Elections 2010 Mungai apandishwa kizimbani kwa rushwa

Mungai mkenya..nenda kagombee kericho au naivasha kwenu....wawatoe kafara na watanzania pia....
mix with yours:embarrassed1:
 
Hivi TAKUKURU hawana kitu tunaita kwenye Audit "Materiality" Hivi kweli hivyo vipesa ambavyo hata laki moja havifiki vinajustfy kuitwa rushwa, kweli ni material kumerits kesi?. Hii sio ile takrima aliyoitetea kikwete, hivi kweli shs 10 za kitanzania zitafanya nini. Waliosoma Taxation wanajua ile principle ya cost effectiveness, kwamba gharama za kukusanya kodi lazima ziwe ndogo kuliko kodi inayokusanywa. Gharama za kuendesha kesi ya rushwa lazima ziwe ndogo kuliko madhara na faida itakayopatikana. Kwa kumshitaki Mungai serekali inafaidika na nini, afterall alishashindwa. Hiyo kesi ya laki moja itatumia resources kiasi gani za nchi hii. TAKUKURU, be serious na kesi kama hizo hazina manufaa kwa mtanzania. Na je mbona aliyepokea rushwa hajafikishwa mahakamani, nijuavyo mimi aliyetoa na aliyepokea rushwa wote wana makosa. Sijaona kama kina Kiyeyu sijui na Mdaligwa etc, waliopokea hiyo rushwa wakiunganishwa katika kosa, au walikuwa undercover agents"

Hii kesi haina merits na Mungai atashinda, nadhani ni kutapatapa kwa CCM ili kuwazuga wadanganyika, afterall Mungai alishaloose, what is he for anyways, kuloose is enough punishment. Wale waliokamatwa kwa rushwa na kushinda mbona hawajafikishwa mahakamani, hivi kweli TAKUKURU wako serious. To me Tanzania is a safer place without TAKUKURU.
Na je rushwa ni fedha (monetary) tu, hiyo sheria haibainishi rushwa nyingine kama ahadi hewa, ngono, ukabila etc. Muungwana alivyojaza washikaji wake kwenye serekali sio rushwa hiyo?-- ethics?

Mungai pole, umetumiwa kama chambo, fight to prove them wrong, TAKUKURU wanafunika uozo wa rushwa. Rushwa haichunguzwi kihivyo, eti elfu mbili, come on, now be serious. Mpiga kura akiomba shs 2000 za kununua kilo ya sukari kwa mgombea tayari ni rushwa hiyo ya kuweza kubadili matokeo?

Simtetei Mungai, but nashangaa kama kweli hizo takrima ndogo ndogo hizo zinamerits kuiingiza serekali kwenye gharama kubwa ya kuendesha kesi.

Mla rushwa anapewa pole, tutafika kweli? Madhara ya rushwa unayapima kwa kiasi cha hongo iliyotolewa au kwa kiasi cha umomoaji wa maadili hiyo rushwa inayosababisha? After all Mungai kukamatwa akitoa laki moja haimaanishi ndio rushwa pekee aliyotoa, inawezekana alitoa mamilioni lakini aliyokamatwa akitoa ni laki moja! Vilevile kuwepo kwa rushwa sehemu nyinginezo sio kigezo cha yeye kuwa mla rushwa!
 
This guy should havebeen imprisoned long time ago when he stole millions of shillings during his stint as a minister for education: hopefully God willing, he will pay for his accumulated sins!!
 
Ni sawa kumpatia mashtaka haijalishi kiasi gani katoa kama rushwa,ila cha msingi ni kuwa wanaweza kutumia kana kwamba ni kipimo kile kile kwa upinzani so kaeni chonjo wakina Regie na wezenu ,they try to play smart game here in the name of PCCB.
 
TAKUKURU should be disbanded ili Uchaguzi ufanyike kwa amani. Mimi sjaifanya uchunguzi wowote kuhusu Campaign Finance laws,kwa sababu sheria kama hizo hazinihusu mimi,kwa vile mimi sina hela nyingi. Lakini nadhani watu wanaongea kuhusu Campaign Finance reform wanapoona kwamba,from the way things are going,nwisho wake watakaoweza kugombea Uchaguzi ni Bill Gates tu na Warren Buffet.

Lakini kumpeleka mtu mahakani kwa vile ametoa rushwa ya sh. 10,000,this is ridiculuos. Niliponunua kadi ya Chama Cha Mapinduzi miezi michache iliyopita,nilitoa rushwa kama hiyo,I handed out sh.10,000 notes again and again. Kwa sababu unapovaa designer shoes,halafu unamuona mtu mwingine hana kanda mbili,you are compelled to do such things.
 
Mkuu mpaka rushwa iwe rushwa ni lazima ifikie shilingi ngapi? Rushwa ni rushwa tu regardless of its value. Is long as you pay it in return of favours ni rushwa tu.

Lakini swali ni kuwa why Mungai? there is no doubt that many if not all have done the same as Mungai did, why him? Why not others who did exactly as him or even worse?
 
Dah wabongo kwa kumix mambo na hisia ni soo! Yaani hakuna jema! Wasipokamatwa kelele pccb wanakula kodi bure, wakikamatwa pccb wanaleta sanaa! Akikamatwa dagaa oh wanamwonea, akikamatwa papa oh kiini macho, mara rushwa ndogo! Dah kazi kwelikweli!
 
WAZIRI wa zamani katika Serikali ya Tanzania, Joseph Mungai jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa mjini Iringa , kujibu mashitaka ya kutoa rushwa wakati wa kinyang’anyiro cha kura ya maoni katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mungai anakabiliwa na mashitaka 15 ya utoaji rushwa kwa wapiga kura wa CCM wa kata ya Ihalimba katika jimbo la Mufindi Kaskazini.

Imedaiwa kuwa mwanasiasa huyo alitoa rushwa wakati akitafuta ridhaa ya wapiga kura wa CCM wa jimbo la Mufindi Kaskazini ili wamchague kwa mara nyingine kugombea ubunge wa jimbo hilo ambalo ameliongoza kwa miaka mingi.

Katika kura hizo za maoni, Mungai alishika nafasi ya pili kwa Kupata kura 3,430 dhidi ya kura 6,386 zilizompa ushindi Mahamud Mgimwa katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na wagombea sita.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamuunganisha pia Moses Masasi aliyetajwa kwamba ni Mhasibu na Fidel Cholela ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM kata ya Mafinga.

Mungai alikana mashitaka na kurudishwa rumande na watuhumiwa hao wengine kusubiri taratibu za dhama ambapo walihitajika wadhamini wawili kwa kila mmoja.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Mary Senapee, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Prisca Mpeka, alidai kuwa Mungai na wenzake walitoa rushwa kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kata ya Ihalimba waliokuwa na kikao Julai 8, mwaka huu kwenye ofisi ya CCM ya kata ya Ihalimba, ili wampigie kura ya maoni.

Alidai kwamba Mungai na watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa Sh 10,000 kwa Obadia Mtokoma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi la kijiji cha Vikula na Katibu wa Uchumi na Fedha wa tawi la CCM la kijiji cha Vikula, Konjeta Kiyeyeu ambaye pia alihongwa Sh 10,000.

Wengine kwa mujibu wa Mpeka na kiasi cha fedha walichopewa kwenye mabano, ni pamoja na Katibu wa CCM wa Kata ya Ihalimba, Aldo Lugusi (Sh 10,000), Mwenyekiti wa CCM wa Ihalimba, Ezekiel Mhewa (Sh 10,000) na Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Ihalimba, Tulaigwa Kisinda (Sh 10,000).

Wengine ni Jiston Mhagama (Sh 10,000), Maria Kihongozi (Sh 20,000), Lurent Mdaligwa (Sh 5,000), Victory Kalinga (Sh 20,000), Francis Chonya (Sh 2,000) na Alfred Kisinga (Sh 2,000).

Waliohongwa wengine kwa mujibu wa mashitaka, ni Issac Tewele (Sh 2,000), Sosten Kigahe (Sh 10,000), Raphael Lutomo (Sh 10,000) na Andrew Mkiwa (Sh 20,000). Wanakabiliwa na jumla ya mashitaka 15 ya rushwa.

Pamoja na kukana mashitaka hayo, watuhumiwa hao walishindwa kukamilisha kipengele cha dhamana mara moja, na hadi tunakwenda mitamboni walikuwa bado rumande wakisubiri kukamilisha kipengele hicho.

Akitoa masharti ya dhamana kwa watuhumiwa hao, Senapee alisema kila mtuhumiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, na kila mmoja akiwa na Sh milioni tano na mmoja wao lazima awe mkazi wa hapa.

Mpeka alisema pia kuwa mwana CCM mwingine Fredrick Mwakalebela, ambaye naye anatuhumiwa kujihusisha na rushwa wakati wa kampeni hizo Iringa Mjini, atafikishwa mahakamani Agosti 17 mwaka huu, baada ya kushindwa kutokea jana kwa kilichoelezwa kwamba ana udhuru.

Wakati huo huo, Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Iringa, Donasian Kessy aliwaambia waandishi wa habari kwamba katika kesi inayomkabili Mungai wana CCM wanaotuhumiwa kupokea rushwa hizo, watafikishwa mahakamani hapo kama mashahidi kwa sababu ndio walioisadia Takukuru kupata taarifa hiyo.

Kessy alisema pamoja na washitakiwa hao kufikishwa mahakamani alisema suala la kuwaengua kushiriki uchaguzi ni la Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye kabla ya kufanya hivyo ni lazima ajiridhishe na tuhuma.

Alisema pamoja na kwamba Takukuru inatambua kuwa katika kesi hizo kuna kushinda au kushindwa, endapo watashindwa hilo halitakuwa kosa la chombo hicho cha Dola.
 
TAKUKURU should be disbanded ili Uchaguzi ufanyike kwa amani. Mimi sjaifanya uchunguzi wowote kuhusu Campaign Finance laws,kwa sababu sheria kama hizo hazinihusu mimi,kwa vile mimi sina hela nyingi. Lakini nadhani watu wanaongea kuhusu Campaign Finance reform wanapoona kwamba,from the way things are going,nwisho wake watakaoweza kugombea Uchaguzi ni Bill Gates tu na Warren Buffet.
Lakini kumpeleka mtu mahakani kwa vile ametoa rushwa ya sh. 10,000,this is ridiculuos. Niliponunua kadi ya Chama Cha Mapinduzi miezi michache iliyopita,nilitoa rushwa kama hiyo,I handed out sh.10,000 notes again and again. Kwa sababu unapovaa designer shoes,halafu unamuona mtu mwingine hana kanda mbili,you are compelled to do such things.

Du kadi hizi ambazo wenzako walikuwa wanapewa bure wewe umehonga kupata?? Mbona haileweki mkuu?

By the way Ganesh wale jamaa zako walioenda kununua ndege za kijeshi China vp wamerudi, tujulisha basi ili nasi tujidai with our expanded airforce.
 
Hehehe Mzee anatoka kwa aibu with more than 30 years in service! Matunda ya tamaa iliyokithiri ya uongozi.
 
Hakuna wa kuachwa CCM kwenye mambo haya RUSHWA. Waliiacha mwaka 2005 ikatupatia RAIS basi.
 
Mungai na watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa Sh 10,000 kwa Obadia Mtokoma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi la kijiji cha Vikula na Katibu wa Uchumi na Fedha wa tawi la CCM la kijiji cha Vikula, Konjeta Kiyeyeu ambaye pia alihongwa Sh 10,000.

Wengine kwa mujibu wa Mpeka na kiasi cha fedha walichopewa kwenye mabano, ni pamoja na Katibu wa CCM wa Kata ya Ihalimba, Aldo Lugusi (Sh 10,000), Mwenyekiti wa CCM wa Ihalimba, Ezekiel Mhewa (Sh 10,000) na Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Ihalimba, Tulaigwa Kisinda (Sh 10,000).

Wengine ni Jiston Mhagama (Sh 10,000), Maria Kihongozi (Sh 20,000), Lurent Mdaligwa (Sh 5,000), Victory Kalinga (Sh 20,000), Francis Chonya (Sh 2,000) na Alfred Kisinga (Sh 2,000).

Waliohongwa wengine kwa mujibu wa mashitaka, ni Issac Tewele (Sh 2,000), Sosten Kigahe (Sh 10,000), Raphael Lutomo (Sh 10,000) na Andrew Mkiwa (Sh 20,000).

Sasa waliopokea rushwa mbona nao hawajashitakiwa kama sheria invyosema?
 
Pengine wao ndio waliotoa taarifa je. Utamshitaki vipi informer wako?
 
TAKUKURU should be disbanded ili Uchaguzi ufanyike kwa amani. Mimi sjaifanya uchunguzi wowote kuhusu Campaign Finance laws,kwa sababu sheria kama hizo hazinihusu mimi,kwa vile mimi sina hela nyingi. Lakini nadhani watu wanaongea kuhusu Campaign Finance reform wanapoona kwamba,from the way things are going,nwisho wake watakaoweza kugombea Uchaguzi ni Bill Gates tu na Warren Buffet.
Lakini kumpeleka mtu mahakani kwa vile ametoa rushwa ya sh. 10,000,this is ridiculuos. Niliponunua kadi ya Chama Cha Mapinduzi miezi michache iliyopita,nilitoa rushwa kama hiyo,I handed out sh.10,000 notes again and again. Kwa sababu unapovaa designer shoes,halafu unamuona mtu mwingine hana kanda mbili,you are compelled to do such things.

Dah yaani na elimu yako bado hujui nn maana ya rushwa au unajua rushwa lazima iwe laki ndo rushwa?Kuanzia cent na kuendelea hiyo ni rushwa mkuu si unashawishi watu wakutekelezee kila unacho kitaka.
Yaani mkuu na Elimu yako bado ukatoa 10,000/= kupata kadi ya chama cha mafisadi, kweli kazi tunayo kuwaelimisha watu.
 
[ Lakini kumpeleka mtu mahakani kwa vile ametoa rushwa ya sh. 10,000,this is ridiculuos. Niliponunua kadi ya Chama Cha Mapinduzi miezi michache iliyopita,nilitoa rushwa kama hiyo,I handed out sh.10,000 notes again and again. Kwa sababu unapovaa designer shoes,halafu unamuona mtu mwingine hana kanda mbili,you are compelled to do such things.
hahahaha hapa kipi ni ridiculous? wewe ulietoa sh. 10000 kununua kadi? ama pccb? kweli bado tunayosafari ndefu sana.....:becky:
 
Pengine wao ndio waliotoa taarifa je. Utamshitaki vipi informer wako?

Sidhani........wasingepokea kwa kuwa ukipokea tu nawe ni sehemu ya rushwa kwa mujibu wa sheria...shitaka lenywe linasema 'wanadaiwa' na sio 'wamekamatwa' wakitoa rushwa....ni vitu tofauti...la kwanza ni based on hearsay na pili ni reality
 
hahahaha hapa kipi ni ridiculous? wewe ulietoa sh. 10000 kununua kadi? ama pccb? kweli bado tunayosafari ndefu sana.....:becky:

Hahahaha naona jamaa hiyo 10,000 anaona pesa ndogo wakati trafic hata buku 1 wanapokea ambayo nayo ni rushwa
 
tukukuru na silikali yao wanacheza usani tu hapa, kuna rushwa kubwa kubwa za richmond, na nyingine nyingi tu wameziacha, sasa uchaguzi unakuja na watu wamekosa imani na silikali, ndio wanajidai wamejipanga, kwanza tunajua hii ni danganya toto uchaguzi ukipita wembe ni ule ule, na zaidi ya hpo ra akishinda, ana madaraka ya kumsamehe mtoa rushwa baada ya hukumu. hivyo wanaweza mwambia JMunga we ka huko baada ya erection tunakutoa.
 
Back
Top Bottom