Mungu humpa kila mtu utajiri ila mtu huukataa

Ghost boss

Member
May 3, 2019
33
56
Kuna habari inatembea sasa ikimwonesha mvuvi anayedaiwa kuvua samaki mwenye thamani ya pesa za Tanzania billion 6 na anadaiwa baada ya kumvua alimla na wanakijiji wenzie. Kwa haraka haraka hakuna anayeweza kumlaumu jamaa maana angejuaje kama thamani yake ndio hiyo.

Ila swali nikuwa huyu jamaa si mvuvi, anavua kibiashara? Kama anavua kibiashara labda tungesema angemuuza lakini hapana asingeweza, ila alijua leo amepata samaki la ajabu ajabu hivyo akapiga nalo picha kuonyesha ni ajabu, jamaa alipiga picha na billion sita bila kujua the end akamla.

Ila nimejifunza kitu kupitia huyu mvuvi kwamba unapopatwa na jambo lolote lile lisilo la kawaida Basi jipe muda huwenda muda utatibu hilo jambo au ndio fursa ya kufanikiwa kupitia jambo ilo. Mimi siwezi kushangaa alichokifanya cha kumla, sio dhambi ila dah!

Kala billion sita akiwa bado kijana sana. Binafsi niseme tu kwamba kila mtu awe amesoma, hajasoma, naishi mjini au kijijini, awe mweupe au mweusi awe vyovyote vile Mungu ajali yeye atampa fursa ya kuwa tajiri ila kuuchukua ni.😯

Nakumbuka niliwahi sema jambo laajabu au wazo la ajabu ambalo kila MTU analistajabia ilo ndilo lenye kuleta mafanikio ila jambo la kufanana ni umasikini tu. Jamaa alivua samaki la kipekee bila kujua upekee ndio utajiri ila akamla na kijiji.

Simlaumu najua hakujua ila somo tumepata.
 
Huyo jamaa angekuwa na taarifa sahihi za yule samaki angeweza kutajirika lakini hakuwa na ufahamu wowote kuhusu yule samaki hivyo alichobaki nacho ni majuto mara baada ya hizo kampuni za viumbe wa baharini kuja kutoa tangazo lao.
 
Somo la Mungu hapo, linaamaanisha ukipata utajiri kula na wenzako! Mungu amejua akimpa hizo b 6 huyo Jamaa asingegawa Mpunga kwa Wanakijiji wenzie, angefanya kama Matajiri wengi wanavyofanya ya kuzidi kujilimbikizia Mali zaidi!! mwisho wa siku yote ni Mipango yake Mungu.
 
Ila haya mambo huwa hayana formula, unaweza kusema kuwa ujipe muda, wajanja nao wakaja wakakuzidi maarifa ukakosa kila kitu, ni bora hata alivyoambulia kumla huyo samaki...
 
Somo la Mungu hapo,linaamaanisha ukipata utajiri kula na wenzako! Mungu amejua akimpa hizo b 6 huyo Jamaa asingegawa Mpunga kwa Wanakijiji wenzie,angefanya Kama Matajiri wengi wanavyofanya ya kuzidi kujilimbikizia Mali zaidi!! mwisho wa siku yote ni Mipango yake Mungu!!
Thinking gani hii

Angeajiri watu wangapi angepata hiyo pesa kwako wao kula uyo samaki ambaye washampeleka chooni ni bora zaidi.
 
Mimi nashauri uyo jamaa arudi sehemu ile ile alipolivua hilo lisamaki yawezekana akapata samaki la tilioni moja
 
Back
Top Bottom