Mungu huonesha njia pasipo na njia

May 22, 2017
65
298
YAPO MAWILI MATATU YA KUJIFUNZA HAPA

Anaandika Goliath Mfalamagoha
_
Boniface Murage, mkazi wa Embakasi, Nairobi nchini Kenya, amekuwa gumzo katika vyombo vya habari Afrika Mashariki baada ya kukamatwa akijaribu kumtorosha mwanae Hospitali kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu.

Murage alishindwa kulipa Shilingi 56,000/= za Kenya (sawa na 1.3 milioni za Tanzania), ambazo ni bill ya mtoto wake aliyepatiwa matibabu hospitali ya Kenyatta.

Gharama hizi ni kubwa sana kutokana na uhalisia wa hali yake ya kiuchumi na hivyo akaamua kumtorosha mtoto wake kwa kumficha kwenye Begi.

Askari walipofungua begi walimuona mtoto. Murage akakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Jumanne February 19 mahakama ilimkuta na hatia na kumhukumu kifungo cha nje cha miezi mitatu na kutakiwa kulipa gharama hizo.

Tukio hili limegusa hisia za watu wengi nchini Kenya, na baadhi walijitokeza kumuwekea dhamana, na wengine kumlipia gharama za mawakili.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amelipia gharama zote za hospitali na amemfanyia shopping mtoto huyo ya mahitaji yake muhimu ikiwemo nguo, chakula na vifaa vya kuchezea. Pia amempa Murage offer ya kazi ili aweze kutunza familia yake.

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino amempatia Murage KSH 200,000/= (sawa na 4.5Milion za Tanzania) kama alivyoahidi siku Murage anakamatwa.

Mkuu wa Polisi Embakasi SSP Tamo Sanaiet alifika hospitali kulipa bill lakini akaambiwa Sonko ameshalipa. Hivyo akamtafuta Murage na kumkabidhi KSH 56,000/= ambazo angelipa hospitali. Pesa hizo ni mshahara wake.

Kuna mengi ya kujifunza katika kisa hiki cha Murage. Lakini kwa uchache;

Mosi ni namna kina baba wanavyohangaika ili kutunza familia zao. Hujui anapitia mangapi kuhakikisha mnakuwa salama. Anapitia mangapi kuhakikisha mnapata chakula. Anapitia mangapi kuhakikisha bili zinalipwa. Anapitia mangapi kuhakikisha mnasoma. Anapitia mangapi kuhakikisha mnakuwa na afya bora.

Pili, haijalishi unapitia magumu mangapi, usikate tamaa. Hali yako ya sasa ni ya muda tu. Ipo siku itatoweka, na hutabaki kama ulivyo. Pengine jaribu lako ndio njia ya kukufikia mafanikio yako. Murage hakujua kama kitendo cha kumtorosha mwanae kingebadili kabisa maisha yake. Mungu hufanya njia pasipo na njia.

Pia kitendo Afisa wa Polisi kuamua kutoa mshahara wake kumpa Murage ni ishara kwamba utu ni tunu muhimu kwa wakenya. Polisi haohao waliomkamata na kumpandisha kizimbani ndio wanatoa hela wanampa. That means walimkamata tu ili kukidhi matakwa ya kisheria. Wakaiacha sheria ichukue mkondo wake, lakini haikuwaondolea ubinadamu wa

MUNGU HUFANYA NJIA PASIPO NA NJIA!

Amen.
 
Mtazamo Ya Kujifunza ni Mingi Kwenye hili...! Mnasemaje Watakaojifunza Mbinu Za Kutoroka Deni La Hospili Kwa Kumfanya mtoto ni Kifurushi na kumuingiza Ndani Ya Begi..? Nyie Wakenya Mnatakiwa Muwafundishe Watu wenu Njia Sahihi pia za Kutatua Matatizo..!
 
Ila sidhani kama kuna Polisi wa Tanzania mwenye roho hiyo,naona moja ya mafunzo yao ni ukatili na roho mbaya
 
Back
Top Bottom