Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
Mwanadada Maria, umeendelea kwa juhudi kubwa kuutahadharisha umma uchukue tahadhari juu ya ugonjwa wa Korona.
Tangu miezi kadhaa nyuma ambapo serikali ya awamu ya tano ilikuwa ikiutangazia ulimwengu kuwa nchini hakuna Korona, hukuchoka kuutahadharisha umma ujikinge maana kiukweli Korona nchini ipo
Wakati unapaza sauti ulikejeliwa na wana MATAGA na mashabiki maandazi wa hata mambo ya kijinga yafanywayo na watawala
Leo ugonjwa wa "changamoto za kupumua" umeanza kupiga "pabaya", Taifa limekuwa kama limezinduliwa kutoka usingizini kuwa hii kitu ipo!
Ndugu Watanzania wenzangu, Hii vita hatuiwezi mtu mmojammoja maana ni kama Mtumbwi, huwezi kuwa unaziba tobo moja halafu mwingine anatoboa kwingine!.
Bila serikali kuchukua nafasi yake na kuact responsibly kama mamlaka kuu yenye dhamana ya kuchukua hatua za kuthibiti hili janga kwa kuwashirikisha wananchi, basi Janga hili litatuacha nyang'anyang'a.
Ndiyo maana nampongeza huyu binti Sarungi kwa jitihada kubwa za kunusuru maisha ya wananchi.
Binti alifikia hatua ya kuziandikia jumuia za kimataifa barua ziokoe Wataanzania dhidi ya denial na hatua za kusuasua za serikali hii kulinda uhai wa watu wake. Kwa hakika huyu binti anastahili pongezi, Kazi zake za kutetea watu na haki zao ni kazi nzuri sana.
Namuomba asikate tamaa aendelee hivyohivyo, maana jitihada zake zinasaidia