Mungu amenisikia. Sasa Magufuli bingwa wa mitandao ya kijamii

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Nilishtuka sana kusikia Rais Magufuli akisema kuwa anatamani siku moja mitandao ya kijamaa isiwepo Tanzania (duniani?). Alisema hivyo kwa kuwa aliamini inamzuia kufanya kazi zake za kuinyoosha nchi.

Kwa kauli yake, nilifunga na kuomba kwa siku 40 ili Mungu asisikie kilio chake. Nashukuru Mungu wangu ni mwaminifu na hakumsikiliza.

Pamoja na kutomsikiliza, alimpa nafasi ya kujitafakari na sasa amegundua kuwa mitandao ya kijamii, hasa Twitter na Jamii Forums ni muhimu sana kwake. Inamsaidia kupata habari, maoni ya wananchi wake na zaidi sana anaitumia kuwasiliana.

Ona sasa, kwa kutumia Twitter ameweza kuwasiliana na dunia, hasa wananchi wa Zimbabwe kuwapa pole kwa kifo cha Morgan Tsvangirai. Kama siyo njia hiyo ya mtandao wa kijamii, ingemlazimu kumoigia simu tu Rais wa Zimbabwe nasi tusingejua, labda kwa kuambiwa na kina Msigwa.

Nasema tena, aksante Mungu kwa kumpa Rais wangu Magufuli fursa ya kutambua umuhimu wa mitandao ya kijamii.
 
Atambue na umuhimu wa watu kutoka upinzani asitumie pesa Kuwanunua hajengi anabomoa demokrasia...
Atambue pia yeye sio malaika akubali akosolewe afanye marekebisho..
Atambue pia kuna maisha baada ya urais
Ushahidi please
 
Back
Top Bottom