Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,295
Hii ni sala ya kumuombea Raisi wa Jamuhuri wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete! Mungu baba muumba wa mbingu na na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana tunatanguliza shukrani zetu kwa kumaliza uchaguzi kwa amani japokua kuna kasoro zilizojitokeza hapa na pale!
Tunakuomba umpe Kiongozi huyu busara ya kuweza kuchanga karata zake vizuri katika kutuletea viongozi waadilifu katika hilo baraza la mawaziri ambalo muda si mrefu kuanzia hivi sasa watanzania wote watakua karibu na TV na Radio zao kuweza kusikiliza ni nini muheshimiwa huyu atatutangazia baraza hilo la mawaziri.
Mungu baba pia bila kusahau baraza hilo litakalotangazwa tunaomba liweze kutenda haki na kua karibu na wananchi wenye matumaini ya kupata maisha bora na kuutupilia mbali ufisadi uliokuwepo hapo kipindi cha utawala wake ndugu Kikwete japokua ufisadi sasa hivi neno hilo limebadilishwa na kua ni mtu anayechukua wake za watu!
Tunajua baba wewe ndio utakaye mtangulia Raisi huyu katika kutenda haki kwa watanzania wote ili amani na utulivu viweze kutawala katika taifa hili, tunaomba haya kwajina lako AMINA!
Mungu Ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa!
ray: