Mungu hadhihakiwi, Farao ni mfano wa watawala viburi wa Afrika

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,456
12,666
Kwa mfuatiliaji/msomaji wa biblia yeyote anaelewa vyema kisa cha Firauni/Farao wa Misri katika kitabu cha kutoka. Firauni bwana alikuwa jeuri kwelikweli.

Kisa cha wana Israel kutoka Misri wakiongozwa na Musa kiliweka mwanzo na mwisho wa utawala dharimu wa bwana/mfalme FIRAUNI aliyekuwa kiburi na fedhuli kuliko yeyote hapa ulimwenguni.

Kilichomponza firauni ni kiburi na kujifanya hashauriwi wala kupangiwa na mtu juu ya utawala wake, licha ya kuwa aliwatawala watu waliokuwa na sheria/torati/katiba au utaratibu wa maisha yao hasa waisraeli Firauni alidharau na kuwakataza washishiriki kumuabu Mungu wao, na akatamani watumie wao kuongea juu ya utawala wake.

Kiburi, jeuri na ufedhuri wa farao uliongezeka huku akiamini ukubwa wa jeshi lake wana wa Israel wasingelimfanya chochote, Bwana wa Majeshi (JEVOHA SHAMWAA) alimtazama firauni kutoka juu akachukizwa na jeuri yake.

Alimuandaa Musa mkombozi kwa kukulia ndani ya familia ya Firauni baada ya binti yake kumuokota Musa mtoni kufuatia hofu ya firauni juu ya utawala wake na badae Musa kuandaliwa kumpa mapigo matakatifu fedhuli Firauni.

Hakika Mungu hajaribiwi, na wala siyo huyu firauni huyu Firauni anayetangaza kutojaribiwa, Bwana Mungu kumkomesha Firauni alimtia MOYO MGUMU, firauni akawa mkaidi akapuuza torati/katiba ya watu na majighambo lukuki. Licha ya MAPIGO 10 firauni ukaidi wake ulidumu na mpango wa Mungu ulikuwa Firauni aangamie.

Safari ya wanawa israel ilipoanza tamaa ya Firauni iliibuka tena akaamua kuwafuata ata Mungu alipofanya muujiza kwa kupasua bahari wana wa Israel wakavuka firauni hakukumbuka kuwa alipaswa kuchukua tahadhari alizamia majini moja kwa moja na bahari ilimmeza firauni na ndiyo ikawa mwisho wa utawala wake wa kifedhuli.

Kusema kweli nchi nyingi za kiafrica wapo firauni wengi, kama kagame, Mgabe kuzama tayari na bahari, Kabila, Nkruzinza, Mseveni, Zuma/tayari kazama, na farao wa nyumbani hawa wote UGUMU wa moyo wao umewekwa ba Mungu ili waangamie.

Hawa wote ni wakristo wanaomwomba Mungu yuleyule aliye na hasira juu yao, anachowafanyia ni kuwajaza Mioyo migumu na mwisho cha mtema kuni watakiona!

Alamski....
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
 
Hahahah..! Bado mna mnamatumaini..
 
Ninani alimfanya farao kuwa kiburi,mkaidi na mwenye roho ngumu?
Kutoka 10:1, 27.
BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionyesha ishara zangu hizi kati yao; Lakini BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape ruhusu wana wa Israeli wapate kuondoka.
 
Hizo habari zenu za Mungu zinatuchosha,mwende mkamwambie mbona mzungu na hasa mmarekani ndio anaonekana kama Mungu.basis mwambieni aturejeshee japo amani.vinginevyo ataendelea kudhihakiwa tu japo mnaona na hamtaki kukubali.
 
Wauliza wamarekani kauli mbiu ya taifa lao watakwambia "IN GOD WE TRUST"
 
Kwamba ndie anawatuma wakawaue wenzao.au tuamini wanaotuambia ni gold oil na gas.
Tunahimizwa kuwa na subira, tuombe Roho Mtakatifu atujalie saburi, maana hima Bwana aja kutusaidia.

Jamaa kila siku muniombee uzuri wa Mungu anachungulia mioyoni mwetu na kujua mawazo yetu na matendo yetu maovu tuyatendao gizani.
 
wakawadanganye nyau wa kikristo,sisi waabudu mizimu wametukosa.
 
Kwa mfuatiliaji/msomaji wa biblia yeyote anaelewa vyema kisa cha Firauni/Farao wa Misri katika kitabu cha kutoka. Firauni bwana alikuwa jeuri kwelikweli.

Kisa cha wana Israel kutoka Misri wakiongozwa na Musa kiliweka mwanzo na mwisho wa utawala dharimu wa bwana/mfalme FIRAUNI aliyekuwa kiburi na fedhuli kuliko yeyote hapa ulimwenguni.

Kilichomponza firauni ni kiburi na kujifanya hashauriwi wala kupangiwa na mtu juu ya utawala wake, licha ya kuwa aliwatawala watu waliokuwa na sheria/torati/katiba au utaratibu wa maisha yao hasa waisraeli Firauni alidharau na kuwakataza washishiriki kumuabu Mungu wao, na akatamani watumie wao kuongea juu ya utawala wake.

Kiburi, jeuri na ufedhuri wa farao uliongezeka huku akiamini ukubwa wa jeshi lake wana wa Israel wasingelimfanya chochote, Bwana wa Majeshi (JEVOHA SHAMWAA) alimtazama firauni kutoka juu akachukizwa na jeuri yake.

Alimuandaa Musa mkombozi kwa kukulia ndani ya familia ya Firauni baada ya binti yake kumuokota Musa mtoni kufuatia hofu ya firauni juu ya utawala wake na badae Musa kuandaliwa kumpa mapigo matakatifu fedhuli Firauni.

Hakika Mungu hajaribiwi, na wala siyo huyu firauni huyu Firauni anayetangaza kutojaribiwa, Bwana Mungu kumkomesha Firauni alimtia MOYO MGUMU, firauni akawa mkaidi akapuuza torati/katiba ya watu na majighambo lukuki. Licha ya MAPIGO 10 firauni ukaidi wake ulidumu na mpango wa Mungu ulikuwa Firauni aangamie.

Safari ya wanawa israel ilipoanza tamaa ya Firauni iliibuka tena akaamua kuwafuata ata Mungu alipofanya muujiza kwa kupasua bahari wana wa Israel wakavuka firauni hakukumbuka kuwa alipaswa kuchukua tahadhari alizamia majini moja kwa moja na bahari ilimmeza firauni na ndiyo ikawa mwisho wa utawala wake wa kifedhuli.

Kusema kweli nchi nyingi za kiafrica wapo firauni wengi, kama kagame, Mgabe kuzama tayari na bahari, Kabila, Nkruzinza, Mseveni, Zuma/tayari kazama, na farao wa nyumbani hawa wote UGUMU wa moyo wao umewekwa ba Mungu ili waangamie.

Hawa wote ni wakristo wanaomwomba Mungu yuleyule aliye na hasira juu yao, anachowafanyia ni kuwajaza Mioyo migumu na mwisho cha mtema kuni watakiona!

Alamski....
Acha kufananisha vitu visivyofanana kabisa, Farao alikuwa anawaendesha wayahudi ambao hawakuwa ni raia wa asili wa nchi yake (watumwa). Hao wote umewaorodhesha wanaendesha nchi zao wenyewe.
 
Kakuunga mkono dadaangu.Na kila mtawala kesho mbele ya mungu ataulizwa ametumiaje utawala wake ?
 
PIGO la pili mtu anatokea kamasi akatubu hakuna namna..
 
Back
Top Bottom