bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,668
Kwa mfuatiliaji/msomaji wa biblia yeyote anaelewa vyema kisa cha Firauni/Farao wa Misri katika kitabu cha kutoka. Firauni bwana alikuwa jeuri kwelikweli.
Kisa cha wana Israel kutoka Misri wakiongozwa na Musa kiliweka mwanzo na mwisho wa utawala dharimu wa bwana/mfalme FIRAUNI aliyekuwa kiburi na fedhuli kuliko yeyote hapa ulimwenguni.
Kilichomponza firauni ni kiburi na kujifanya hashauriwi wala kupangiwa na mtu juu ya utawala wake, licha ya kuwa aliwatawala watu waliokuwa na sheria/torati/katiba au utaratibu wa maisha yao hasa waisraeli Firauni alidharau na kuwakataza washishiriki kumuabu Mungu wao, na akatamani watumie wao kuongea juu ya utawala wake.
Kiburi, jeuri na ufedhuri wa farao uliongezeka huku akiamini ukubwa wa jeshi lake wana wa Israel wasingelimfanya chochote, Bwana wa Majeshi (JEVOHA SHAMWAA) alimtazama firauni kutoka juu akachukizwa na jeuri yake.
Alimuandaa Musa mkombozi kwa kukulia ndani ya familia ya Firauni baada ya binti yake kumuokota Musa mtoni kufuatia hofu ya firauni juu ya utawala wake na badae Musa kuandaliwa kumpa mapigo matakatifu fedhuli Firauni.
Hakika Mungu hajaribiwi, na wala siyo huyu firauni huyu Firauni anayetangaza kutojaribiwa, Bwana Mungu kumkomesha Firauni alimtia MOYO MGUMU, firauni akawa mkaidi akapuuza torati/katiba ya watu na majighambo lukuki. Licha ya MAPIGO 10 firauni ukaidi wake ulidumu na mpango wa Mungu ulikuwa Firauni aangamie.
Safari ya wanawa israel ilipoanza tamaa ya Firauni iliibuka tena akaamua kuwafuata ata Mungu alipofanya muujiza kwa kupasua bahari wana wa Israel wakavuka firauni hakukumbuka kuwa alipaswa kuchukua tahadhari alizamia majini moja kwa moja na bahari ilimmeza firauni na ndiyo ikawa mwisho wa utawala wake wa kifedhuli.
Kusema kweli nchi nyingi za kiafrica wapo firauni wengi, kama kagame, Mgabe kuzama tayari na bahari, Kabila, Nkruzinza, Mseveni, Zuma/tayari kazama, na farao wa nyumbani hawa wote UGUMU wa moyo wao umewekwa ba Mungu ili waangamie.
Hawa wote ni wakristo wanaomwomba Mungu yuleyule aliye na hasira juu yao, anachowafanyia ni kuwajaza Mioyo migumu na mwisho cha mtema kuni watakiona!
Alamski....