Mungu huwa anakuwa upande gani?

Maengo

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
280
29
Ndugu wanaJF, nimejaribu kujiuliza hili swali ila sikupata majibu kabisa! 'HIVI MUNGU HUWA ANAKUWA UPANDE GANI IKITOKEA UPANDE MMOJA UNADHULUMU NA MWINGINE UNADAI HAKI? Kama anakuwa upande wa haki, ni kwanini basi upande wa dhuluma huwa unashinda? Na kama anakuwa upande wa dhuluma, ni kwanin akae upande huo ilihali anajua wapi haki ilipo?

kwa maana hiyo kama Mungu yu upande wa Watz waliopigika na maisha, kwanin basi anakubali MAGAMBA washinde kwa ujanjaujanja na waendelee kutunyanyasa?
 
Biblia inasema Bwana akiwa upande wako hakuna wa kukushinda. Pia sehemu nyingine anasema lazima mtii mamlaka zote kwasababu zimetoka kwa Mungu.
 
Tatizo ni kwamba kazi za Mungu huwa hazihojiwi. NI dogma. Kwa hiyo hata ukiuliza maswali yakoje hutakaa upate jibu, kwa kuwa si yeye wala watumishi wake watakuwa tayari kuyajibu. Watumishi wengi wanaogopa kuquestion ukuu, mamlaka na maamuzi ya Mungu.
 
Yote ya yote Mungu humsidia yule anaeonyesha jitihada binafsi za kujisaidia kwanza yeye,
Sasa isiwe umetulia zako tu kwenye PC ya internet cafe au Kisimu chako cha mchina muda wote kazi kulalamikia tu Magamba halafu unataka mungu akuunge mkono katiko hilo, never!!!
Ingia barabarani, andamana mkuu!!!
 
usiridhike na ule msemo wa kiswahili wa " haki ya mtu haipotei" sisemi kuwa msemo huu ni wa uongo, lahashaa! ila ni kwamba msemo una maana kwamba hata kama utadhulimiwa hapa duniani siku ya mwisho (kiama) utalipwa kile ulichodhulumiwa na yule aliyekudhulumu. ila hapa duniani kwa kweli ni kwenda mbio inavyowezekana kuipata haki yako. Si sahihi pia kusema Mungu anakaa upande wa wadhulumifu kwani yeye ameweka wazi haki na batili sisi wanadamu ndo tunazilinda na kuzipotosha haki. hata hivyo unapomuomba Mungu kwa dhati basi naye hukupa msaada. ila hii mungu nisaidie tu kavukavu we andika maumivu tu.
 
anakuwa upande wa waaminio kuwa yeye ni BWANA wa mabwana na MUNGU wa miungu.
 
Biblia inasema Bwana akiwa upande wako hakuna wa kukushinda. Pia sehemu nyingine anasema lazima mtii mamlaka zote kwasababu zimetoka kwa Mungu.
<br />
<br />

Sio mamlaka zote zinatoka kwa mungu! Ndio maana tumeshuhudia mamlaka kama za akina Hitler, Tailer. Makaburu na nyinginezo. Na unatakiwa utambue uwepo wa mamlaka ya shetani!
 
Sio mamlaka zote zinatoka kwa mungu! Ndio maana tumeshuhudia mamlaka kama za akina Hitler, Tailer. Makaburu na nyinginezo. Na unatakiwa utambue uwepo wa mamlaka ya shetani!
Mkuu, unaweza kunitajia nchi mbili tu ambazo mamlaka zake zinatoka kwa mungu
 
Biblia inasema Bwana akiwa upande wako hakuna wa kukushinda. Pia sehemu nyingine anasema lazima mtii mamlaka zote kwasababu zimetoka kwa Mungu.

Duh.......kwa hiyo mwaka jana alikuwa upande wa CCM na tumtii Kikwete sio?
 
Njia za Mungu hazichunguziki na huwezi kupata majibu ya maswali yako na ujue pia shetani yupo kazini na wakati mwingine Mungu anaacha tujaribiwe ili aone tutafanyaje tutaendelea kumwamini au tutakata tamaa na kuishia kulalamika.
 
Mi ninacho amini ni kuwa Mungu huwa ana msaada wowote kwa mtu yeyote yule hapa dunia...ila tu binadamu wamwamua kuwalaghai binadamu wenzao kuwa Mungu huwa anasaidia
 
Ndugu wanaJF, nimejaribu kujiuliza hili swali ila sikupata majibu kabisa! 'HIVI MUNGU HUWA ANAKUWA UPANDE GANI IKITOKEA UPANDE MMOJA UNADHULUMU NA MWINGINE UNADAI HAKI? Kama anakuwa upande wa haki, ni kwanini basi upande wa dhuluma huwa unashinda? Na kama anakuwa upande wa dhuluma, ni kwanin akae upande huo ilihali anajua wapi haki ilipo?

kwa maana hiyo kama Mungu yu upande wa Watz waliopigika na maisha, kwanin basi anakubali MAGAMBA washinde kwa ujanjaujanja na waendelee kutunyanyasa?

Ukweli ni kwamba kuna nguvu kuu mbili zinazoongoza dunia,...nguvu ya Mungu na ile ya shetani,..sasa hapo ndio ndio sijaelewa mpaka sasa ipi ina nguvu zaidi ya nyingine,....maake wanaseama hata ukitaka ufanikiwe iwe kwa mali,na vitu vingine ni la lazima either ummtumikie Mungu au shetani,....

Tunasikia hata hizi habari za kusadikika za freemasons kua ni watu wenye mafanikio makubwa na ni waabudu shetani,......lakn kwa upande mwingine kuna mafanikio ya kimungu,......kwa hiyo inawezekana kabisa hao magamba ni waumini wa nguvu hasi ya shetani na ndio anayewawezesaha kufanikiwa.

Haya mambo ya kiimani bana,...........................who knows bana?
 
Njia za Mungu hazichunguziki na huwezi kupata majibu ya maswali yako na ujue pia shetani yupo kazini na wakati mwingine Mungu anaacha tujaribiwe ili aone tutafanyaje tutaendelea kumwamini au tutakata tamaa na kuishia kulalamika.

Ulijuaje?Halafu anafaidika na nini?
 
Back
Top Bottom