Mungu awalaani madaktari na wanaharahati iwapo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu awalaani madaktari na wanaharahati iwapo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wakuziba, Jun 29, 2012.

 1. w

  wakuziba Senior Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siyo kawaida yangu nichangiapo au kuanzisha thread kutumia lugha ya laana. mazingira yaliyopo yamenilazimu kufanya hivyo. kazi ya udaktari ina miiko yake. inahitaji daktari awe na sifa maridhawa. miongoni mwake ni ukarimu, ucheshi, bashasha, huruma, uadilifu, utunzaji siri, ukweli, upendo nk...... sifa kuu ni lazima awe na utu.


  daktari ajue kuwa ansimamia UHAI wa binadamu. binadmau akiwa mgonjwa anahitaji tiba ili apone. asipopewa tiba pana uwezekano mkubwa akafariki. hii inaonesha unyeti na umuhimu wa kazi ya utibabu. madaktari wanafaa kulijua hilo!


  JE NI SAHIHI KWA DAKTARI KUGOMA?

  nionavyo mimi siyo sahihi. katika hali yoyote ile, dr hafai kugoma. akigoma maana yake ni kwamba ameamua kuua watu. daktari anatamka kuwa anagoma! ili watu wafe! nchi tunaipeleka wapi? mishahara yetu iko chini kwa ujumla. lkn licha ya mishahara midogo, madaktari wamekua wakilipwa zaidi ya watumishi wengine, ukiweka kando wabunge. serikali ilikua ktk mgogoro na madaktari baada ya kugoma miezi 2 iliopita. madaktari walitanguliza madai zaidi ya kumi. serikali ilijaribu kutatua baadhi ya madai yao yakiwemo kubadilisha waziri, naibu wake na katibu mkuu nyoni. wameongezewa marupurupu kadha wa kadha. wameahidiwa kuwa mambo yaliyosalia ktk maombi yao. hadi mwezi wa nane yatakua yameshatatuliwa. ile mashine kuu ya vipimo ilyoharibika wameagizwa mafundi kutoka kiwanda kilichoitengeneza au watanunua nyengine.  VITUKO VYA WANAHARAKATI WA BONGO  wazungu wameasisi taasisi za kutetea haki za binadamu. zina mema na mbaya. tangu mgomo uliopita, wanaharakati wamekua bega kwa bega na madaktari wakiwasihi kuendeleza mgomo! nitoe mfano mmoja. mama kijo ni mkurugenzi wa LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE (LHRC). ni taasisi ya kisheria ya kutetea haki za binadamu. HAKI KUU ya binadamu NI HAKI YA KUISHI. badala ya kusihi madaktari kutibu wagonjwa ili waishi, wanawahamasisha kugoma ili wagonjwa wafe. huu ndiyo uanaharakati!!!!? nauliza huu ndiyo utetezi wa haki za binadamu!? wanatetea nyongeza ya mshahara na kuignore haki ya kuishi. wangewasihi madaktari waendelee na matibabu ili nao wasaidiane nao kudai madai yao. mbona serikali ilikua imeonesha mfano. imejibu na kutatua 60% ya maombi ya madaktari!


  ANGALIENI KITUKO HIKI


  mama kijo hajali watanzania kwa mamia wanaokufa kutokana na kukosa huduma ya kutibiwa. amehangaika kumtoa ulimboka mwabepande na kumuwahisha icu ili akatibiwe. uli ni bora kuliko watanzania wengine? mbona yeye amepewa huduma ya kutibiwa!? kwa nini wengine wananyimwa huduma!?

  nawasihi wanaharakati na madaktari pamoja na wanasiasa wasitishe kuunga mkono mgomo. wasipofanya hivyo MUNGU AWALAANI WOTE.

  wakatabahu: wakuziba
   
 2. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nenda kazibe mdomo wako huo mchafu wakuziba
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Huo uchangamfu, bashasha, tabasamu n.k vinaletwa na conducive wprking environment!!! UNatoka nyumbani kwako watoto hawajapata chai, Ada unadaiwa... Ofisini hakuna dawa tabasamu litoe wapi? Kama unadhani Madaktari ni watu Spesho ungeishauri serikali itekelze madai yao kwenye ule mgomo wa kwanza. Au umesahahu hii ni mara ya tatu kwa madaktari kugoma? Hata la kuwafukuza kina Mponda na Lucy Nkya lilihitaji gharama?
  Na mwisho... Kati yako wewe, John Komba, Livingstone Lusinde, Stevem Wassira, Maji Marefu na Martha Mlata nani alikuwa anshika nafasi ya kwanza kutoka mwishoni darsani kwenu?
   
 4. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  akulaani na wew uliacha akili zako kitandani...go end pick it then come again......hayo ni matokeo ya Udhaifu wa JK na serikali yake.over
   
 5. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Msimulaumu sana ndo mwisho wake wa kufikiria hapo
   
 6. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umetumwa na MR. LITAKALO KUWA NA LIWE... Kazi imekamilika sasa nenda kachukue posho yako.
   
 7. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  siasa hizi zitatumaliza nawaomba tuwe na utu tuweke uhai mbele kabla ya maslahi. Nawashauri madaktari warudi kazini waokoe maisha ya watz wasio na hatia kisha 2015 wasiichague ccm labda madai yao yatasikilizwa. Kumbukeni wengi wenu mmepata elimu yenu baada ya huyu maskini kikamuliwa.....Mbona rahisi sana la sivyo watz. hawatawaelewa
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,136
  Trophy Points: 280
  Ningekuona wa maana iwapo laana zako zingeelekezwa kwa serikali ya CCM kwa kushindwa kutatua kero za madaktari
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mungu huwa halaani hovyo hovyo kama unavyodhani eti kisa wakubwa wamekosea...
   
 10. m

  maingu z Senior Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu halaani wapigani haki, mtalaaniwa wajinga wajinga kama ninyi ambao mmeshindwa hata kutambua haki zenu badala ya kuibana serikali iwape madai yao kwasababu ndo tuliowapa dhamana ya kuendesha nchi kwa niaba yetu, wanachi hatuna mkataba na ma daktari, sisi tuna mkataba na serikali na ndo maana kila baada ya miaka mitano wanakuja kutuomba kula, uliona wapi daktri anakuja kwa wananchi kuomba akasomee na kuwa daktri. DU tatizo bado watz ujinga umetumaliza watu kama hawa ni vikwazo vya maendeleo na mabadiliko yakija inabidi watu wa aina hii wapewe elimu ya bure kwani ni mzigo sanaaa hata kwenye maendeleo kwani si rahisi kubata ubunifu kwa watu wa aina hii wenye mawazo mgando
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  [h=2]MNYIKA-Taifa na Madaktari: Tumefikia hapa tulipo kwa sababu ya Rais Kikwete na Bunge[/h]
  Sababu ya hali tete ya nchi na maisha ya wananchi kwenye sekta ya afya ni udhaifu wa serikali na uzembe wa bunge. Rais Jakaya Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka Steven na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro. Spika Anna Makinda aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha.
  Taifa limeingizwa kwenye hali tete katika sekta ya afya na maisha ya wananchi wanaotegemea huduma toka hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma yapo mashakani.
  Tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa serikali wa kushughulikia matokeo badala ya chanzo cha mgogoro wake na madaktari na uzembe wa bunge katika kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi kusuluhisha pandembili zinazolumbana kwa gharama ya vifo na nyingi kwa wagonjwa wasio na hatia.

  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianza ikashindwa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijaribu akashindwa, Rais Jakaya Kikwete naye akaingilia kati kuondoa udhaifu uliokuwepo naye anaelekea kushindwa; kwa kuwa wote wanashughulikia matokeo ya mgogoro badala ya chanzo.
  Chanzo cha mgogoro wa serikali na madaktari na wananchi kuhusu sekta ya afya ni bajeti finyu inayotengwa na serikali na kiasi kidogo cha fedha kinachotolewa katika sekta hii nyeti, na hivyo kushindwa kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari kwa upande mmoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kwa upande mwingine.

  Rais Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro:
  Hatua ya serikali kukimbilia mahakamani na kutumia kivuli cha mahakama kukwepa kushughulikia madai ya msingi ya madaktari ni kuendelea kushughulikia matokeo na hivyo kuendeleza migogoro na migomo.

  Hata kama serikali ikitumia vyombo vya dola kukamata au kujeruhi madaktari, inapaswa kutambua kwamba mgomo wenye madhara makubwa kwa nchi umekuwa ukiendelea chini chini kwa muda mrefu kwenye sekta ya afya nchini na kuchangia vifo vya wananchi kwa magonjwa yanayotibika kutokana na huduma mbovu na kukosekana kwa madawa na vifaa tiba katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma.

  Rais Kikwete anapaswa kujitokeza na kutoa ahadi ya kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuongeza fedha za bajeti ya afya katika mwaka wa fedha 2012/2013 kupitia mkutano wa nane wa bunge unaoendelea hivi sasa ili kushughulikia chanzo badala ya kupanua wigo wa migogoro katika taifa.
  Aidha, Rais Kikwete anapaswa kutumia nguvu zake za ukuu wa nchi na uamiri jeshi mkuu kulaani tukio la kutekwa, kuteswa na kutaka kuuwawa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dr. Ulimboka Stephen ambapo baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa vyombo vya dola wanatuhumiwa kuhusika. Ili kurejesha imani juu ya Serikali na vyombo vyake badala ya kutegemea jopo la wapepelezi kutoka jeshi la polisi pekee ambalo nalo baadhi ya vituo vyake Jijini Dar es salaam vimetuhumiwa, Rais Kikwete aunde tume huru ya kuchunguza tukio husika ambalo limeongeza madoa kwa nchi kitaifa na kimataifa.

  Spika aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha:
  Kwa kipindi cha takribani miezi minne nimetumia njia za kibunge kutaka suala la madai ya madaktari lijadiliwe bungeni ili kushughulikia chanzo badala ya matokeo hata hivyo hitaji hilo la kikatiba limekuwa likipuuzwa na kusababisha bunge lizembee kuchukua hatua kwa wakati kuepusha mgogoro na mgomo.

  Izingatiwe kwamba katiba ya nchi ibara ya 63 (2) inatamka kwamba "Sehemu ya pili ya bunge (yaani wabunge) ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba".
  Nawaomba wananchi wa Tanzania waliotutuma kuwawakilisha kumtaka Spika Makinda na wabunge wote kuwajibika kujadili bungeni hali tete ya sekta ya afya nchini na kauli tata za serikali katika kushughulikia hali hiyo. Spika, uongozi wa bunge na wabunge kwa pamoja tutakiwe kukataa visingizio vya serikali vya kutumia mahakama kuathiri haki, kinga na madaraka ya bunge ya kuisimamia serikali juu ya suala la madaktari na hali ya sekta ya afya nchini.

  Hivyo; wabunge, umma na wadau wa haki za binadamu tuungane pamoja kutaka Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyoshughulikia suala la madai ya madaktari itolewe bungeni na hadharani na bunge liruhusiwe kutumia mamlaka yake ya kuisimamia serikali kujadili taarifa hiyo na kupitisha maazimio maalum ya kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea na pia kuboresha hali ya huduma katika hospitali, vituo vya afya na zahanati inayoendelea kutetereka.
  Kanuni ya 64 (1) (c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayoelekeza kwamba "Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika bunge, mbunge hatazungumzia jambo lolote ambalo linasubiri uamuzi wa mahakama"; inatumiwa vibaya na serikali kuficha udhaifu na kudhibiti mamlaka ya bunge kwa kisingizio cha mahakama.

  Hata hivyo, zipo njia zaidi ya nne ambazo umma unaweza kutaka spika na wabunge wazitumie kukwepa bunge kuonekana linazembea kuchukua hatua za kuisimamia serikali na kuokoa maisha ya wananchi katika hatua hii ya dharura.

  Mosi, hoja inaweza kutolewa ya kutengua kanuni husika kuliwezesha bunge kujadili Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu madai ya madaktari kwa kuwa imekuwa kawaida kwa serikali kutoa hoja za kutengua kanuni wakati mwingine kuilinda serikali na kupunguza madaraka ya bunge. Mathalani, kanuni ya 94 inayolitaka bunge kukaa mwezi Februari kama Kamati ya Mipango kutoa mapendekezo ya mpango wa taifa, ilitenguliwa na matokeo yake ni kuwa serikali iliandaa bajeti ikiwemo ya sekta ya afya na kuwasilisha mwezi Juni bajeti ya serikali isiyozingatia kwa ukamilifu mpango na madai ya madaktari.

  Pili, Spika anaweza kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni 114 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kutaka kamati husika ya bunge kukutana kwa dharura na kuishauri wa haraka serikali kufuta kesi iliyoko mahakama kuu kitengo cha kazi ili kulipa fursa bunge kutumia madaraka yake ya kikatiba kujadili na kupitisha maazimio ya kuweza kusuluhisha pandembili za mgogoro badala ya mahakama. Uamuzi wa kurejea mahakamani unapaswa kuwa wa mwisho baada ya hatua zingine kushindikana.

  Tatu; Spika kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni ya 114 (17) na 116 kuitaka Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kupatiwa na kupitia nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, na kuandaa taarifa maalum ya masuala yanayoweza kujadiliwa bungeni bila kuingilia suala lililo mahakamani. Izingatiwe kwamba Serikali imefungua kesi dhidi ya Chama Cha Madaktari (MAT) na haijafungua kesi dhidi ya Jumuiya ya Madaktari na Taasisi zingine katika sekta ya afya; hivyo kufunguliwa kwa kesi hiyo hakuwezi kulizuia bunge kujadili masuala mengine yanayohusu madaktari na sekta ya afya nchini.

  Nne; Kanuni ya 53 (2) au 47 (1) za Kanuni za Kudumu za bunge inaweza kutumiwa kwa Waziri husika kwamba suala la namna ambavyo serikali imejipanga kutoa huduma katika hospitali kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea au mbunge yoyote kutoa hoja kuhusu hali kwa sasa ilivyo katika hospitali na sekta ya afya kwa ujumla kufuatia kuendelea kwa mgogoro kati ya serikali na madaktari na masuala hayo yakajadiliwe. Izingatiwe masuala hayo hayahusu mgogoro ulioko mahakamani bali ni ya dharura kwa ajili ya kuepusha madhara zaidi kwa wananchi na nchi kwa ujumla wakati taifa likisubiri taratibu za mahakama kukamilika.

  Ni muhimu umma ukapuuza taarifa isiyokuwa ya kweli iliyotolewa na Naibu Spika Job Ndugai bungeni tarehe 27 Juni 2012 ya kudai kwa tayari kamati ya huduma za jamii imewasilisha taarifa yake bungeni wakati ambapo taarifa hiyo iliyohusisha kazi ya kubwa ya kamati na matumizi ya ziada ya fedha za wananchi imefanywa kuwa siri hata kwetu wabunge. Naibu Spika Ndugai kwa kauli hiyo amekwepa kutekeleza muongozo wake mwenyewe alioutoa katika mkutano wa sita wa bunge mwezi Februari mwaka 2012 kwamba baada ya kamati kumaliza kazi yake taarifa ingewasilishwa bungeni na kujadiliwa. Tayari nilishamuandikia barua Spika tarehe 27 Juni 2012 kupuuza maelezo hayo ya Naibu Spika na kutoa kwa wabunge na bunge taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii ili wabunge tusiendelee kupokea kauli za upande mmoja wa serikali bila kuwa na maelezo na vielezo vya upande wa pili wa madaktari.

  John Mnyika (Mb)
  Bungeni-Dodoma
  28/06/2012
   
 12. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mgomo sio mzuri lakini una faida zake.
  Ninakubaliana nawe kuwa mishahara ya sekta nyinginezo ni midogo sana. Ingawa wana unafuu wa kusafiri hapa na pale kutoa huduma au kuhudhuria vikao na kuongeza vipato (ukiacha wale wa masijala).Hiyo mishahara ya madaktari inaziba hilo pengo.

  Sijasikia kama serikali ilikuwa imetoa mwisho wa kutatua madai ya madaktari ikiwemo kuboresha huduma katika hospitali zetu. Sasa wewe ndugu yetu hiyo august umeitoa wapi? Kama kweli je, bajeti ya wizara imelenga kutatua hayo matatizo? Jinsi ulivyoandika unaonekana kama mtu wa hiyo wizara au magamba au mwenye uwezo wa kutuletea taarifa hapa, tupe bajeti na mchanganuo wa wizara ya afya tuone watatatua vipi?

  Mimi naamini hii ndio njia sahihi ya kuleta mabadiliko. Tuna bahati nchi yetu ilipata uhuru bila kumwaga damu lakini nchi nyingi za afrika na asia kama korea ilikuwa hivyo. Tukiweza kuwa pamoja na madaktari na kumuomba Mungu zaidi basi huu ndio mwanzo wa mabadiliko.

  Kama unaona mshahara wa sekta yako mdogo au mambo hayaendi tafuteni suluhisho kwasababu hii nchi ina hela sana huko uswis, nyingine tunataka kuwajengea ofisi wabunge mambumbu na dhaifu, nyingine tumewaachia watu wa madini na nishati n.k. wakati wakulima wanalalamika bei za mazao, mbolea, kutolipwa fedha zao na wastaafu hivyohivyo. Ukienda hospitali dawa hakuna, akina mama au wagonjwa wengi hulala watatu watatu. Hivyo usilete maneno yako tuungane na madaktari na nyie TUCTA na waalimu, wakulima wanaonyanyasika kuondoa udhalimu wa serikali kwa ajilli ya kizazi chetu cha baadae.

  Bora mateso haya ya wiki mbili kuliko tukiacha hali hii tukaishi nayo kwa miaka 10-20. Kwasababu vifo vitakuwa vingi zaidi ya tunavyoviona sasa na huduma ya afya itakuwa ghali sana kuliko sasa kama hayatatatuliwa. EEE Mola tuepushie janga hili.
   
 13. m

  mbagalakigoma Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raisi wako ye anafanya nin??? Naskia Leo Kaenda bagamoyo..... Wewe umefanya nin kuokoa hao wanaokufa?? Seri Ali ni sis
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  wakuziba.....! nimekusoma kwa sehemu.... TAASISI YA HAKI ZA BINADAMU...INATETEA UHAI WA MTU MMOJA. .......ila uhai wa watu wengi ambao hawana influence hasa kwenye media wamenyamaza kimya......! two wrongs do not make one RIGHT
   
 15. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Laani serikali yako kwanza!!. Watanzania hatuna shukurani, yani we unaogopa kufa wakati daktari hayupo, lakini huogopi kufa madawa na vifaa vya kazi mahospitalini kama havipo. Hao madaktari wanafanya vipi kazi zao kama hawawezeshi. Akili za watu wengine sifuri kabisa. Ndio mnavyotumika kudanganya umma namna hiyo. Watanzania sasa hawadanganyiki kwa taarifa yako. Mngekuwa mnalaani serikali yenu kupeleka viongozi wake matibabu India halafu nyie hamna hata vitanda vya kulala mahosipitalini. Pumb.....vu
   
 16. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeangalia mita 1 lakini Taasis ya Haki za Binadamu wameangalia mita 500
   
 17. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Shortsitedness! Mwisho wa pua ndio mwisho wako wa kufikiri! Au na ww ni among wanaoendaga india kutibiwa? Poor you!
   
 18. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,244
  Trophy Points: 280
  hao wabunge wanahaki gan kulipwa hayo mafweza?
   
 19. A

  Aswel Senior Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  siungi mkono hoja madaktari acha waendelee kudai stahiki zao bwana na wao wanahaki ya kudai, mzee wa magogoni inabidi awatimizie stahiki zao then tuone kama watagoma tena, hapa wa kulaumiwa ni serikali iliyoko madarakani
   
 20. a

  abousalah2 Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asiyemrehemu mwenzake hawezi kurehemewa na m/ mungu. Nina wasi wasi kuwa wote wawili wanogoma na wanaogomewa! Wanawezekana wamelaaniwa!
   
Loading...