Mungu anajibu maombi,shemeji yenu kanichumbia

Amani ya Mungu na iwe juu yenu wapendwa wangu.

Najua nimepotea machon mwenu kwa kitambo sasa,lkn sikua na tatizo lolote ni michakato tu ya kimaisha ndo ilifanya nikose muda wakuwa nanyi wapendwa wangu.
Hapa nilipo nina furaha ya ajabu,ni muda mrefu sijawahi kuwa na furaha ya kiwango cha juu namna hii.Shemeji yenu nimpendae kuliko kitu chochote hapa duniani amenifanya the happiest woman alive kwa kunivalisha pete ya uchumba.Huyu shem wenu kuna kipindi nilidhan ananipotezea muda maana kila nilikua nikimtajia mambo ya ndoa alionekana hayuko tayari.Baada ya kusubiri sana nikaamua kufunga kwa MAOMBI,nikasema Mungu kama huyu kijana siye uliyeniandalia naomba umfanye aniache nisonge mbele asinipotezee muda ila kama ndiye uliyenipangia basi naomba unipe ishara kwa yeye kunivalisha pete bila ya mim kumwambia wala kuongea lolote lenye kuhusiana na ndoa.Kwa kweli Mungu wangu is the most highest God,no one like him,i will always serve him.Ndugu zangu lengo la kuandika hapa,sio tu kuwashirikisha furaha yangu bali pia ni kuwashuhudia kwamba tumshirikishe Mungu kwenye mambo yetu yote,maana hekima zake si kama zetu.

Ashadii niandalie kitchen party.


Hongera
 
Kwa kweli hiyo furaha yako ni ya uhakika, ila ninalo swali kidogo; huyo shem wetu uliwahi kufanya naye mambo ya kikubwa???????? Maana unasema mmejuana siku nyingi kivipi??? Kama ni hivyo mtabidi mtubie dhambi zenu kwanza kabla ya kumshirikisha Mungu kwenye mipango yenu ya ndoa. Msirudie tena kukutana kimwili hadi harusi!!!!!!!!! Bila shaka mmenielewa!!!!!!!!!

sawa mtumishi,umeeleweka vizuri kabisa,ubarikiwe.
 
ni kweli BE hata mie nimeshashahudia mauchumba mengi yakivunjika,lkn huu wa kwangu umesimikwa kwa damu ya Yesu,Hautavunjika hata kwa kifo,maana mim na mume wangu tukifa ktk mwili tutakutana tena mbinguni kwa baba.Mungu apewe sifa maana anastahili.

Hongera Sana Cheusimangala

Hapo bold umenikumbusha Wimbo wa Tenzi za Rohoni: Watakatifu twonane mtoni...

Cha Msingi mdogo wangu Cheusi ni UPENDO:


"... Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika..." 1 Wakorintho 13:-
 
Hongera sana cheupe,...ops cheusiManga,...
Usisahau hata stage moja ya maisha yako kumshirikisha Mungu,...

Nasubiria majibu kabla ya kwenda kupima na wifi yako mwezi ujao so
i hope ntatoa pete soon pia
(mmh,natetemeka balaa hapa)

asante mkuu,hongera kwa hatua unayokaribia kufannya.Mungu akutangulie.usitetemeka kupima ndo ujanja wenyewe.
 
Hahaha!!! Kwahiyo wewe utakuwa bestman kwenye harusi ya cheusimangala halafu yeye atakuwa matron wa Hus kwenye harusi yako hapo ngoma droo lol!!!

uporoto ni mwanaume anaweza kujikaza akawa best manmlkn mm kuwa matron wa Hus,inabidi niandaliwe vizuri kisaikolojia maana naweza kujikuta natoa kipingamizi ndoa isifungwe pale mch. atakapouliza kama kuna mwenye kipingamizi.mm na uporoto tumetoka mbali sema tu hakuiona dhamani yangu hadi sasa wengine wamenichukua ndo anaona almas aliyoipoteza LOL
 
Hongera Sana Cheusimangala

Hapo bold umenikumbusha Wimbo wa Tenzi za Rohoni: Watakatifu twonane mtoni...

Cha Msingi mdogo wangu Cheusi ni UPENDO:


"... Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika..." 1 Wakorintho 13:-


Baba E ni wewe? gosh!....Cheusimangala hii ndoa yako itadumu milele...Amen.
 
Hapa sasa cheusimangala hommie wangu Fidel kwa statement hii ngoja nimsubiri nione atajibu nini lol!!!

uzuri wa fidel ukimpa ofa,hakomoi.ila safari hii anaruhusiwa hata akitaka kukumoa,niko kwenye pozi la furaha,chochote ntatoa.
 
Hongera sana dada, safari ndiyo imeanza sasa kama nikuomba omba zaidi ya vile ulivyoomba mpaka kufikia hatua ya kukuvisha pete. Inaonekana maombi ndiyo catalyst ya kumfanya kukuvika pete. Ukipunguza tu! urudi hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom