Mungu mkubwa: Nimeokota nyumba Mbweni

Kweli akili ni mali. Umetangaza mpaka ilipo nyumba. Aisee🤣🤣🤣.

Kuna mwenzako Arusha yeye aliingia kwenye gofu tu akaanza kukaa baada ya miaka kupita akaanza kuweka milango na mwishowe akapangisha upande wa juu, alikula pesa za wapangaji mpaka mwenye nyumba aliporudi na kukuta nyumba ipo na wapangaji ikabidi airenovate na kumwachia aendelee kuisimamia. Mpaka leo yupo hapo.
 
Dogo umekosea sana kuja hapa. Kwa herufi kubwa ”UMEKOSEA SANA KUJITANGAZA HAPA. IKIWEZEKANA FUTA HUU UZI FASTA.. Hiyo nyumba ni yako. Nakuambia futa huu uzi hivi watu hawachelewi kuunganisha dot. Kesho utakuta mtu amekuja na hati kabisa na wewe utajua kweli ni ndugu na yule,lakini kumbe wamechora racket tu

Kifupi nyumba na viwanja vya namna hiyo ni vingi sana mjini. Unakuta mwanamke anajenga nyumba kimya kimya bila mumewe wala ndugu yoyote kujua. Mara pap anafariki ghafla.

Kuna pagara nalimendea kimya kimya hapa tiwn liko kama hilo katikati ya nyumba,miaka 10 sasa hsliendelezwi. Nimewaweka vijana wanafyatua tofali pale mwaka wa pili sasa. Nimeweka kwanza kafence ka kutegesha tegesha napima upepo nani atajitokeza. Nakukuta kimya
 
Dogo umekosea sana kuja hapa. Kwa herufi kubwa ”UMEKOSEA SANA KUJITANGAZA HAPA. IKIWEZEKANA FUTA HUU UZI FASTA.. Hiyo nyumba ni yako. Nakuambia futa huu uzi hivi watu hawachelewi kuunganisha dot...
Tena asithubutu kujifanya muungwana kutafuta ndugu wa mwenyenyumba kama anavyoshauriwa humu na wenye wivu. Atulie kimya ajilie pango kama mwenyewe yupo atarudi
 
Maelezo yako ni tofauti na ya mleta mada
Huioni point yangu ilipokaa? Kuna watu wanajenga nyumba bila kumwambia mwanafamilia yeyote na Mungu anapowachukua ghafla tatizo linakuwa kubwa. Wengine hasa wanawake wanawajulisha mashoga zao na wanapopatwa na mauti ghafla mashoga wasio waaminifu wanajimilikisha majengo hayo bila kuwashirikisha wanafamilia.
 
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.

Mimi nimezaliwa mtwara,mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili,nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie dar kutafuta maisha...
Hata viwanja huwa tunaokota
 
Dogo umekosea sana kuja hapa. Kwa herufi kubwa ”UMEKOSEA SANA KUJITANGAZA HAPA. IKIWEZEKANA FUTA HUU UZI FASTA.. Hiyo nyumba ni yako. Nakuambia futa huu uzi hivi watu hawachelewi kuunganisha dot...
😁😁😁😁 Aisee mimi namendea kiwanja jirani tunapakana miaka zaidi ya 6 sasa hajitokezi mwenye kiwanja Wala hakuna anaemjua si viongozi wala nini..

Sasa nataka nisuke documents kwamba ni yangu afu najenga akija kujitokeza mtu ana vielelezo tutamalizana kisela ila sitoki
 
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.

Mimi nimezaliwa mtwara,mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili,nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie dar kutafuta maisha...
Kwanza kama ni kweli kaa kimya na ufute huu uzi.

Jifunze kuwa na kifua, utakuja kupoteza bahari zingine kwa sababu ya kupenda matangazo
 
Huioni point yangu ilipokaa? Kuna watu wanajenga nyumba bila kumwambia mwanafamilia yeyote na Mungu anapowachukua ghafla tatizo linakuwa kubwa. Wengine hasa wanawake wanawajulisha mashoga zao na wanapopatwa na mauti ghafla mashoga wasio waaminifu wanajimilikisha majengo hayo bila kuwashirikisha wanafamilia.
Nina wasi wasi na mleta mada.
Ila haya yanawezekana
 
Msichokijua ni kuwa muandishi kasema ni mbweni ili kuzuga tu lakini huenda ikawa hata ni kigamboni huko.chakushauri nenda fuatilia hiyo namba kama ni tigo makau makuu uwaeleze unataka kujua hii namba miaka kumi nyuma ilikuwa inawasiliana sana na namba zipi ??? Hao ndio watakuwa watu wake wa karibu la sivyo na ww umetulia unafurai dodo chini ya mpera.

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.

Mimi nimezaliwa mtwara,mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili,nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie dar kutafuta maisha.

Nikatafuta vibarua vya kupalilia mikorosho ili nipate nauli ya kwenda dar maana akili yangu haipo sawa nafikiria dar tu.ilikuwa nikiona vijana wenzangu wakija kijijini kutoka dar mambo yao safi,nguo nzuri wana fedha za kutosha.nikapiga mzigo nikapata 170,000/=

Mwaka 2010 nikanda gari pruuu mpaka dar,breki ya kwanza tandika sudani.nimeshukapa pale sina ramani nashangaa shangaaa sina pa kwenda.usiku ukaingia nikapata menu nikalala stand.

Siku ya pili nikakutana na jamaa mmoja katika kupiga story nikamwambia mm natoka mtwara kumbe na yy anatoka mtwara lakini mshikaji alikuwa anafanya biashara ya kuuza mayai.basi nikamwambia mm ndio nimeingia jana yake kutoka mtwara, akaniambia mjini kugumu nikwambia nataka nijumuike na yy tufanye biashara ya mayai akaniambia hakuna tatizo.mshikaji alikuwa anaishi mbagala mgeni nani.

Siku zikaenda vijihela vyangu vikaisha mtaji ukafa kwasababu ya mahitaji ya kujikimu kila siku.kutabalisha biashara tukauza nguo za mali kauli,tembezeza sana nguo kila sehemu dar lkn nikao nikazi ngumu wakati mwingine unaporwa nguo unaporwa hela.

2011 kuna jirani mmoja alikuwa ni fundi ujenzi akanishawishi niwe msaidizi wake ktk ujenzi nimwambia hamna shida.
Site ipo mbweni,basi wasaidizi walikuwa kama watano.nyumba ilikuwa ya ghorofa moja.nyota ilianza kuwaka baada bosi mwenyumba kuniambia niwe mlinzi wa malighafi za ujenzi,mshahara 100,000/= kwangu nilimshuru mungu sana,huku nalipwa kama kibarua na mwisho wa mwezi nadaka.

Yote kwa yote site ikaisha kila kitu boss akajenga kikota kidogo akaniambia nikae pale kama mlinzi na mshahara ukawa 150,000/=nikashukuru sana.mchana naenda kufanya daika waka nyingine usiku pakulala papo.

Mwisho wa mwezi ukifika boss anakuja na funguo za nyumba yote nafanya usafi na ananiletea mshahara wangu.
Mwezi wa kwanza alikuja kama kawaida,mwezi alikuja kama kawaida,mwezi watatu alikuja akaniachia funguo za vyumba vyote akaniambia nyumba anaipangisha kwahiyo nyumba iwe safi muda wote na nisitoke kwenda kokote ili akileta mteja apate kuikagua.

Basi nilikaa na funguo nisubiri boss alete wateja miezi minne ikapita kimya na mshahara wangu nilikuwa sijapata nikaamua kwenda hewani kumtafuta boss simu yake haipatikani. Miaka 10 imepita sijamuona boss na namba yake baada ya miaka ikawa amepewa mteja mwingine.

Mwaka jana niliamua kujilipua nikaamua kuipangisha ile nyumba 700,000/= kwa mwezi.mpangaji aliponiona nikamwambia mm ndio mwenyumba alikataa maana nipo kisela na nimechoka kimaisha.na hajui kinachoendelea kuhusu nyumba.

Swali ninalojiuliza yule boss yupo hai kweli maana miaka 10 imepita.wana nzengo au nimekosea kuipangisha.
Mwenye ushauri wowote anishauri
Una documents zozote?
Unamfahamu ndugu au mtu wake yeyote wa karibu?
Nenda ardhi kwanza ukajue status ya documents
 
Back
Top Bottom