Mungu aliruhusu Polepole aingie Segerea na msafara wake kwasababu alijua binadamu walipanga kufanya nini baadae kwa wafuasi wa CHADEMA hapo Segerea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Naomba nianze kwa kusema maneno haya ninayoyaamini mimi kama mimi:

"CHADEMA kwa watanzania ni mpango wa Mungu kama alivyokuwa Mussa kwa wana wa Israel".

Nimeanza na maneno hayo kuwatahadharisha wale wote wanaofikiri wanapambana na CHADEMA kumbe wanapambana na nguvu za Mungu anaeitumia CHADEMA kuwakomboa watanzania kutoka katika tawala za CCM.

Ukweli huu ni sababu kwanini hata ile kauli ya JK kuwa vyama vya upinzani(akiilenga CHADEMA) kuwa ni vyama vya msimu ilikuifa kifo cha Mende na hata huyu wa sasa anaetuhumiwa kutaka kuua upinzani na ususa CHADEMA, atafeli na huenda akaja kujikuta anawakabidhi ofisi.

Na kwa msingi huo huo wa CHADEMA kuwa ni mpango wa Mungu, ndio maana Mungu aliruhusu Polepole aingie pale Segerea na msafara wake kwani alijuia ni nini kingetokea baada ya pale ili Dunia ione doublestandard ya vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama.

Si hivyo tu,hata mtu kutamka kuwa tunatumia dola kubaki madarakani ni mpango wa Mungu kuwaumbua hawa watu na ndio maana kauli ile kwa sasa ni kama inatekelezwa kwa vitendo(Mungu kawanyima maarifa ili waumbuke na hatimae waanguke).

Mnaofikiri CHADEMA itakufa kwa kuhujumiwa kwa miaka karibu mitano sasa,mjue mtaishia kuumbuka hasa pale mtapokuja kushuhudia CHADEMA inakamata dola na Mungu atawaweka hai ili mje mshuhudie jambo hili likitimia.

Narudia,CHADEMA ni chama teule na ndio maana hakiyumbi,hakifi na zaid ndio maana wale wotei wanaotaka kukihujumu wao ndio kila siku wanaumbuka kwa kauli na matendo yao wenyewe.

Haya mnayoshuhudia leo Mungu kayuruhusu akiwa na makusudi yake na hawa kina Lissu,Mbowe,Mdee,Heche,Msigwa na wengineo wameteuliwa tu kutumika kukamilisha mipango ya Mungu ambayo sisi binadamu hatuwezi kuitambua kwa sasa.
1584342093273.png

1584342568391.png

1584342675990.png

1584342805152.png
 
Yaani hili tukio linazidi kuanika huu uhayawani wanaofanyiwa cdm kwa matumizi mabaya ya madaraka. Polepole kaenda magereza na makamera, wakati hairuhusiwi kupiga picha huko gerezani lakini kaachwa, huku yeye sio mwanacdm na huyo Msigwa aliyemfuata sio mwanaccm. Lakini wanacdm kumfuata mwanacdm mwenzao imegeuka wameenda kufanya fujo! Kama cdm walihitaji kufanya fujo, mbona hawakufanya siku zote kesi ikiendelea, au siku waliohukumiwa, hadi wangoje wakiwa wamelipa kiongozi wao wa mwisho kutoka ndio wafanye fujo? Hapo kuna mtu atashindwa kuona ukweli wa yale maneno kuwa ccm itatumia dola kubaki madarakani?
 
"Tulipofika Gereza la Segerea hatukuruhusiwa kuingia ndani, Askari Magereza walitufukuza kwa maneno ya matusi, kashfa na kutuambia kuwa 'walikuwa wametupania sana hasa mimi na Halima Mdee, kwamba tuliwahi kuondoka na walipanga kututesa sana'"
 
Yaani hili tukio linazidi kuanika huu uhayawani wanaofanyiwa cdm kwa matumizi mabaya ya madaraka. Polepole kaenda magereza na makamera, wakati hairuhusiwi kupiga picha huko gerezani lakini kaachwa, huku yeye sio mwanacdm na huyo Msigwa aliyemfuata sio mwanaccm. Lakini wanacdm kumfuata mwanacdm mwenzao imegeuka wameenda kufanya fujo! Kama cdm walihitaji kufanya fujo, mbona hawakufanya siku zote kesi ikiendelea, au siku waliohukumiwa, hadi wangoje wakiwa wamelipa kiongozi wao wa mwisho kutoka ndio wafanye fujo? Hapo kuna mtu atashindwa kuona ukweli wa yale maneno kuwa ccm itatumia dola kubaki madarakani?
Duh..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom