Mungu atuepushe na pepo la kuspend na mtu huku tukijua kabisa kwamba ni wa muda mfupi tu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,339
2,000
Wanabodi,naenda moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu!

Baina yetu, ni kawaida sana kumuagiza mwanamke /mwanaume kutoka mtaa au mkoa mwingine kwa ajili ya kuspend /kutembea nae huku moyoni ukijua kabisa kwamba huwezi kuishi nae, yaani ni wa muda tu au 'short time kama ambavyo tumezoea kusema. Wakati huo ukijua fika kabisa kwamba una mtoto /watoto/ familia au ndugu ambao wangeweza kufaidika na hela hiyo unayofuja kwa huo "upuuzi/umalaya" wako unaoufanya.

Wanaume ndo wamekuwa vinara wa kuagiza wanawake /wake za watu yaani kwa jina lingine wanaume ni "waagizaji" na wanawake ndo "waagizwaji". Unakuta mmoja au wote wawili wana familia na ndoa zao halali kabisa mbele za MUNGU na Serikali. Hii ni laana.

Kuna risks au athari/risks nyingi sana zinazohusiana na kuchepuka au kuwa na mchepuko hasa kuagizana Wilaya kwa Wilaya, Mkoa kwa Mkoa na hata tu Mtaa kwa Mtaa. Boda boda umekuwa usafiri muhimu sana unaotumiwa na wachepukaji wa Mtaa kwa Mtaa kwa sababu bodaboda ni rahisi kupenya uchochoroni na pia ni rahisi kumkimbia anayekufukuza kwa gari au miguu. Vijana wa boda boda wako connected sana na hizi mambo. Hii ni laana.

Kupata ajali njiani ukiufuata mchepuko wako, kufariki guest , kuuawa kwa fumanizi, kuambukizwa magonjwa au gonjwa la zinaa, kupoteza fedha kipuuzi na laani ni baadhi ya risks ambazo huwakumba wachepukaji. Huwezi kukoswakoswa kwenye hizo. Hii ni laana.

Mke wa mtu ndani ya familia anamuaga mume wake kwamba anaenda kumsalimia shoga yake mtaani wa pili, kumbe anaenda "kudinywa" na kijana wa mtaani ambaye yupoyupo tu Au anaenda kugongwa na mwanaume ambaye anajua au hajui kwamba ni mume wa mtu. Na wakati huo huo akijua kabisa kwamba anaenda kwa "short time" tu, yaani kufanya sex na kurudi nyumbani kwa mume wake. Wakati mume wake yupo na "dude" analo. Hii ni laana.

Mwanaume unamdanganya mtoto wa watu au mke wa my kuwa hujaoa, baadae umamtumia nauli anatoka Dsm anakufuata Arusha mnakula bata na kupoteza fedha nyingi huku mke wako na watoto wakijua baba amesafiri kikazi. Hii ni laana.

Kwanini uwe na mchepuko? Mkeo / mumeo hakutoshi?

Kwann umapoteza fedha nyingi kwakuwa na mchepuko?

Kwanini unajiweka kwenye risk nyingi kwa kuwa na mchepuko?

MUNGU atuepushe na tabia hii ya kipumbavu katika maisha.
 

james bendui

JF-Expert Member
Dec 3, 2015
437
500
Yn hii mada imenigusaa japo sijaowa ila kuna binti ananisumbua jap tup kwen mahusianoo ilaa nampend kushinda maelezo na fik najuaa sitamuowaa nanakuwa mkalii sn kwa makosa yk sijui sijitambuii au nn kimo kichwani kila nikijarib ni ngumu kutok mpk marafiki zangu wananiambia lkn bd nimemngangania na bd nipo naee
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,079
2,000
Yn hii mada imenigusaa japo sijaowa ila kuna binti ananisumbua jap tup kwen mahusianoo ilaa nampend kushinda maelezo na fik najuaa sitamuowaa nanakuwa mkalii sn kwa makosa yk sijui sijitambuii au nn kimo kichwani kila nikijarib ni ngumu kutok mpk marafiki zangu wananiambia lkn bd nimemngangania na bd nipo naee
Angalia mkuu asije akakuchuna hizo million 28 ulizoomba ushauri kule kwenye Uzi wako
 

aker2011

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
687
1,000
Nina mpango wa kuagiza kutoka dar(npo mkoani) kwa hili bandiko ngoja niwatumie wazee hii pesa itawasaidia sana! Ubarikiwe sana hivi punde
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,543
2,000
Nilikuwa mbioni kumuagiza Mary Mwakibb aje kutoka Mbeya ila nishaahirisha kwa bandiko lako
 

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,410
2,000
Ifike mahala tuache kupangiana matumizi!
Pesa zake alitafuta kwa jasho lake iweje usikitike yeye anavyozitumia?

Mtu kama anafanya jambo na aharibu maisha yako kwa njia yoyote ile basi mwache.
 

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,085
2,000
Baada tu ya kuimport, na kufanya starehe zote, ukimaliza tu hela unapata simu kutoka nyumbani kwamba mama anaumwa na hela inatakiwa.

Hapo umeshamaliza hela zote. Unakuja kugundua kumbe ile hela Mungu alikupa umtibu mama na sio kufanya starehe.
 

Bervy

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
6,694
2,000
Umesahau wanaoagiza masafa marefu......masaa tisa na zaidi kwenye ndege kwa starehe ya weekend....
Pesa kitu kingine. ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom