Mungu mkubwa: Nimeokota nyumba Mbweni

Una documents zozote?
Unamfahamu ndugu au mtu wake yeyote wa karibu?
Nenda ardhi kwanza ukajue status ya documents
Akienda ardhi atakuwa amekosa pa kulala(Watamuondoa), mwache kwanza ale bahati yake.Nyumba hajaiba aliambiwa aiangalie watakuja wapangaji kukagua. Sasa mwenye nyumba hajaja miaka kumi pengine hajapata mpangaji.Si kosa la mtani wangu mtoto wa NTWARA mwache ale maisha na isitoshe hajara mshahara kwa miaka kumi, mwache ajilipe.
 
Next week ngoja nikaangalie shamba langu,Mwandege.
Wenye mashamba yetu tujitahidi kwenda kuyatembelea.
Kuna mzee mmoja ana mashamba mbalimbali mpk mengine anasema hakumbuki location,imebidi amuachie mwanae wa kiume afuatilie kwa kupitia document zilizobaki ndani.
Nikatie kipande hapo Mwandege pana mvuto sana Mkuu, na li stendi la mikoa ya kusini linamwagika hapo.Fanya Jambo mkuu.
 
Kuna jamaa mmoja kijijini kwetu enzi za JK alikamata mchongo gani sijui akawa anavuta hela ndefu. Jamaa akajenga kijijini fasta fasta akamweka kijana wa kuangalia nyumba. Kumbe jamaa akipiga mishe zake, baadhi ya hela akawa anakuja kuzificha kwenye ile nyumba bila mtu yoyote kujua. Mwaka juzi jamaa akapata ajali ya gari akafariki.

Sasa ikawa mazishi yanatakiwa yakafanyike kijijini so kijana akapigiwa simu aandae mazingira ikiwa ni pamoja na kusafisha nyumba yote na kuweka kila kitu sawa. Katika kusafisha kijana akakutana na begi limefichwa lina kitu kama 60m. Akahamisha lile begi na kulificha huku akisikilizia. Mpaka mazishi yameisha, mali za marehemu zimegawanywa, hela zilizoko benki nk hakuna alietaja hela yoyote iliopotea wala kuuliza kama kuna hela imeonekana. Msiba ulipoisha kijana akawakabidhi nyumba akasepa zake.
 
Ndio yale ya baba anajenga nyumba bila hata mke wake kujua. Matokeo yake hua hivi kama umekufa na mali imekufa
Hii miaka ya nyuma iliwahi tokea kwa profesa pekee kule kijijini kwetu alikuwa na maghorofa dar,na siku alikufa ghafla mpaka wa leo hamna anaejua mali zake zilipo
 
Iyo ilitokea pia maeneo ya mabibo Dar, kuna father mmoja alijenga nyumba kali kinoma akaimaliza akapiga adi vioo na vinishing yote.. alipoondoka hakurudi tena huu ni mwaka wa 8 unaenda wa 9. Nabhakuwai kuonekana ata ndugu watu wanaiogopa nyumba adi inaanza kuchoka rangi inakwisha
Alifariki aliletwa kuzikwa kijijini na wala kijijini hakuwahi kujenga hata nyumba ya tofali,alikuwa prof
 
Kuna mambo hupaswi sema hadharani kama hili

We ungekaa kimya huko uliko ungepangisha hio nyumba Hadi wahusike watokee wenyewe

Hivi sasa matapeli watakusaka ile mbaya na watakupata tu Maana huna hadhi wala mwendano na hio nyumba watakujua tu maadam umesema uko mbwenj .
 
Jamaa atakuwa ana manyumba mengi sana so aidha amepotea au amekufa na ajali! Na nyumba za siri hivi lazma atakuwa jamaa alikuwa anakuja mwenyewe tu haji na mtu kabisa sababu hataki watu wajue ni
Ndio yale ya baba anajenga nyumba bila hata mke wake kujua. Matokeo yake hua hivi kama umekufa na mali imekufa
yake
 
Tatizo na nyie mkijua mwanaume ana mali nyingi ndio visa huanza hapo!
Hahaaaa hamna uoga wenu tu. Kuna siku nilienda kwenye msiba mmoja huyo kaka alifariki. Mke wake alikua anajua mumewe ana shamba huko mkuranga ila hakuwahi kufika na hata hajui ni mkuranga sehemu gani. Na hakuna hata ndugu aliyekua anajua. Kaacha mtoto mdogo bila hata mali ya urithi. Bahati nzuri wazazi wake wako vizuri na ndio mjukuu pekee
 
Akienda ardhi atakuwa amekosa pa kulala(Watamuondoa), mwache kwanza ale bahati yake.Nyumba hajaiba aliambiwa aiangalie watakuja wapangaji kukagua. Sasa mwenye nyumba hajaja miaka kumi pengine hajapata mpangaji.Si kosa la mtani wangu mtoto wa NTWARA mwache ale maisha na isitoshe hajara mshahara kwa miaka kumi, mwache ajilipe.
Na kama mwenye nyumba alikuwa muuza madawa ama anafanya vitu haramu na akakamatwa na yupo jela ama la.siku akitoka tu anakuja kwenge Nyumba yake
 
a
Kisheria hio nyumba ni ya kwako!
Mali ya dhuluma haina mwisho mwema! mwisho wake mbaya!

Huwezi kuchukua mali ya mtu kirahisi hivyo!

Atafute na yeye yake

Ipo siku utabebeshwa hiyo nyumba na ardhi kichwani je ataweza?

Dawa ni Kisomo cha kumshitakia MUNGU!

Mambo yote yanakuwa bayana! Itajulikana tu mwenye nyumba yupo au kafa na kama amekufa je amekufa kwa sababu Zipi ameuwawa au amekufa kwa amri ya Mwenyezi MUNGU?

Wapo wanaadamu wakifa makaburi yao hayatoshi kuwazika!

Makaburi mengine hujaa maji kabla ya maiti kuzikwa!

Makaburi mengine unamkuta nyoka anamsubiri maiti ndani ya kaburi

Na mengi mengine ya dhuluma!

Tuache kudhulumu!
 
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.

Mimi nimezaliwa mtwara,mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili,nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie dar kutafuta maisha.

Nikatafuta vibarua vya kupalilia mikorosho ili nipate nauli ya kwenda dar maana akili yangu haipo sawa nafikiria dar tu.ilikuwa nikiona vijana wenzangu wakija kijijini kutoka dar mambo yao safi,nguo nzuri wana fedha za kutosha.nikapiga mzigo nikapata 170,000/=

Mwaka 2010 nikanda gari pruuu mpaka dar,breki ya kwanza tandika sudani.nimeshukapa pale sina ramani nashangaa shangaaa sina pa kwenda.usiku ukaingia nikapata menu nikalala stand.

Siku ya pili nikakutana na jamaa mmoja katika kupiga story nikamwambia mm natoka mtwara kumbe na yy anatoka mtwara lakini mshikaji alikuwa anafanya biashara ya kuuza mayai.basi nikamwambia mm ndio nimeingia jana yake kutoka mtwara, akaniambia mjini kugumu nikwambia nataka nijumuike na yy tufanye biashara ya mayai akaniambia hakuna tatizo.mshikaji alikuwa anaishi mbagala mgeni nani.

Siku zikaenda vijihela vyangu vikaisha mtaji ukafa kwasababu ya mahitaji ya kujikimu kila siku.kutabalisha biashara tukauza nguo za mali kauli,tembezeza sana nguo kila sehemu dar lkn nikao nikazi ngumu wakati mwingine unaporwa nguo unaporwa hela.

2011 kuna jirani mmoja alikuwa ni fundi ujenzi akanishawishi niwe msaidizi wake ktk ujenzi nimwambia hamna shida.
Site ipo mbweni,basi wasaidizi walikuwa kama watano.nyumba ilikuwa ya ghorofa moja.nyota ilianza kuwaka baada bosi mwenyumba kuniambia niwe mlinzi wa malighafi za ujenzi,mshahara 100,000/= kwangu nilimshuru mungu sana,huku nalipwa kama kibarua na mwisho wa mwezi nadaka.

Yote kwa yote site ikaisha kila kitu boss akajenga kikota kidogo akaniambia nikae pale kama mlinzi na mshahara ukawa 150,000/=nikashukuru sana.mchana naenda kufanya daika waka nyingine usiku pakulala papo.

Mwisho wa mwezi ukifika boss anakuja na funguo za nyumba yote nafanya usafi na ananiletea mshahara wangu.
Mwezi wa kwanza alikuja kama kawaida,mwezi alikuja kama kawaida,mwezi watatu alikuja akaniachia funguo za vyumba vyote akaniambia nyumba anaipangisha kwahiyo nyumba iwe safi muda wote na nisitoke kwenda kokote ili akileta mteja apate kuikagua.

Basi nilikaa na funguo nisubiri boss alete wateja miezi minne ikapita kimya na mshahara wangu nilikuwa sijapata nikaamua kwenda hewani kumtafuta boss simu yake haipatikani. Miaka 10 imepita sijamuona boss na namba yake baada ya miaka ikawa amepewa mteja mwingine.

Mwaka jana niliamua kujilipua nikaamua kuipangisha ile nyumba 700,000/= kwa mwezi.mpangaji aliponiona nikamwambia mm ndio mwenyumba alikataa maana nipo kisela na nimechoka kimaisha.na hajui kinachoendelea kuhusu nyumba.

Swali ninalojiuliza yule boss yupo hai kweli maana miaka 10 imepita.wana nzengo au nimekosea kuipangisha.
Mwenye ushauri wowote anishauri
Standard 7? Sema ukweli hapa JF umekuja kutaka nini......

Baada ya miaka 10? Kwa nini leo?

Sema ukweli mzee wa watu umemfanya nini?
 
Hakuna mali inayopotea.kaa ukijua iko siku wenye mali atajitokeza so ushauri wangu endelea kuitunza vyema.

Kuipangisha sio sawa sio makubaliana na utapoteza haki zako zote za msingi.
Mfano kama mimi ndio mwenye mali nimekuta umepangisha(sijui umeweka wapangaji kwa mda gani).

Kama umepangisha wapangaji kwa muda wote ambao sipo.
Mfano niseme umepangisha kwa miaka mitano.kodi unachukua laki saba,hapo means ni Million 42.

Sasa mimi na wewe nan atakua ana mdai mwenzake?
42-18=24.
Mzee kuwa mwaminifu baki kwenye makubaliano yenu usibadili chochote.
Iko siku wenye mali watarudi na usikae kizembe.
 
Mkuu hii hutokea nakushaurinendelea kuiangalia nyumba iko siku wahusika watakuja na vielelezo. Nina mfano mmoja juu ya hili.
Kuna jirani yangu pale kigamboni alikuwa na shamba kubwa sana kwa mazingira ya sasa yapata ekari kumi, mimi nilihamia lile eneo nilimkuta akiishi hapo na kila.mmoja alijua yeye ndie mmiliki wa lile eneo. Alikuwa analisafisha na kulima kila mwaka hakuuza hata squre meter moja ya lile shamba pamoja na dhiki aliyokuwanayo akiwa anaishi kwenye kibanda kidogo kilichochakaa. Sasa hivi majuzi kuna jamaa alikuja ndio hapo wengine tukafahamu kwamba jamaa alikuwa mlinzi aliwekwa pale miaka zaidi ya kumi na tano iliyopita kwa makubaliano ya mshahara wa sh 50,000 kwa mwezi. Baada ya jamaa kurudi majadiliano yakafanyika mlinzi akapewa ekari tano kama fidia na shukrani kwake kwani mwenye mali hakuamini kama jamaa yupo salama na hajauza hata sehemu ndogo ya lile shamba ilihali kila mmoja pale mtaani alijua kuwa ndie mmiliki.
Kuna watu waaminifu sana dunia hii
 
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.

Mimi nimezaliwa mtwara,mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili,nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie dar kutafuta maisha.

Nikatafuta vibarua vya kupalilia mikorosho ili nipate nauli ya kwenda dar maana akili yangu haipo sawa nafikiria dar tu.ilikuwa nikiona vijana wenzangu wakija kijijini kutoka dar mambo yao safi,nguo nzuri wana fedha za kutosha.nikapiga mzigo nikapata 170,000/=

Mwaka 2010 nikanda gari pruuu mpaka dar,breki ya kwanza tandika sudani.nimeshukapa pale sina ramani nashangaa shangaaa sina pa kwenda.usiku ukaingia nikapata menu nikalala stand.

Siku ya pili nikakutana na jamaa mmoja katika kupiga story nikamwambia mm natoka mtwara kumbe na yy anatoka mtwara lakini mshikaji alikuwa anafanya biashara ya kuuza mayai.basi nikamwambia mm ndio nimeingia jana yake kutoka mtwara, akaniambia mjini kugumu nikwambia nataka nijumuike na yy tufanye biashara ya mayai akaniambia hakuna tatizo.mshikaji alikuwa anaishi mbagala mgeni nani.

Siku zikaenda vijihela vyangu vikaisha mtaji ukafa kwasababu ya mahitaji ya kujikimu kila siku.kutabalisha biashara tukauza nguo za mali kauli,tembezeza sana nguo kila sehemu dar lkn nikao nikazi ngumu wakati mwingine unaporwa nguo unaporwa hela.

2011 kuna jirani mmoja alikuwa ni fundi ujenzi akanishawishi niwe msaidizi wake ktk ujenzi nimwambia hamna shida.
Site ipo mbweni,basi wasaidizi walikuwa kama watano.nyumba ilikuwa ya ghorofa moja.nyota ilianza kuwaka baada bosi mwenyumba kuniambia niwe mlinzi wa malighafi za ujenzi,mshahara 100,000/= kwangu nilimshuru mungu sana,huku nalipwa kama kibarua na mwisho wa mwezi nadaka.

Yote kwa yote site ikaisha kila kitu boss akajenga kikota kidogo akaniambia nikae pale kama mlinzi na mshahara ukawa 150,000/=nikashukuru sana.mchana naenda kufanya daika waka nyingine usiku pakulala papo.

Mwisho wa mwezi ukifika boss anakuja na funguo za nyumba yote nafanya usafi na ananiletea mshahara wangu.
Mwezi wa kwanza alikuja kama kawaida,mwezi alikuja kama kawaida,mwezi watatu alikuja akaniachia funguo za vyumba vyote akaniambia nyumba anaipangisha kwahiyo nyumba iwe safi muda wote na nisitoke kwenda kokote ili akileta mteja apate kuikagua.

Basi nilikaa na funguo nisubiri boss alete wateja miezi minne ikapita kimya na mshahara wangu nilikuwa sijapata nikaamua kwenda hewani kumtafuta boss simu yake haipatikani. Miaka 10 imepita sijamuona boss na namba yake baada ya miaka ikawa amepewa mteja mwingine.

Mwaka jana niliamua kujilipua nikaamua kuipangisha ile nyumba 700,000/= kwa mwezi.mpangaji aliponiona nikamwambia mm ndio mwenyumba alikataa maana nipo kisela na nimechoka kimaisha.na hajui kinachoendelea kuhusu nyumba.

Swali ninalojiuliza yule boss yupo hai kweli maana miaka 10 imepita.wana nzengo au nimekosea kuipangisha.
Mwenye ushauri wowote anishauri
Bongo nchi ya ajabu kweli!
Alianza huyu mtu mhuni Johannes Rebmann, eli aliokota Ml. Kilimanjaro; akaja yule mwingine naye akaokota vichwa vya treni; Sasa nawe umeibuka eti umeokota nyumba. Wewe Chinga Boy, itabidi uingizwe katika Guinness World Records!
 
Kuna baba alipangishwa nyumba na mbaba huyo, akachukua kodi yake ya mwaka. Since then hajawahi kuonekana mwaka wa 7 huu na simu hapatikani wala hajui kwake maana alikuwa anaishi mkoa tofauti.

Hao itakuwa ni wale huwa wanajenga kimya kimya bila kushirikisha ndugu wala mke na hakuna mahali wameandika.
 
Nyumba za hivi zipo nyingi sana kunduchi mbweni na masaki wamakonde wanabahati hii sanaa
Sidhani kama ni bahati tu, maana inakuwa kama coincidence???.. "waswahili" wanasema hawa watu ukiwapa walinde au kukuangalizia kiwanja basi utatokewa na mambo kama haya, either usikuendeleze tena kiwanja au ukisahau kabisa
 
Back
Top Bottom