Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
14,185
8,559
Ndugu zangu Uongozi unatoka Kwa Mwenyezi Mungu anayetufahamu sisi Tungali katika Matumbo ya Mama zetu, Yeye Ndiye Anayejuwa hatima yetu, yeye ndiye mtoa Riziki, Neema na Baraka, yeye ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote hapa chini ya jua. Ndiye mtoa Maarifa na Njia kwa wale wamchao na kufuata njia zake.

Rais Samia yupo hapo ,Amefika hapo kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimuandikia kufika hapo. Mama Samia Hajafika hapo kwa uweza wa Mwanadamu, hajafika hapo kwa ujanja wake, kwa Akili zake, kwa Dini yake,kwa kabila lake, kwa jinsia yake, kwa nguvu zake, kwa mipango ya kiuanadamu, kwa Fedha zake, kwa ukarimu wake, upole wake, ucheshi wake, sura yake, Mwendo wake, Sauti yake, Umbo lake, kimo chake, Maono yake, mikakati na mbinu zake, familia yake na Elimu yake.

Mama Samia Amefika Hapo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa mipango ya Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa kuwa ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu alimwandikia hivyo, Kwa kuwa ndivyo Mwenyezi Mungu alipanga iwe Hivyo, Ndivyo Ambavyo alitaka agano litimie katika ulimwengu wa kiroho wa uumbaji wa Mama Samia Tangia Akiwa Tumboni mwa mama yake

Mbele za Mwenyezi Mungu kila Jambo na wakati wake na majira yake, huu ulikuwa Ni wakati wa Mama Samia, Haya Ni majira ambayo MWENYEZI MUNGU alipanga iwe Hivyo kwa Rais Samia kuinuliwa kiuongozi kuongoza nchi yetu, siyo sisi wanadamu, siyo sisi tuliyo waamuzi. Ni Mungu Ndiye Aliyempaka Rais Samia Mafuta ya Uongozi, Ni Mungu Ndiye aliyempa kibali Cha kufika Hapo. Ni Mungu Ndiye aliyemcholea Ramani yake na njia yake kufika hapo, Ni Mungu Ndiye aliyemshika mkono kumfikisha hapo, Ni Mungu Ndiye Aliyemvusha katika mabonde na milima, katika majaribu na mitihani, ni Mungu Ndiye aliye mpitisha njia ambayo wengine hawakupitishwa, Ni Mungu Ndiye aliyemlinda na kumpigania kufika hapo.

kwote alikopita na kufanya na watu kazi ilikuwa ni mipango ya Mungu katika Kumwandaa na kumfundisha namna ya kuishi na watu wa aina zote, hao watu na hayo maeneo ya kikazi ilikuwa Ni madaraja tu ya kumvusha, lakini Mipango ya Mungu ilikuwa ni kumuinua Hadi hapa Alipo kwa Sasa nafasi ya mwisho kiuongozi na kicheo. Hivyo Hakuna wakumshushaa Mama Huyu Mzalendo wa kweli.

Sasa wewe Mwanadamu Ni Nani mbele za Mwenyezi Mungu? Ni Nani aliyewahi kuongoza kwa akili zake akafanikiwa? Ni Nani awezaye kushindana na Mwenyezi Mungu? Ni Nani kwa Fedha zake Amewahi kununua Urais wa nchi hii? Ni Nani kwa kusuka makundi ya kumshambulia na kumhujumu Rais wake amewahi kufanikiwa kupata Urais wa nchi hii? Ni Nani huyo? Yupo wapi? Wangapi walikuwa na mapesa na marafiki wenye mapesa waliojaribu kununua Urais lakini hawajawahi kufanikiwa? Wangapi wamewahi kuutamani Urais lakini bado wanausikia kwenye Redio? Nani alitegemea Odinga atafika Hadi Leo hii bila kuapishwa kuwa Rais ? Vipi Hillary Clinton? Nani alitegemea mfungwa Nelson Mandela atakuja kupata heshima ya ulimwengu?

Ndugu zangu Amini Amini Nawaambieni kuwa Kama Haikupangwa Na Mwenyezi Mungu Wewe uwe kiongozi Au Rais Basi Tambua kuwa Hata Ufanyeje utaishia kusononeka tu Moyoni Mwako pale utakapoona miaka inayoyoma huku hakuna Dalili za wewe kutimiza Ndoto Zako.

Rais Samia huwezi Ukamchafua na kumpaka matope kwa watanzania na ukafanikiwa,kwa sababu watanzania tunamkubali Sana Rais Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kulitumikia Taifa hili, Amekuwa mkweli na muwazi Sana katika kuongoza Taifa letu, kwa kila changamoto tuipitiayo amekuwa mkweli kueleza mikakati ya kukabiliana nayo

Rai Yangu kwa Wana CCM wenzangu na Wazalendo Wa Taifa Hili Tusikubali kuchonganishwa na wenye maslahi Binafsi,Tusikubali watugawe Wala kutupandikiza mbegu za chuki, Marais wote Watano waliopita na kumtangulia Rais wetu mpendwa na kipenzi cha watanzania mama shupavu.

Rais Samia walikuwaa Ni wanaccm na waliotekeleza ilani ya ccm, Hivyo asitokee mtu wakutuletea mbegu za wale na sisi. CCM Ni moja ,Wana CCM Ni wamoja Na Chama Ni kimoja chini ya mama yetu jasiri, Hodari, shupavu, mchapa kazi, mcha Mungu, Mzalendo Na mwenye Dhamira ya Dhati na Taifa hili Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
 
Na kamwe haitatokea hata wajiandikishe vi threads uchwa asubuhi Hadi jioni 24 hrs haitakuja kuwa Kama vile Lowassa na Raila walivyoshindwa.

Samia amekuwa akiongea Mara nyingi sana kwenye ziara zake kwamba kila.mtu yupo alipo kwa sababu kwa wakati huo Mungu amependa iwe hivyo na so wawajibike kwa Mujibu wa inavyotakiwa,full stop..

So makelele ya kijinga na kipuuzi Ni kupoteza mda wao bure..👇

2973195_FB_IMG_16332143456548674.jpg
 
Ndugu zangu Uongozi unatoka Kwa Mwenyezi Mungu anayetufahamu sisi Tungali katika Matumbo ya Mama zetu, Yeye Ndiye Anayejuwa hatima yetu, yeye ndiye mtoa Riziki,Neema na Baraka, yeye ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote hapa chini ya jua. Ndiye mtoa Maarifa na Njia kwa wale wamchao na kufuata njia zake.
Hata Hitler na holocust yake yawezekana walisema hivo. Tunakwepa kuwa responsible kwa kumsingizia Mungu na shetani.
 
Hata Hitler na holocust yake yawezekana walisema hivo.
Tunakwepa kuwa responsible kwa kumsingizia Mungu na shetani.
Ndio hivyo Mungu alitaka wajerumani wapitie hayo ila haiondoi Wala kufuta historia yake Kama ambavyo Historia ya Jiwe haitafutika maana mlisema JK Ni dhaifu akawaonyesha Moto ili mjifunze.
 
Rais Samia Ni kiongozi Mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu Ndio sababu unaona namna anavyoungwa mkono na mamillion ya watanzania,huyo Hitler Nadhani unafahamu hatima yake kule ujerumani na historia yake katika Taifa lake mpaka leo
Kwani Hitler hao mamilioni ya watu aliwaua peke yake!? Si aliungwa mkono na watu pia. Anyway hayo ni mawazo yako.
 
Sisi tunataka maji na umeme full stop mambo ya mungu kampa nani urais sisi hayatuhusu leo misri kesho china mara usa tunataka maji tanzanite na dhahabu zetu zinazopelekwa india kila saa.
Maji yapo kila sehemu Ila sema kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka ndio imeleta changamoto ya kutotosheleza Mahitaji ya watu wote, kwa kutambua Hilo serikali imeongeza bajeti yake ili kutekeleza miradi ya maji maeneo mengi ya nchi yetu, hapa majuzi wewe Ni shahidi umeona Rais wetu akizindua mitambo mikubwa ya kuchimba visima virefu vya maji vitakavyo saidia katika kumaliza tatizo la maji.
 
Ukiutazama Urais kama fursa basi utakuwa na mawazo kama ya mleta mada.

Ila Urais ni nafasi ya juu kabisa ya utumishi wa umma na kwa kitambua tu majukumu yake sidhani kama swala la wivu lingetajwa hapa.
 
Oky!!! Ngoja tusubiri hatima yake
Hatima yake Rais wetu mpendwa Ni njema Sana na kila mtanzania anamuombea heri Rais wetu katika kutimiza majukumu yake, Ni Rais muungwana,mcha Mungu,Mzalendo, Mkweli na mwenye Dhamira njema na Taifa hili aliyedhamilia kuinua maisha ya watanzania kiuchumi na ndio maana anaendelea kuungwa mkono na watanzania
 
Hatima yake Rais wetu mpendwa Ni njema Sana na kila mtanzania anamuombea heri Rais wetu katika kutimiza majukumu yake, Ni Rais muungwana,mcha Mungu,Mzalendo, Mkweli na mwenye Dhamira njema na Taifa hili aliyedhamilia kuinua maisha ya watanzania kiuchumi na ndio maana anaendelea kuungwa mkono na watanzania
Nikweli kabisa ndio maana unahitaji uprove kila siku kwa kuanzisha thread zake.
Future is uncertainty
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom