Mungu na Shetani wanawasiliana na binadamu kupitia utashi

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
Mungu na Shetani wapo katika Utashi wa kila binadamu mwenye akili timamu.

Binadamu ndiyo kiumbe pekee mwenye kubeba mipango na malengo ya aliye muumba,binadamu ni kiumbe ambacho kinatekeleza majukumu mhuhimu yaliyosababishwa kuumbwa kwake.

Uthamani wa binadamu umesababishwa na kupewa kiasi kidogo cha nguvu ya ya kiungu kiasi hicho kidogo cha nguvu hiyo ya kiungu ndiyo kinaitwa UTASHI.

Kutokana na nguvu ya utashi ndiyo maana binadamu ni kiumbe hatari zaidi ya viumbe vyote vyenye mwili wa nyama au mimea.

Fahamu kwamba kiwango cha utashi alicho nacho mwanadamu ni kidogo zaidi kuliko kiasi cha utashi cha viumbe visivyo na mwili.

Viumbe visivyo na mwili yaani roho zina utashi mkubwa kuliko binadamu ila ni dhaifu kuiathiri dunia sababu zimenywimwa mwili.


Binadamu mwenye akili timamu ndiye pekee anayekuwa na utashi,akili ya mwanadamu ndiyo huwezesha nguvu ya utashi kuwa timilifu.

Utashi ndiyo nguvu ya kiungu ambayo hujenga muhimili mkuu wa mawasiliano kati ya mwili wa mwanadamu na nguvu zisizo za kimwili (nguvu za kiroho).

Binadamu kwa biadamu pia wana uwezo wa kuwasiliana kwa njia hizi zisizo za kimwili kwa kufahamu au kuto kufahamu.

Wanao fahamu uwepo wa nguvu hizi hujifunza zaidi matumizi yake na huzitumia katika maisha yao ya kila siku.

Ambao hawafahamu uwepo wa nguvu hizi hawazitumii japo mara kwa mara nguvu hizi hutokea juu yao na huhisi ni maajabu au miujiza

MFANO: Unapojikuta unamuwaza mtu ambae una ukaribu nae (lazima uwe na ukaribu nae ) ghafla wakati unamuwaza mtu huyo anafika nyumbani kwako au anatokea hapo ulipo au anakupigia simu

Au Unakua unafanya kitu flani nje ya nyumba yako ghafla unaacha hicho kitu unachofanya na kuingia ndani bila sababu yoyote na hujui kwanini unaenda ndani lakini ukifika unakuta kuna tukio flani ni kama uliliona ukiwa nje ndo maana ukaingia ndani mfano unaweza kukuta simu inaita mara nyingi inakua haitoi sauti au kama una mtoto mdogo anakua alikua anataka kutokewa na jambo la hatari mafano kusogelea jiko,au unamkuta anachezea kitu cha hatari.

Nguvu hizi ni nguvu za kiungu ambazo hubebwa katika utashi,ili uweze kufikia nguvu hizi na ziweze kufanya kazi bila kubahatisha inatakiwa uwe na maamuzi dhidi ya akili yako.

WANAO FIKIA HATUA HII BILA KUJIJUA

Binadamu huweza kufikia atua hii akiwa hajitambui (out of mind ) ni mara kadhaa binadamu huwa nje ya ufamu wao,jambo hili huweza kutokea ghafla wakati wowote akiwa hajalala.(yupo macho)

Hali hii humtokea binadamu wakati umezama katika wazo flani la aina moja wazi lisilo tumia akili bali hisia zaidi,hapa mtu huyu anaweza kwa sekunde kadhaa akasahau kuhusu yeye mwenyewe,nguo uliyo vaa,madeni,pesa,mtu wa pembeni yake, n.k

Aifikia hali hii huweza kuwasiliana na roho ya mtu wa karibu yake,Nguvu hii ikiwa kubwa sana husababisha mwenye ile roho yake akapata hisia za huyu ambaye anawasiliana na roho yake hivyo anaweza akafany tendo la harisi mfano kumpigia simu yule yule aliyekuwa anaongea na roho yake.

Na yule aliyekuwa anaongea na roho ya huyu aliyepiga simu utasikia akipokea atasema "yaani nilikua nkuwaza sasa hivi"

WANAO FIKIA HATUA HII KWA KUJIJUA

Wenye uwezo tu wa kuitawala akili yao ndiyo huweza kufikia hatua hii kwa kuamua.

Ukiweza kuitawala akili yako na ukatambua akili ni kitu cha kawaida sana hata kuku anayo akili basi hapo ndiyo utaweza kufikia kiwango cha juu cha utashi na ili ufike katika kiwango hicho cha juu itakulazimu uikane akili na uikumbatie imani yako yoyote iwe uislamu au ukristu au imani yoyote itakayo kufanya utumie utashi kutekeleza jambo flani.

Utashi huweza kuanzisha nguvu ya mawasiliano na nguvu za juu za kiroho na hapo ndiyo utaweza kuwasiliana na nguvu hizo ila kumbuka utashi una pande mbili Upande wa mema na Upande wa mabaya,itategemeana wewe utashi wako unauongoza katika lipi unacho kiomba utapata liwe jema au baya.

Kumbuka kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho hubaki katika utashi akili huongozwa na utashi,utashi ndiyo huathiri akili na akili ndiyo huathiri mwili.

Mapato ya maombi hujidhihirisha katika mwili kupitia utashi kiasi cha ulivyo amini ndivyo kiasi ambacho akili itaatathi mwili.

Akili ina uwezo dhidi ya mwili athari za akili dhidi ya mwili itategemeana na namna akili ilivyoathirika na utashi.

Utashi hauongozwi na akili ila utashi unaongoza akili.Ili uwasiliane na Mungu au shetani ni lazima uikane akili na mwili na utumie utashi.

Ukiikana akili ambayo kila mnyama anayo utabakiwa na utashi ukifika hatua hii unakua umefikia kiwango cha juu cha kuathirika kiroho(imani) iwe katika jema au baya kutegemeana na lengo la utashi wako.

Ukiomba mema utashi wako utaathirika na mema (Mungu) ukiomba mabaya utashi wako utaathirika na mabaya (Shetani).

Baada ya kurudi katika akili yako ya kawaida akili hupokea taarifa za kiroho kutoka katika utashi na hufanyia kazi mara moja.

Kama uliomba kumchukia mtu flani utamchukia kwelikweli na kama uliomba kupona ugonjwa flani utapona kweli.

Fahamu kuwa akili inayoongozwa na utashi inaweza kuponya ama kuua ndiyo maana ni binadamu pekee ndiyo mwenye uwezo wa kujiua kwa kukusudia na mwenye uwezo wa kujipona kwa kukusudia.
 
Bado sijaelewa tofauti ya akili na utashi na kazi za kila mojawapo.. Naomba Ufafanuzi zaidi.
 
Bado sijaelewa tofauti ya akili na utashi na kazi za kila mojawapo.. Naomba Ufafanuzi zaidi.
Utashi no nguvu ya kiungu ambayo huiongoza akili ya mwanadamu mwenye akili timamu katika kutimiza anacho kitaka

Lakini pia utashi ndiyo unao kuwezesha kuikana akili na kutengeneza msingi mkuu wa mawasiliano kati yako na nguvu za kiroho (imani).

Akili ni uwezo wa kupambanuaa mambo na kuyatenda kwa mahitaji ya kuutunza mwili au kuulinda kila kiumbe kina akili ila binadamu ana akili zaidi.
 
Hivi kiumbe ni nini? Inakuaje kiwe kiumbe harafu hakionekani tena naomba kusaidiwa hapo.
 
Hivi kiumbe ni nini? Inakuaje kiwe kiumbe harafu hakionekani tena naomba kusaidiwa hapo.
Si kila kinachoumbwa kinonekana majini yameumbwa ni viumbe vilivyo katika roho na si mwili,malaika ni viumbe lakini havina miili
 
Ungeeleza basi namna mtu anavyotakiwa afanye ili aweze kumiliki wake (au kuingia katika hali ya kuweza kuwa na utashi unaozidi akili).
 
Ulichoeleza kinafanana na kile kinachofanywa na Budhist Monks? Maana wale wanaweza kuwasiliana kabisa hata wakiwa mbali na hata wakikanyaga moto hauwaguzi
 
Back
Top Bottom