Elections 2010 Mungai apandishwa kizimbani kwa rushwa

SHUPAZA

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
562
23
Waziri wa zamani Joseph Mungai amepandishwa kizimbani kwa kosa la 'kuchakachua' kwenye kura za maoni za CCM.

Source: TBC1 Habari
 
Hahaha Kiongozi sio wote wanaelewa hilo neno la kuchakachua kura za maoni! Eleza tu kwa uwazi kwamba amepandishwa kizimbani kwa kosa la kutoa rushwa ili kuwashawishi wananchi wampitishe kura za maoni!
 
Nimeipenda hii ya kuchakachua. Kumbe maana yake ndiyo hiyo? Asante JF
 
Nimeipenda hii ya kuchakachua. Kumbe maana yake ndiyo hiyo? Asante JF
Maana yake inaweza kubadilika kutokana na.mwandikaji anamaanisha nn! Maana sa ingine kuchakachua kura inamaanisha kubadili matokeo ya kura za maoni!
 
Kwani ni Mungai tu? Na wengine vipi? au ndo wanataka kuwaziba watu midomo?
 
nchi ya wasanii hii, kwani hakuna wengine wenye makesi huko mahakama kuu juu ya ubadhirifu?mbona wamepita? hata hii itaisha kiaina tukiambiwa hakuna ushahidi wa kutosha hivyo mshtakiwa hana hatia
 
ru9slg.jpg

Si mchezo
 
List ya wanaostahili kupandishwa kizimbani
1. January makamba
2. Rostam Aziz
3. Amos Makala
4.
5.
.
.

Invisible

huu ndiyo ule wakati wa kuweka ule ushahidi wa video ulioahidi kuuweka kama wataofikishwa watakuwa ni hawa tu wasiokuwa close allies wa muungwana
 
Habari kupitia blogu ya Francis Godwin inasema kuwa, Aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu Tanzania, bw. Joseph Mungai pamoja na na wapambe wake wawili, Moses na Fidelis ambaye ni katibu wa UVCCM kata ya Mafinga, leo wamesomewa mashtaka 15 yanayohusiana na tuhuma za rushwa kufuatia uchaguzi ulioisha hivi karibuni wa kuwapata wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania.

Bwana Mungai na wenzake walitakiwa kudhaminiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja na wadhamini wawili ambapo mmoja anapaswa kuwa mkazi wa Manispaa ya Iringa, lakini kutokana na kushindwa kutimiza masharti hayo, iliwabidi kuwekwa chumba cha mahabusu, kama inavyoonekana pichani.

Awali, iliripotiwa leo asubuhi kuwa Donatian Kessy wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, alisema taasisihiyo itawafikisha mahakamani Bwana Joseph Mungai na Frederick Mwakalebela kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Mary Senapee, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Prisca Mpeka alisema Mungai pamoja na Moses Masasi na Fidel Cholela ambao wameunganishwa katika mashitaka hayo, wanashitakiwa mahakamani hapo kwa kukiuka Sheria ya Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 kipengele cha 1b pamoja kifungu namba 21 sehemu ya kwanza A na kifungu namba 24 sehemu ya nane vya Sheria ya Gharama za Uchaguzi Namba 6 ya mwaka 2010.

Alisema katika tukio lililotokea Julai 8, 2010 katika kata ya Ihalimba, Mungai na watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa Sh 10,000 kwa Obadia Mtokoma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi la kijiji cha Vikula kama kishawishi ili apigiwe kura za maoni.

Wengine kwa mujibu wa Mpeka na kiasi cha fedha walichopewa kwenye mabano kwa lengo la kumpigia kura Mungai siku ya kura za maoni za CCM ni pamoja na Katibu Uchumi na Fedha wa tawi la CCM la kijiji cha Vikula, Konjeta Kiyeyeu (Sh 10,000), Katibu wa CCM wa Kata ya Ihalimba Aldo Lugusi (Sh 10,000), Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Ihalimba Ezekiel Mhewa (Sh 10,000), Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Kata ya Ihalimba Tulaigwa Kisinda (Sh 10,000), Jiston Mhagama (Sh10,000), Maria Kihongozi (Sh20,000), Lurent Mdaligwa (Sh 5,000), Victory Kalinga (Sh 20,000), Francis Chonya (Sh 2,000) na Alfred Kisinga (Sh 2,000), Issac Tewele (Sh 2,000), Sosten Kigahe (Sh10,000), Raphael Lutomo (Sh 10,000) na Andrew Mkiwa (Sh 20,000).

Mpeka alisema Mungai na watuhumiwa hao wawili Masasi ambaye ni Mhasibu na Cholela ambaye ni Katibu wa Umoja wa UVCCM Mafinga walitoa rushwa hizo kwa wanaCCM hao wakati wakifanya kikao chao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika katika ofisi ya CCM ya kata ya Ihalimba Julai 8, mwaka huu ili wampigie kura za maoni Mungai na hivyo kufanya jumla ya mashitaka ya rushwa dhidi yao kuwa 15.

Hata hivyo katika kura hizo za maoni, Mungai alishika nafasi ya pili kwa kuambulia kura 3,430 dhidi ya kura 6,386 zilizompa ushindi Mahamud Mgimwa katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na wagombea sita.

Mpeka alisema Fredrick Mwakalebela ambaye naye anatuhumiwa kujihusisha na rushwa wakati wa kampeni hizo katika jimbo la Iringa Mjini, atafikishwa mahakamani hapo Agosti 17 baada ya kushindwa kutokea leo kwa kile kilichoelezwa kwamba ana udhuru.

Chanzo: wavuti.com
 
Wapinzani inabidi wawe makini sana kuna hatari ya kubambikiwa kesi na TAKUKURU, hasa hasa sehemu ambazo wataonekana kuwa na nguvu. Kwani watu kama kina RM na wengine wasifikishwe mahakamani na wao...naye MWAKALEBELA....naona wanafanya targeting ili watu wengine watupwe nje hata kama walishinda kura za maoni...
 
Tatizo la Wabunge wetu hawakujua kwamba walijitungia kitanzi, Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010!
 
Habari kupitia blogu ya Francis Godwin inasema kuwa, Aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu Tanzania, bw. Joseph Mungai pamoja na na wapambe wake wawili, Moses na Fidelis ambaye ni katibu wa UVCCM kata ya Mafinga, leo wamesomewa mashtaka 15 yanayohusiana na tuhuma za rushwa kufuatia uchaguzi ulioisha hivi karibuni wa kuwapata wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania.

Bwana Mungai na wenzake walitakiwa kudhaminiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja na wadhamini wawili ambapo mmoja anapaswa kuwa mkazi wa Manispaa ya Iringa, lakini kutokana na kushindwa kutimiza masharti hayo, iliwabidi kuwekwa chumba cha mahabusu, kama inavyoonekana pichani.

Awali, iliripotiwa leo asubuhi kuwa Donatian Kessy wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, alisema taasisihiyo itawafikisha mahakamani Bwana Joseph Mungai na Frederick Mwakalebela kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Mary Senapee, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Prisca Mpeka alisema Mungai pamoja na Moses Masasi na Fidel Cholela ambao wameunganishwa katika mashitaka hayo, wanashitakiwa mahakamani hapo kwa kukiuka Sheria ya Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 kipengele cha 1b pamoja kifungu namba 21 sehemu ya kwanza A na kifungu namba 24 sehemu ya nane vya Sheria ya Gharama za Uchaguzi Namba 6 ya mwaka 2010.

Alisema katika tukio lililotokea Julai 8, 2010 katika kata ya Ihalimba, Mungai na watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa Sh 10,000 kwa Obadia Mtokoma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi la kijiji cha Vikula kama kishawishi ili apigiwe kura za maoni.

Wengine kwa mujibu wa Mpeka na kiasi cha fedha walichopewa kwenye mabano kwa lengo la kumpigia kura Mungai siku ya kura za maoni za CCM ni pamoja na Katibu Uchumi na Fedha wa tawi la CCM la kijiji cha Vikula, Konjeta Kiyeyeu (Sh 10,000), Katibu wa CCM wa Kata ya Ihalimba Aldo Lugusi (Sh 10,000), Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Ihalimba Ezekiel Mhewa (Sh 10,000), Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Kata ya Ihalimba Tulaigwa Kisinda (Sh 10,000), Jiston Mhagama (Sh10,000), Maria Kihongozi (Sh20,000), Lurent Mdaligwa (Sh 5,000), Victory Kalinga (Sh 20,000), Francis Chonya (Sh 2,000) na Alfred Kisinga (Sh 2,000), Issac Tewele (Sh 2,000), Sosten Kigahe (Sh10,000), Raphael Lutomo (Sh 10,000) na Andrew Mkiwa (Sh 20,000).

Mpeka alisema Mungai na watuhumiwa hao wawili Masasi ambaye ni Mhasibu na Cholela ambaye ni Katibu wa Umoja wa UVCCM Mafinga walitoa rushwa hizo kwa wanaCCM hao wakati wakifanya kikao chao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika katika ofisi ya CCM ya kata ya Ihalimba Julai 8, mwaka huu ili wampigie kura za maoni Mungai na hivyo kufanya jumla ya mashitaka ya rushwa dhidi yao kuwa 15.

Hata hivyo katika kura hizo za maoni, Mungai alishika nafasi ya pili kwa kuambulia kura 3,430 dhidi ya kura 6,386 zilizompa ushindi Mahamud Mgimwa katika kinyang'anyiro hicho kilichokuwa na wagombea sita.

Mpeka alisema Fredrick Mwakalebela ambaye naye anatuhumiwa kujihusisha na rushwa wakati wa kampeni hizo katika jimbo la Iringa Mjini, atafikishwa mahakamani hapo Agosti 17 baada ya kushindwa kutokea leo kwa kile kilichoelezwa kwamba ana udhuru.

Chanzo: wavuti.com
Hivi TAKUKURU hawana kitu tunaita kwenye Audit "Materiality" Hivi kweli hivyo vipesa ambavyo hata laki moja havifiki vinajustfy kuitwa rushwa, kweli ni material kumerits kesi?. Hii sio ile takrima aliyoitetea kikwete, hivi kweli shs 10 za kitanzania zitafanya nini. Waliosoma Taxation wanajua ile principle ya cost effectiveness, kwamba gharama za kukusanya kodi lazima ziwe ndogo kuliko kodi inayokusanywa. Gharama za kuendesha kesi ya rushwa lazima ziwe ndogo kuliko madhara na faida itakayopatikana. Kwa kumshitaki Mungai serekali inafaidika na nini, afterall alishashindwa. Hiyo kesi ya laki moja itatumia resources kiasi gani za nchi hii. TAKUKURU, be serious na kesi kama hizo hazina manufaa kwa mtanzania. Na je mbona aliyepokea rushwa hajafikishwa mahakamani, nijuavyo mimi aliyetoa na aliyepokea rushwa wote wana makosa. Sijaona kama kina Kiyeyu sijui na Mdaligwa etc, waliopokea hiyo rushwa wakiunganishwa katika kosa, au walikuwa undercover agents"

Hii kesi haina merits na Mungai atashinda, nadhani ni kutapatapa kwa CCM ili kuwazuga wadanganyika, afterall Mungai alishaloose, what is he for anyways, kuloose is enough punishment. Wale waliokamatwa kwa rushwa na kushinda mbona hawajafikishwa mahakamani, hivi kweli TAKUKURU wako serious. To me Tanzania is a safer place without TAKUKURU.

Na je rushwa ni fedha (monetary) tu, hiyo sheria haibainishi rushwa nyingine kama ahadi hewa, ngono, ukabila etc. Muungwana alivyojaza washikaji wake kwenye serekali sio rushwa hiyo?-- ethics?

Mungai pole, umetumiwa kama chambo, fight to prove them wrong, TAKUKURU wanafunika uozo wa rushwa. Rushwa haichunguzwi kihivyo, eti elfu mbili, come on, now be serious. Mpiga kura akiomba shs 2000 za kununua kilo ya sukari kwa mgombea tayari ni rushwa hiyo ya kuweza kubadili matokeo?

Simtetei Mungai, but nashangaa kama kweli hizo takrima ndogo ndogo hizo zinamerits kuiingiza serekali kwenye gharama kubwa ya kuendesha kesi.
 
Huo ndo ujanja wa CCM, wanamtoa kafala mmoja ili wapate cha kuongelea wakati wa kampeni. Mbona kuna wezi wa mali ya umma kama wanaodaiwa wamerudisha pesa za EPA lakini serikali haijawachukulia hatua yoyote?
 
Hhmmm....why do I have a sneaky suspicion that this is just a facade...? Is he really going to face the music? And why now - two and a half months out from the vote?

I'm gonna go out on a limb and say this is just a another one of those perception v. reality efforts that I expected to see ahead of the election in order to hoodwink the hoi polloi....
 
Back
Top Bottom