Mungu alivyomjibu mtesi wa Oliver N'Goma, dikteka Omary Bongo

Kuna watu roho mbaya Sana wakipata madaraka wanajiona Miungu kumbe haya maisha tunayo kwa muda tu then yanapita ila kwakweli Oliver alipitia kipindi kigumu mno mtu kukosa haki yake kikatiba isitoshe matibabu yalikuwa ni kwa faranga yake it's too much terrible
Na izi ni roho za kiafrica... Tuna roho mbaya kinoma!!!! Na wakati huo huo ukute na ngoma za jamaa alikuwa anasikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I see, just imagine unamuwekea vikwazo mtu asipate tiba ili afe, nawewe uendelee kutawala.
Baadhi ya viongozi wa Africa ni matatitizo kuliko matatizo yenyewe.
Viongozi wa aina hii wanaididimiza Afrika.
 
Hayo aliyafanya huyo Mungu? Duh huyo Mungu wa visasi na kuonyeshana ubabe mbona kama tumekwisha sasa.

Sasa badala ya kumuonyesha muhitaji figo kwa kumuweka hai ili aone watesi wake wakifa si angemtengenezea figo mpya?
Mungu wa Oliver alikuwa na uwezo. Wa kuuwa tu na si kuponya
 
kumbe mfalme wa zuku kifo chake kilitokana na kunyimwa kusafiri kwa ajili ya kupata matibabu. Walaaniwe familia ya kina Bongo wapumbavu sana jinga kabisa
 
Viongozi wa Africa wanaviburi sana. Huwa wanajiona wao na MUNGU ni sawa.

Nachukia sana mtu ambaye ana hisi ana power ya kuamua hatima ya mwingine au maisha ya mwingine. Huwa nachukia sana watu wanaohisi wao wananguvu na mamlaka juu ya wengine.

Mbona amekufa sasa kama alijihisi yeye ni kidume kuzuia mwenzake asipatiwe matibabu?! Fala sana huyo Bongo.
 
Sawa
 
Mwaka 2008 nguli wa Zouk barani Afrika, Oliver Ngoma aliugua figo na alihitaji matibabu nje ya nchi. Lakini aliwekewa zuio la kusafiri nje. Serikali ya Rais Omary Bongo ilimtuhumu Oliver kwamba anaandaliwa na mataifa ya Ulaya kuwa Rais wa Gabon.

Japo Oliver alikanusha madai hayo lakini hakuaminika. Wakati huo kulikua na wimbi la wanamuziki na wanamichezo kujiingiza ktk siasa. Mkongwe Youssou N'Dour alitangaza kugombea Urais Senegal. Oliver alitarajiwa kugombea Gabon. Alihofiwa kwa sababu alikua kwenye kilele cha mafanikio. Alifanya kazi na record label kubwa na nyimbo zake zilishika chati za juu barani Ulaya, Amerika, Carebean, Afrika na nchi za Asia.

Jarida la Vogue Paris liliutaja wimbo wa Bane, wa Oliver, Yekeyeke wa Mory Kante na Mario wa Franco kwamba ndizo nyimbo 3 za Afrika zilizochezwa zaidi barani Ulaya.

Album ya Bane yenye nyimbo kama Bane, Alphoncine na Lusa iliuza nakala milioni 2 kabla ya mwaka mmoja na kuwa "best-selling African album" rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Akaunti zake nchini Gabon zilikua na ukwasi wa $1M.

Mafanikio hayo yalimtisha Bongo na kuona njia rahisi ya kumdhibiti ni kumuwekea kizuizi cha kusafiri. Pia alizuiwa kuingiza pesa kutoka nje. Inadaiwa Oliver alikua na pesa nyingi Paris kuliko alizokua nazo Gabon. Rais Bongo aliamini Oliver alipewa pesa hizo na "mabeberu" kama njia ya kumuandaa kugombea Urais wa Gabon.

Mwaka 2008 alipougua alilazimishwa kutibiwa kwenye hospitali ya umma. Alitakiwa kupandikizwa figo lakini hospitali hiyo haikua na uwezo huo. Aliomba rufaa kwenda Paris, lakini serikali ilikataa.

Dikteta Bongo alitaka Oliver akose matibabu afe. Lakini njia za Mungu hazichunguziki. Tar.14 March 2009 mke wa Bongo (Edith) alifariki huko Rabat Morocco. Siku chache baadae Bongo akabainika kuwa na saratani na June 08 mwaka huohuo akafariki.

Mwanae (Ali Bongo) akashika madaraka baada ya kifo cha baba yake, lakini bado alimnyima Oliver haki yake ya kutibiwa nje. Oliver aliendelea kupigania maisha yake kitandani nchini Gabon na hatimaye 07 June 2010 alifariki dunia. Lakini kabla ya kifo chake alimshuhudia mtesi wake (Dikteta Omary Bongo) na mkewe wakitangulia kaburini.

Umejifunza nini?

RIP Mfalme wa Zouk. Huyu mwamba alikuwa na ubunifu wa pekee kabisa katika kukuza soko la aina ya muziki aliokuwa anaupiga. Miaka ile ya mwanzoni mwa 90's soukouss ikiwa ndio inashika kasi ya ajabu, hakufanya ajizi. Katika albam yake ya Bane kuna nyimbo mbili za Lusa na Mayumba ambazo alifanya mchanyato wa Zouk na Soukous. Aliwaleta wanamuziki mashuhuri sana akiwamo Dally Ndala Kimoko(Soloist), Lokassa ya Mbongo(Rythym) na Ngouma Shungu Omba Lokito(base guitar). Hawa walitenda haki ya hali ya juu katika nyimbo hizi mbili.

RIP Oliver N'goma.
 
Mwaka 2008 nguli wa Zouk barani Afrika, Oliver Ngoma aliugua figo na alihitaji matibabu nje ya nchi. Lakini aliwekewa zuio la kusafiri nje. Serikali ya Rais Omary Bongo ilimtuhumu Oliver kwamba anaandaliwa na mataifa ya Ulaya kuwa Rais wa Gabon.

Japo Oliver alikanusha madai hayo lakini hakuaminika. Wakati huo kulikua na wimbi la wanamuziki na wanamichezo kujiingiza ktk siasa. Mkongwe Youssou N'Dour alitangaza kugombea Urais Senegal. Oliver alitarajiwa kugombea Gabon. Alihofiwa kwa sababu alikua kwenye kilele cha mafanikio. Alifanya kazi na record label kubwa na nyimbo zake zilishika chati za juu barani Ulaya, Amerika, Carebean, Afrika na nchi za Asia.

Jarida la Vogue Paris liliutaja wimbo wa Bane, wa Oliver, Yekeyeke wa Mory Kante na Mario wa Franco kwamba ndizo nyimbo 3 za Afrika zilizochezwa zaidi barani Ulaya.

Album ya Bane yenye nyimbo kama Bane, Alphoncine na Lusa iliuza nakala milioni 2 kabla ya mwaka mmoja na kuwa "best-selling African album" rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Akaunti zake nchini Gabon zilikua na ukwasi wa $1M.

Mafanikio hayo yalimtisha Bongo na kuona njia rahisi ya kumdhibiti ni kumuwekea kizuizi cha kusafiri. Pia alizuiwa kuingiza pesa kutoka nje. Inadaiwa Oliver alikua na pesa nyingi Paris kuliko alizokua nazo Gabon. Rais Bongo aliamini Oliver alipewa pesa hizo na "mabeberu" kama njia ya kumuandaa kugombea Urais wa Gabon.

Mwaka 2008 alipougua alilazimishwa kutibiwa kwenye hospitali ya umma. Alitakiwa kupandikizwa figo lakini hospitali hiyo haikua na uwezo huo. Aliomba rufaa kwenda Paris, lakini serikali ilikataa.

Dikteta Bongo alitaka Oliver akose matibabu afe. Lakini njia za Mungu hazichunguziki. Tar.14 March 2009 mke wa Bongo (Edith) alifariki huko Rabat Morocco. Siku chache baadae Bongo akabainika kuwa na saratani na June 08 mwaka huohuo akafariki.

Mwanae (Ali Bongo) akashika madaraka baada ya kifo cha baba yake, lakini bado alimnyima Oliver haki yake ya kutibiwa nje. Oliver aliendelea kupigania maisha yake kitandani nchini Gabon na hatimaye 07 June 2010 alifariki dunia. Lakini kabla ya kifo chake alimshuhudia mtesi wake (Dikteta Omary Bongo) na mkewe wakitangulia kaburini.

Umejifunza nini?

Mungu ni Fundi na Mungu hadhihakiwi
 
Namkubali sana mkali wa zouk oliver ngoma... Nimefarijika kupata historia ya kifo chake japo inaumiza..... Lakini jamaa ana ngoma tamu sana walahi kuna ngoma yake inaitwa Nge ni hatari nina flash ina nyimbo za uyu jamaa tu... Na napenda kusikiliza nikiwa nasafiri kwenye gari yangu R.I.P Oliver

Sent using Jamii Forums mobile app

Back
Top Bottom