Mumewangu ndio chanzo cha mimi kuwa na uhusiano nnje ya ndoa!

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Imenukuliwa kutoka katika utafiti wa 'saidia jamii'....
*****************************************************************

Suala la nyumba ndogo halipo kwa wanaume tu hata wanawake pia tunalo! Hii inatupunguzia stress tuzipatazo kwa waume zetu! ikiwa ni pamoja na kunyimwa uroda mara kwa mara kwani wanaume walio wengi wakishajichapia nje basi hawawajali wake zao! Kwahiyo wanawake nao huamua kujitafutia vijana ili wawe wanajipongeza! Mzee akienda zake nje na mama naye anatoka kwenda kujipongeza. Mwisho wa siku ni ngoma droo!

************************
Mimi na mumewangu tumekuwa katika ndoa kwa muda wa miaka 15 sasa. Kuna wakati mumewangu alianza kuwa na uhusiano na msichana fulani (jina kapuni) na nilipogundua yule binti alinijia juu na kusema kwamba mimi simfikishi kokote 'buzi' lake (mumewangu)!!!

Nilivumilia sana lakini mumewangu alikuwa akirudi amelewa na wakati mwingine harudi siku 2-3, hasa wakati wa mwisho wa wiki! Mumewangu alipoteza kabisa hamu ya kufanya tendo la ndoa na mimi! Niliumia sana mpaka siku moja nilipkwenda kufanya manunuzi ya vitu vya ndani sokoni kariakoo! Nilikutana na 'kijana' mmoja mtanashati katika duka wanalouza nguo na viatu! Kijana huyo alinisemesha kwa maneno matamu na mwisho wa yote tuliagana na kupeana namba za simu!

Baada ya siku kama 3, kijana huyo alinipigia simu na kunijulia hali! Ikawa ndiyo kawaida yake kupiga mara kwa mara kwani mzee wangu si 'hayupo'.... Nilianza kuvutiwa na kijana na siku aliponitamkia kwamba anaomba twende nje kwa ajili ya chakula cha jioni (dinner) nikawa sina pingamizi!

Baada ya muda kama wa mwezi mzima nikatokea kumpenda sana huyo kijana na hali yangu ilibadirika kabisa nikawa na furaha hata mumewangu akirudi nyumbani au asiporudi mimi sina wasiwasi kwani kabla sijalala nitaongea na mtu ambaye anayenijari!

Mwisho wa siku aliponitamkia kwamba anaomba nimtembelee kwake sikusita kwani niliona ndio wakati mwafaka wa 'kujuana' vizuri! Na mambo yalienda hivyo kama unavyofikiria! Nina amani na sina hata haja ya mumewangu!

Sasa imeshafika miaka mi 2 mimi na mumewangu hatujawahi kulala kitanda kimoja kwani yeye akirudi amelewa na anarudi usiku sana! Na hata akirudi anakuwa ameshamalizana huko kwa nyumba ndogo yake!

Wito: Enyi waume wapendeni wake zenu na jitahidini kuheshimu ndoa zenu kwani nyie ndio chanzo cha sisi wanawake kutoka nje ya ndoa! Kama wewe hunitimizii mahitaji yangu....unataka nifanyeje? Nibaki nateseka wakati kuna watu weeeeeeeengi kama wewe?
 
Duh! haya bana.
Sasa kajamaa kakitaka kuoa utakuwa nyumba ndogo yake?
Au utatafuta serengeti boy mwingine!!
 
eeeh hiki kisanga mheshimiwa Buchaman aje atoe ushauri hapa ni ngumu lakini duh
Masaki una la kusema ?
 
Kwa hiyo ni JINO kwa JINO.. Mwisho wake ni wote kuleta kaugonjwa ndani.. Nakushauri achana na huyo Mtu.. mvumilie mumeo.. siku moja atajirudi.. Na inawezekana wewe ndio ulikuwa chanzo cha yeye kwenda nje..
 
Kwa hiyo ni JINO kwa JINO.. Mwisho wake ni wote kuleta kaugonjwa ndani.. Nakushauri achana na huyo Mtu.. mvumilie mumeo.. siku moja atajirudi.. Na inawezekana wewe ndio ulikuwa chanzo cha yeye kwenda nje..
what about her feelings
 
Fix-there is no truth in it!!!!!!!!!

Mkuu unaishi BONGO kweli? yaani sasa hivi ni kitu ipo sana, wanawake wengi wanateseka sana kwenye ndoa zao, wakiwa wao kwa wao wanashauriana, kwa nini uteseke na wewe tafuta wa kukupoza, siku hizi ukimchezea shere tu mkeo, akigundua tu na yeye anatafuta wa kummega, chunga sana kamanda
 
Mlete mmeo hapa nae atoe story yake
Utakuta na yy ulimchosha vile vile akaamua kusepa mdogo mdogo!!
 
Nilikutana na 'kijana' mmoja mtanashati katika duka wanalouza nguo na viatu! Kijana huyo alinisemesha kwa maneno matamu na mwisho wa yote tuliagana na kupeana namba za simu!
Huyo kijana na wewe mnawiana vipi kiumri, je kakuzidi au umemzidi? Kama kakuzidi (??????????????????)
 
si kweli wanaume ndo chanzo cha wake kutafuta serengeti boy no i say no and i mean it no question
 
Mimi na mumewangu tumekuwa katika ndoa kwa muda wa miaka 15 sasa. Kuna wakati mumewangu alianza kuwa na uhusiano na msichana fulani (jina kapuni) na nilipogundua yule binti alinijia juu na kusema kwamba mimi simfikishi kokote 'buzi' lake (mumewangu)!!!

Kwa nini usingefanyia kazi kwanza hiyo statement alafu ungeona mambo hayabadiliki ndo ungefanya uamuzi wa kuwa na KISERENGETI!!!
 
... mwisho wa yote utakuwa ni mbaya ... jaribuni kurekebisha kasoro ya ndoa yenu coz so far hakuna ndoa hapo!!
 
Suala la nyumba ndogo halipo kwa wanaume tu hata wanawake pia wanalo! Hii inawapunguzia stress wazipatazo kwa waume zao! ikiwa ni pamoja na kunyimwa uroda mara kwa mara kwani mwanaume akishajichapia nje basi hamjali mkewe! Kwahiyo wanawake nao uamua kujitafutia vijana ili wawe wanajipongeza! Mzee akienda zake nje na mama naye anatoka kwenda kujipongeza. Mwisho wa siku ni ngoma droo!

For sure wote wataambukizana Virus vya Ukimwi au Magonjwa ya zinaa na NGOMA itakuwa Droo!
 
eeeh hiki kisanga mheshimiwa Buchaman aje atoe ushauri hapa ni ngumu lakini duh
Masaki una la kusema ?
FL1, kila jambo huwa lina chanzo chake. Hata mbuyu ulianza kama mchicha baadaye likawa jimti kubwa ajabu! Kuna mahali fulani kwa pande zote mbili nati zilianza kulegea hadi chombo yalianza kwenda mrama! The "first love" grew colder and colder until it went off!
Mimi naamini kwamba "two wrongs can not make a right!" Kwa hiyo siamini kwamba jino kwa jino ndio suluhisho, umeongeza tatizo juu ya tatizo! Watu wengi wanapenda kutatua matatizo ya muda mfupi (eg nyumba ndogo, etc) na kujifanya hawaoni matatizo yanayozunguka hilo "suluhisho" la muda!
Kama unamwamini Mungu, timiza sehemu yako katika ndoa, without any qualification or excuse, mwache mwenzako atimize sehemu yake!
Mwisho: Furaha ya kweli inatokana na kufuata Mapenzi ya Mungu, sio kwa kuwa na fedha na mali nyingi, kwani "Wamejaa amani nyingi waishikao Sheria ya BWANA!"
Pape, acha kwenda nje ya ndoa, eti kwa sababu unatimiziwa haja yako ya muda! Unalea bomu, likija kulipuka utakuja kujuta, it will be too late for sure! Tafuta njia ya kutengeneza ndoa yako badala ya kuchangia katika kuivunja. "Alichokiunganisha Mungu, Mwanadamu asikitenganishe!"
 
Acha kwenda nje ya ndoa, eti kwa sababu unatimiziwa haja yako ya muda! Unalea bomu, likija kulipuka utakuja kujuta, it will be too late for sure! Tafuta njia ya kutengeneza ndoa yako badala ya kuchangia katika kuivunja. "Alichokiunganisha Mungu, Mwanadamu asikitenganishe!"
well noted!
 
Back
Top Bottom