Mungu Ashukuriwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu Ashukuriwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lord, May 5, 2010.

 1. Lord

  Lord Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna wakati nawaza nini hatma ya Tanzania hii lakini baada ya muda namshukuru mungu kwa yote aliyotupatia. Inawezekana vipi kwa nchi nzuri kama hii mungu aliyoijalia kila aina ya vitu vya kipekee kama tanzanite, dhahabu, almasi, ruby, saphire, silver, wanyama wa kipekee, mito mizuri na maporomoko ya kipekee pamoja na ardhi safi ya kutupatia chakula ashindwe kutupatia viongozi safi na wenye maono?? Kipindi nipo nasoma nilipata kusikia usemi ili nchi iendelee tunahitaji ardhi, siasa safi na uongozi thabiti. Nikawa nawaza uongozi dhabiti inakuwaje???? Si mtu akifikia hatua mpaka aamue kugombea uongozi ameshajipima akajiona ni kiongozi thabiti??? Au kuna la ziada??
  Sasa naelewa dhana nzima ya kiongozi thabiti. Kiongozi thabiti si wa ku copy na ku paste. Kiongozi thabiti si kama kasuku ambaye hulirudia kila neno analoambiwa japo kuwa mengine si maneno ya maana. Ni heri kuwa kong'ota kuliko kuwa kasuku mropokaji. Mwajiri mkuu ni sawa na kasuku ambaye "huropoka" kila jambo analoambiwa bila kujua maana yake. Ni aibu kwa mkubwa kama yeye leo hii watu kugundua kwa mara nyingine tena amepotoshwa. Barua ya TUCTA ni ushahidi tosha kwamba nchi haina viongozi imara. Inadhihirisha kwamba kwa namna ya uongozi tulionao maendeleo ni ndoto la maana tumshukuru mungu mpaka atakapotupatia taifa lenye viongozi wakati huo ardhi yenye kila aina ya baraka ikiwa hatunayo na ndipo tutakapoendelea na matatizo yetu yale yale.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  hivi mkuu ina barua ya tukta hapo?
  naomba kama unayo itupe hapa janvini tafadhali
   
Loading...