Mungu ndani ya katiba ya watanzania hongera judge samata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu ndani ya katiba ya watanzania hongera judge samata

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by DSN, Apr 2, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  MUNGU NDANI YA KATIBA YA WATANZANIA HONGERA JUDGE SAMATA

  My hope sasa Mungu anajibu kupitia wazee wachache wenye BUSARA, kama Judge Samata.Nilikua napata shida sana ni jinsi gani MUNGU tusivyomshirikisha kwenye nchi yetu.

  Eti serikali yetu aina dini,ukweli uwa nikisikia kauri hii inaniumiza sana sana sana sanaaaaaaaaaa.Sawa yaweza kua iliwekwa kwa ajili ya kuvuka hatua fulani na si forever kwa hilo sina utata nalo.

  Hivyo kwa ujio wa katiba mpya ni wakati sasa wa kuandika maneno kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watu wake wanaamini katika MUUMBA.

  Aijarishi muslim or Christian kila mmoja wao anaamini katika muumba.Hivyo kwa kutaja hivyo dhamira ya kushitakiwa na nafsi kwa wale wote wanaopata viapo kupitia katiba watafungwa kiroho na dhamira pindi wanapokiuka katiba kwa kuwatend wananchi na nchi ndivyo sivyo kwa matendo yasiyo na UTU. Kumcha mungu ni chanzo cha maarifa.

  Hakika Mungu anasikia, pole zangu kwa wale wote wasiotaka kusikia maono ya watu kama Judge Samata. Gharama yao kwa kuyapuuza maono hayo itakua kubwa kwao wao na vizazi vyao waanze mapema kwa kusikiliza kilio cha katiba mpya kama Kongamano lilivyoongea.

  Deus Spes Nostra.


   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna imani nyingi, wengine mungu wao binadam, wengine mungu mti, wengine jua, wengine ng'ombe, wengine haonekani. Kwenye katiba atawekwa mungu au miungu?
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kama serikali kuu za dunia zinaamini katika Mungu, yakwetu ina upekee gani isiamini!, lakini tukijidhadititi na kuwapinga wachochezi wote, huku tukiamini katika Mungu Amani yetu itadumu!
  Tuseme hapana kwa hawa wadini wanaotamani Tanzania iwe kama Rwanda na Burundi kisa udini uliopitiliza! Mashekhe kuweni wenye busara na fikirieni mnayoyahamasisha mwisho wake utakuwaje.
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa upeo wangu kiimani najua Tanzania kuna Madhehebu mengi ila mungu ni Mmoja. Sijui ww majimshindo.Hatutaji madhehebu kwenye KATIBA bali tuanataja jina la MUUMBA.
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,632
  Trophy Points: 280
  Jamani wengine tulikatiwa umeme,kwani samatta kasemaje?dadavua mkubwa.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Yupi huyo muumba wenguine hawaamini muumba. Mimi namuamini Allah.
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Yupi huyo muumba? wengine hawaamini muumba.

  Mimi namuamini Allah.
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi bado naamini ni busara kusema SERIKALI HAINA DINI ILA WATU WAKE WANA DINI. Ukienda kinyume na msimamo huo, utakaribisha balaa.
   
 9. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hata usa wanaamin mungu yupo....kama unabisha tafuta us$...u w'l find the following words..in God we trust. Usiniulize mungu yupi..Coz mungu ni mmoja ila majina tofauti.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gosbert, hilo linabaki kama lilivyo ila kinachopendekezwa ni kumtanguliza Mungu. Hili limekuwa likifanyika lakini bila utambuzi rasmi wa uwepo wa Mungu. Mfano, angalia Bunge letu linapoanza dua inasomwa. Viapo watu wanashika Biblia au Quran. Hivyo ni busara hilo likafanyika na Mungu akatangulizwa kwa kutajwa kwenye sheria mama.
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nilipomsikiliza Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta akileta hoja hii nilikuwa na mixed feelings:

  Kubwa zaidi ni kwamba kwa miaka mingi Tanzania tumezoeshwa kusikia kuwa Serikali haina dini ( secular state) na dhana hii haijawhi kuchambuliwa watu wakaelewa maana yake ni nini.Je, katika hali tuliyo nayo sasa, ambapo kuna chembechembe za udini katika kila neno linalotamkwa au kitu kinachofanywa, itatafsiriwa vipi pale Katiba itakapoingiza "MUNGU" ?

  Tanzania tuna matatizo makubwa sana na tunahitaji divine intervention kujinasua.Lakini kama tutamuingiza Mungu kwenye Katiba basi hatuna budi tuheshimu na kuheshimiana katika imani zetu za kidini. Isije ikatokea wale wenye kufanya vurugu za kidini wakajifanya wanatumia "haki yao ya kikatiba' kufanya au kudai wanayoyadai.

  Watanzania tujihadhari sana na kila hatua tunayochukua hata kama ni kwa nia njema.
   
 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Kinachonishangaza ni kuwa; watu huwa wanakuwa washauri wazuri saana wakiwa pembeni. Ila wao wakiwa ndio wenye madaraka, hawapendi kusikia mabadiliko. Huyu Samatta alikuwa na nafasi kubwa saana na haya anayozungumza si mapya katika utendaji wa serikali na watu wake, mbona hakuwahi kusema? Huyo Mungu anayetaka aingie kwenye katiba ni yupi? Na kina nani watakubaliana naye? Divine intervention, how na mipaka yake ipi? Au kiongozi wa dini ndio awe Rais maana hiyo ndio purely divine intervention. Au kuwaongezea mamlaka viongozi wa dini? In either way hajawa wazi. Madhambi na mlolongo wa udini si mpya! Madai ya katiba si mapya!
   
 13. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Majimshindo tafuta kamusi ya kiswahili TUKI,Neno MUUMBA kwa Lugha ya Kiingereza manake CREATOR or GOD.Kwa ufahamu wangu mdogo chini ya uso wa dunia hii kuhusiana na matumizi ya neno ALLAH ,nikizingatia mazingira ya maisha yangu na wanajamii walionizunguka wakiwemo ndugu zangu wa kidamu wanaotumia neno ALLAH kiimani tafsiri yao uamanisha MUNGU au MUUMBA.

  Tafsiri ya kamusi ya Kiswahili Kingereza neno ALLAH linamanisha [Waislamu] GOD.Na Tafsiri ya Neno GOD kwa Kiswahili maana yake MUNGU,MOLA, ALLAH or MUUMBA.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nadhani tatizo siyo kuwa nje na kutoa ushauri au kuwa ndani na kushindwa kufanya kitu.
  Utakumbuka hata yeye amechambua vizuri mno kuonyesha tatizo liko wapi - limo ndani ya mfumo.Alitoa mfano wa namna mwananchi alivyopeleka swala la kikatiba mahakamani, mahakama ( Jaji Lugakingira) akatoa tuzo iliyoonyesha mwananchi kashinda lakini Bunge haraka sana likatunga sheria iliyoweza kuifutilia mbali hukumu na haki iliyotolewa na mahakama. Kimsingi kama mfumo ni mbaya hata uwe na ujasiri vipi kuleta mabadiliko, hayo mabadiliko hayatatokea,
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa thread yako mkuu,lakini nimeona mapungufu yafuatayo kwenye hiyo thread yako

  1. Wewe ni mtu unayeamini katika Mungu,na kwahiyo fikra zako zimefunikwa usione kuwa kuna watu wengine hata huyo Mungu hawamjui na hawaamini wameumbwa na Mungu.
  2. Hata kama tu-assume kuwa Watanzania wote wana dini zao yaani Ukristo na uislamu kama dini kubwa sidhani kama ni jambo la busara kuweka mambo ya dini katika katiba....Ni hatari kwa future ya taifa letu.
  3. Sioni tatizo kwa status ya sasa ya serikali as long inatoa uhuru kwa kila mwananchi kuamini katika imani yake ili mradi havunji sheria...
  Fikiria upya.....
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  only83 hata huyo asiyemwamini Mungu anajua kua kuna super nature.Pia katika katiba hatutaji madhehebu mkuu ila tunataja jina la mungu.Mzee Samata kasema wakenya wamemtaja mungu mara mbili kwenye katiba yao mpya.Hoja hapa si kuingiza vifungu vya biblia ama quran ndani ya katiba mpya,bali ni kutambua nchi hii kabla ya yote inatambua uwezo wa Mungu, Muumba, Mola taja majina yote........................,

  Hofu nini wakati kiapo cha utumishi wa umma au popote penye kuitaji kiapo mwisho wa kiapo mpiga kiapo usema "MUNGU NISAIDIE".Akimaanisha kutambua uwezo wa Muumba kumsaidia atende yaliyo mema dhidi ya wenzi wake.
   
 17. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Kwahiyo kwa kuwa mfumo mbaya inamaana wale waliondani ya mfumo na kisha kujitambulisha kuwa wapambanaji wanadanganya? Lets be realistic kwenye hili, mahakama ina uwezo saana wa ushawishi kwenye nafasi yake. Msema kweli katu hatakubali kujidanganya na kutenda kinyume kwa kuwa yupo ndani ya mfumo. Otherwise ni mambo ya maslahi. Ukiachilia mbali hilo la kudai kuingiliwa na mihimili mingine, wao katika yale wenye nguvu nayo wamefanya nini?
   
Loading...