singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAZIRI wa zamani katika serikali za awamu zilizotangulia na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa miaka 35, Joseph Mungai, amerejesha serikalini eneo la Hospitali ya Wilaya ya Mufindi analodaiwa kulihodhi kwa muda mrefu bila kuliendeleza.
Taarifa ya kurejeshwa kwa eneo hilo lililopo nyuma ya hospitali hiyo iliyopo mjini Mafinga wilayani humo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla alipotembelea hospitali hiyo juzi.
Akizungumzia mipaka ya kiwanja cha hospitali hiyo baada ya waziri huyo kutaka kujua kama haijakumbwa na uvamizi kutoka kwa wananchi, Kasunga alisema; “sehemu ya eneo la hospitali hii ilikuwa na mgogoro baada ya Mzee Mungai kudai kuimiliki kihalali.”
Mkuu huyo wa Wilaya alisema mgogoro huo ambao hata hivyo haukutajwa muda wake, umekwisha baada ya mbunge huyo mstaafu kurejesha eneo hilo mikononi mwa hospitali hiyo.
Akipokea taarifa hiyo, Dk Kigwangalla alitoa siku saba kwa uongozi wa Halmashauri ya Mafinga Mji inayosimamia hospitali hiyo kujenga uzio utakaounganisha uzio wa hospitali hiyo ili kulinda mipaka yake.
“Pamoja na kujenga uzio nataka mniletee ofisini kwangu ramani ya eneo zima la hospitali na taarifa rasmi inayoonesha mgogoro baina yenu na mvamizi huyo umemalizika. Haya ni mambo ya kisheria, isije ikawa leo mnasema mgogoro umekwisha halafu kesho tukasikia Mzee Mungai kaenda mahakamani,” alisema.
Dk Kigwangalla alizitaka halmashauri zote nchini kulinda maeneo yake kwa kuhakikisha yamesajiliwa na yana hati ili inapokuja mipango ya kuboresha au kutanua matumizi ya eneo kusiwepo na changamoto.
Akizungumzia huduma hospitali hapo, Naibu Waziri alisema; “hospitali hii ni muhimu katika eneo hilo lakini hamuipatii kipaumbele. Nimekagua na kujionea kwamba kuna maeneo yenye changamoto nyingi, Mfano ni vyumba vya vya upasuaji. Nyie mnaona kama mnavyo lakini kiukweli ni kama hamna kwani vilivyopo vinafanana na stoo, kitu ambacho sio kipimo chake.”
Alisema changamoto nyingine katika vyumba hivyo ni uchakavu, havina mgawanyo wa vyumba, vinavuja, havina maji, makabati yamechoka na paa halina viwango. Alisema angetembelea hospitali hiyo kama mkaguzi angelazimika kufunga vyumba hivyo vya upasuaji visitumike kwa sababu ya upungufu wake