima ijue kuwa nampenda huyu dada


Asanteni sana

Nawasilisha



Screenshot_2019-08-30-20-21-01.jpeg
Screenshot_2019-08-30-20-20-04.jpeg
Screenshot_2019-08-30-20-21-12.jpeg
 
Back
Top Bottom