Mungu na kiza nani mkubwa?

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,211
Watu wengi wanajua adui wa Mungu ni shetani lakini leo pia tutajua maadui wa Mungu.

Kiza si kiumbe, inaama hajaumbwa na Mungu amezuka kama alivyozuka Mungu. Historia haisemi kiza na Mungu nani mkubwa kiumri, nani alikuwepo kbla ya mwenzake, lakini tunaambiwa wamezidiana uwezo. Mungu kafanya uumbaji lakini kiza hajafanya uumbaji wowote. {mwanzo1:26, tumfanye mtu kwa mfano wetu ka sura yetu... Mungu hakuwa anaishi peke yake wakati anafanya uumbaji ndo maana anatumia neno "tufanye" ile neno tafsiri yake ni uwingi. Inamaana kiza na Mungu waliishi pamoja kabla ya dunia kuumbwa.

Tukisoma kitabu cha mwanzo tunaambiwa kabla ulimwengu kuumbwa kulikuwa kiza, kiza ndo alikuwa mtawala, Kila kitu palikuwa na giza. Mungu anaumba ulimwengu tayari palikuwa na giza. Lengo la Mungu ni kumuua kabisa kiza, lakini kutokana na nguvu za giza alizonazo kiza akuuliwa bali alifungiwa, na Mungu akaumba nuru. na athari za giza akaziita usiku na athari za nuru akaziita mchana.

Kutokana na maelezo hayo tunakubaliana kwamba Mungu ni mkuu kuliko kiza, Mungu ana nguvu kuliko kiza.
 
Duuu binadamu bwana umesha ambiwa mungu yupo juu ya yote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom