Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
MUNGU HASAMEHI DHAMBI; TUACHE KUDANGANYANA
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Haya nayo niliandika, kusudi usije ukasema hukuambiwa. Nami najua siwezi kuukimbiza muda, nao umekuwa mchache, umeniacha wala siuoni tena. Basi ikiwa muda wetu wa kuishi Duniani ni mdogo yafaa tuishi kwa tahadhari.
Ni mimi Taikon mwana kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili, Irukayo huku na huku.
Nami nimechunguza mienendo ya muda. Tena mienendo ya nguvu za nishati nimezidadisi. Hata mabadiliko ya Maada nimeyatafakari. Nako sikupata la ziada isipokuwa nalipata huzuni na uchovu.
Mungu hasamehi dhambi bali husamehe Makosa
Ipo tofauti ndogo ila ya muhimu baina ya MAKOSA na DHAMBI ingawaje yote hufanana katika utendaji.
Makosa ni kitendo au hali ya kutofanya kitu kilichosahihi pasipo kujua au kama ajali.
Dhambi ni kitendo au hali ya kutofanya kitu kwa usahihi ukiwa unajua sio sahihi.
Dhambi haitokei kama ajali.
Makosa yanatokea kama ajali
Dhambi ni mchakato unaohitaji kupangwa
Makosa sio mchakato, hauhitaji kupanga
Kisayansi Makosa huitwa Errors
Kwa mfano ninapoandika hapa ninaweza kukosea kuandika bila dhamiri huitwa typing Errors.
Dhambi ni dhamiri/kusudi linalohitaji utayari.
Makosa sio Dhamiri
Kisheria; wale watu wa sheria kama Wanasheria, mahakimu na Majaji wataungana na mimi kuwa kuna Makosa ya kukusudia na yale yakutokukusudia.
Makosa ya Kukusudia huitwa Uhalifu
Na Mahakamani huwezi samehewa kwa uhalifu lakini unaweza samehewa kwa Makosa.
Kwa upande wa kiroho. Mungu hajawahi kusamehe Dhambi na kamwe hatakuja kusamehe dhambi zetu.
Dhambi ni Uasi wa makusudi kabisa.
Ndio maana vitabu vinaeleza usimjaribu Bwana Mungu wako.
Viongozi wa Dini hutufundisha kuwa Mungu anasamehe dhambi jambo ambalo ni uongo wa mchana. Mungu hajawahi kusamehe dhambi na hatakuja Awahi kusamehe dhambi.
Mshahara wa dhambi ni mauti. Haki ya dhambi ni kifo.
Wote tunajua Mungu ni mwenye Haki. Kusema Mungu anasamehe ni kumuondolea sifa ya kuwa na HAKI. Jambo ambalo sio kweli.
Sitajali kama utanikubalia au utakataa ukweli upo hivyo Mungu hasamehi dhambi. Labda tujidanganye.
Ndio maana watoto wadogo hawana dhambi, ila wanamakosa wao hufanya pasipo kujua hivyo haziitwi dhambi bali Makosa.
Nilishasema dhambi ni dhamiri. Makusudi.
Halikadhalika na wema ni dhamiri ya mtu. Mtu anaweza akafanya wema lakini asijue ni wema. Huo hauitwi wema. Halikadhalika mtu anaweza akafanya Dhambi asijue ni dhambi hiyo haiitwi dhambi bali makosa
Mtu asiye na dhamiri ni kama mnyama tuu. Hana wema wala hana ubaya
Ni kama kichaa au mwendawazimu. Hakuna dhambi au wema kwa kichaa au mwendawazimu kwani hawafanyi kwa dhamiri.
Ndio maana hata Mahakamani kichaa hata hatia. Au mnyama hana hatia isipokuwa anayemmiliki.
Ukiona unafanya jambo lolote baya kwa kukusudia jua hutasamehewa Milele zote.
Watu hujidanganya na kudanganywa kuwa Mungu anasamehe hivyo hufanya dhambi makusudi kwa maana wanajua Wataomba msamaha.
Mbona hawafanyi hivyo hata kwenye mahakama za Duniani?
Ikiwa duniani haipo hivyo sembuse kwa Mungu!!
Kufanya kosa kwa Makusudi(Dhambi) ni kukufuru Mungu. Na hili hata Yesu alilitolea maelezo kuwa dhambi ya Kukufuru haina Msamaha. Akiwamaanisha dhambi ya Makusudi.
Nimeshaeleza dhambi ni mchakato
Ukitaka kuzini lazima upange na uweke mikakati.
Lazima utumie gharama na wakati unafanya hayo kuna nafsi yako inakuonya lakini unaamua kukaidi.
Kinachomfanya mtu ajifiche atendapo dhambi ni nafsi yake kuwa na hatia.
Dhambi ni aibu
Makosa ni sehemu ya kujifunza
Ndio maana watoto wadogo wakoseapo hawaoni aibu kwani bado hawana dhamiri.
Dhambi ni Uamuzi
Makosa ni ajali
Mungu hakumsamehe na hatamsamehe Shetani kwa sababu alidhamiria
Mungu hakumsamehe Adam na Hawa kwa sabab walidhamiria.
Mungu sio mpumbavu yaani atuambie jambo Fulani ni kosa tusifanye alafu kwa ukaidi wetu tunafanya alafu atusamehe😀😀😀 hizo tunaita dharau.
Huwezi mdharau Mungu kwa kisingizio cha Msamaha.
Fundishola Msamaha linafundishwa na kutumika vibaya kwa maslahi ya waovu
Yesu alipokuwa msalabani alisema; wasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo.
Hii ni kusema wasiojua walitendalo ndio husamehewa.
Kuna aina mbili ya Kutokujua jambo;
1. Kutokujua kabisa
2. Kutokujua kwa kusahau
1. Kutokujua Kabisa
Hii ni ile hali mtu hajui kitu kabisa yaani hajawahi kufundishwa au kujifunza. Hajawahi kusikia wala kuona
2. Kutokujua kwa Kusahau
Hii ni ile hali mtu alikuwa anajua jambo lakini kwa udhaifu wa kibinadamu akasahau
Asiyejua kabisa na aliyesahau ni sawa sawa tuu.
Ndio maana kwenye mtihani wale ambao hawajui kabisa na wale waliosahau walivyofundishwa hufeli.
Hata hivyo mambo hayo mawili kiroho hupimwa na dhamiri.
Dhamiri haidanganyi
Mtu aliyefanya dhambi utamjua kwani lazima atarudia hata mara Mia licha ya kuomba msamaha
Mtu aliyefanya Makosa; harudii akishambiwa jambo hilo ni dhambi.
Kuomba msamaha mara kwa mara kwa kosa lile ni kumdhihaki Mungu. Na Mungu hadhihakiwi.
Kama neno msamaha lisingekuwepo Duniani bas dhambi zingekuwa chache sana.
Lakini kadiri fundisho la msamaha linavyoenezwa ndivyo dhambi zinavyozidi kuongezeka.
Msamaha ni neno ambalo linatumiwa vibaya na viongozi wa dini au hawalielewi vyema.
Mungu hatatusamehe dhambi zetu.
Unazini kwa makusudi kabisa alafu unategemea Mungu a kusamehe? Acha dhihaka
Unaua kwa makusudi alafu Mungu a kusamehe?
Unaiba, unagonga wake za watu kwa makusudi licha ya kujua ni dhambi bado utake msamaha?
Mwisho; Tusifanye dhambi kwani kusamehewa hakupo
Wale wa Neema waendelee kujidanganya.
Note: Kizazi hiki sio Bora kama kizazi kilichopita. Na kinyume chake ni sahihi pia.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro